Ufafanuzi: Kwanini tuliona Lissu anafaa urais 2020 na sasa hafai Uenyekiti?

Nani kasema apite bila kupingwa? Nilichosema Mbowe akijitoa watu wengi sana watachukua fomu na ndio tutaona demokrasia ya kweli ikifanya kazi. Imagine uenyekiti wachukue fomu watu 10 zifanyike primaries majimbo yote 10 ya chama mpaka tupate mwenyekiti mmoja tu!! Ila Mbowe akigombea watu watahofia retaliation baada ya uchaguzi na kuitwa wasaliti
 
I agree 100% you have a valid points.

Mbowe anahitaji kuandaa successor, not only that anahitaji kuweka mfumo imara zaidi wa democracy ndani ya chama.

Lakini Lissu sio mtu mwenye uwezo wa kujenga chama, he is not leadership material.

My personal opinion sio lazima kila mtu akubaliane na mimi; Wenje, Mnyika na Lema wanaweza kuwa replacement nzuri ya mwenyekiti, makamu na katibu mkuu.

Not Lissu he is too emotional.
 
Kwanini Mbowe AJITOE? Anawazuiaje hao WENGI kuchukua fomu?

Lisu kachukua fomu, Mbowe alimzuia, au unaushahidi kuna waliozuiwa na Mbowe kuchukua fomu kugombea uwenyekiti chadema?

Hata yangekuwa majimbo 100 ya uchaguzi, wagombee hata watu 200 ni sawa na ndiyo demokrasia tuitakayo.

Hiyo wasiwasi ya retaliation baada ya uchaguzi unaitoa wapi wewe, au ndiyo yale maneno tunayoambiwa kila siku kwamba taarifa za intelligensia?

Acheni visingizio, na kumsingizia Mbowe visivyokuwepo.

Hata wewe kagombee kama una nia, nahakika HAKUNA retaliation yoyote!
 
Je JPM alikua ni leadership material? Let's be honest. Yes alifanya mengi (Utendaji 100%) ila kwenye leadership sidhani kama Lissu can do worse than JPM yet ni cult hero kwa wengi.
You can’t compare the two.

Magufuli alikuwa kiongozi na zaidi.

For starters he was a visionary ya Tanzania anayoitaka; kiuchumi na mwenendo wa civil services.

Kwenye uchumi you know uwezi kukopa private banks kama IFM/WB wanaona cash flow yako sio nzuri.

Na miradi aliyoanza Magufuli lengo kubwa ilikuwa ni kufungua access za maeneo ya uzalishaji ambayo aijachangamka. Wakati watu hawana hela ya kununua kilo ya mchele Dar, Ruvuma wakulima mchele ulikuwa unawaozea kwa sababu wafanyabiashara wanataka kununua Morogoro tu.

Sasa you can not do that bila ya infrastructure.

Same haya mabazazi ya civil services, acha tu (ndio wananyofoa kucha wenyewe) utaki kuwaongelea.

Magufuli was special, kazi ya kuwabadili watu tabia sio rahisi (it’s the reason wazungu wanafundisha module ya ‘change management’) people don’t like changes hiko ndio kisiki cha Magufuli. He did not make his work easy maana na yeye nae alikuwa na ushamba wake.

Lakini Lissu hatoshi hata kwenye kiganja cha mkono wa Magufuli. Tanzania ilikuendelea eventually lazima apatikane Magufuli mwengine au civil services ipate katibu mkuu na DGIS imara.

Vinginevyo hadithi.
 
Kupitia pumba ulizoandika hapa, unatuthibitishia CDM nzima hakuna mwenye sifa ya kua mwenyekiti zaidi ya mbowe?

MACHAWA WA MBOWE HAMNA AKILI.
 
Now i can tell you, Sir Mbowe will lead this party until CCM comes out of power and then its mission will be completed….
Kwahiyo chadema nzima yenye wanachama 6M+ ( kwa mujibu taarifa zenu), mwenye sifa za kugombea uenyekiti ni Mbowe peke yake?

Kwann chadema kama taasisi isiwajengee uwezo wanachama wengine ili kuwe na succession plan ya uenyekiti?

Wale wanaosema Yericko Nyerere ni mlamba viatu wa Mbowe, Yericko Nyerere ni Kupe anayefaidi damu (fedha) ya Mbowe utawapinga vipi kama haya ndiyo mawazo yako?

Basi na ccm isiondoke madarakani. Chadema mpo kwa ajili ya nn ili hali hamna sifa ya kutawala nchi hii?
 
Maandiko km haya unaendelea kujidhalilisha tu . sidhani km watanzania watakubeba tena kwenye tuzo zako za mchongo.
 
Kwahiyo Mbowe akifa usiku huu na CHADEMA ndio inakuwa imekufa?!

Chama gani sasa cha hivyo?! Si bora tukalime tu.

Alamsiki.
Uchaguzi wa Chadema huwa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, hivyo Mbowe akifa leo, basi Makamu ataongoza chama
 
Maandiko km haya unaendelea kujidhalilisha tu . sidhani km watanzania watakubeba tena kwenye tuzo zako za mchongo.
Umepata wapi kibali cha kuwasemea watanzania huku ukiwa umelala sebuleni kwa dada yako na unachati kwa bando la singesha kijana?
 
CHAWA WA MBOWE.... DOGO UTAAIBIKA. CHAWA PRO MAX
 
Nimeelewa kwanini familia ya Baba wa taifa ilipiga marufuku wajanjawajsnja kutumia hilo jina ili kulinda legacy ya jina dhidi wa ugoro
 
Mkuu Lissu hatakiwi awe Mwenyekiti kwa sababu makubaliano yasiyo rasmi ya Mbowe kuachiwa gerezani ni pamoja na mambo mengi, kumpa Mwenyekiti wa chama tawala free pass kwenye tiketi ya urais kwenye uchaguzi ujao.

Lissu kuwa Mwenyekiti wa Chadema ni threat zaidi kwa uongozi dhaifu wa CCM, katiba yetu mbovu na muungano wa Tanzania usio wa haki.

Infact Lissu huwa haropoki ila watawala wanajua fika hawawezi kumshinda kesi kwa kutumia kauli yake. Uongozi wa chama tawala unaukukumbuka mziki wa Lissu dhidi ya Magufuli kwenye uchaguzi uliopita mpaka Magufuli akaamua aweke mpira kwapani liwalo na liwe.

Mbowe has been so much compromised to go against the above, as a result Chadema is deeply stuck.

Hicho ndicho hakisemwi na chama tawala au na Mbowe & co.!!!
 
Mahaba niue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…