Lakini nadhani haya ni mafikirio tu, kwani ccm wanahitaji ruhusa ya Mbowe kuendelea kutawala? Tangu lini?Mkuu Lissu hatakiwi awe Mwenyekiti kwa sababu makubaliano yasiyo rasmi ya Mbowe kuachiwa gerezani ni pamoja na mambo mengi, kumpa Mwenyekiti wa chama tawala free pass kwenye tiketi ya urais kwenye uchaguzi ujao.
Lissu kuwa Mwenyekiti wa Chadema ni threat zaidi kwa uongozi dhaifu wa CCM, katiba yetu mbovu na muungano wa Tanzania usio wa haki.
Infact Lissu huwa haropoki ila watawala wanajua fika hawawezi kumshinda kesi kwa kutumia kauli yake. Uongozi wa chama tawala unaukukumbuka mziki wa Lissu dhidi ya Magufuli kwenye uchaguzi uliopita mpaka Magufuli akaamua aweke mpira kwapani liwalo na liwe.
Mbowe has been so much compromised to go against the above, as a result Chadema is deeply stuck.
Hicho ndicho hakisemwi na chama tawala au na Mbowe & co.!!!
Hata Lisu akiwa Mwenyekiti, tutarudi humu humu JF kulalamika kivingine baada ya uchahuzi 2025.
Watasema Mbowe kamuhujumu Lisu, kwasababu chadema visingizio vimejaa, huwa vinasubiri muda tu vitolewe.
NChi hii hatufanyi uchaguzi, huwa tuna halalisha mtu aendelee kuwa madarakani kwa jina la demokrasoa za uchaguzi.
CCM sio wehu, wanafahamu hawashindi uchaguzi wowote, hivyo ili jamii za kimataifa waridhike, inabidi twende studio tuigize, na waone tumefanya uchaguzi. Na sterling (ccm) hauwawi.
Lisu ashinde, sawa lakini tupunguze promo, uchaguzi utaisha chadema iko hoi sana. Na haitakuwa chadema hii tuijuayo, utanambia muda huo ukifika.