Ufafanuzi: Kwanini tuliona Lissu anafaa urais 2020 na sasa hafai Uenyekiti?

Lisu ni Mwiba kwa Serkali dharim pia ni dawa ya vyama vibovu vibovu hivyo matokeo ni mawili tu aidha CDM Ibadilike na kuleta upinzani wa kweli au ife kabisa uwe mwisho wa upinzani wa kinafiki.
Najua chini a Lisu CDM itapitia ban nyingi sana toka kwa Serkali ya CCM na iko ndicho baadhi ya wanaCDM wenye manufaa yao binafs wanachoogopa.
Kina Bonyai na Mawinga wote wa Mbowe wanalinda Maslahi yao Wapuuzwee, Lisu ni Tiba ya CDM na Mchawi wetu hataki kusikia habari ya Mganga.
 
Yeriko, umesema unatoa elimu juu ya maidhaifu ya Lisu? Hiyo ni elimu au ndio umetumwa na mbowe? Actually ww haupo kwa masilai ya CHAMA,upo kwa ajili ya Mbowe, ww kama mwandishi wa vitabu vy kijasusi, na siasa hapa ndo ulikuwa uwanja wako wa kuonesha uwezo wako wa kuchambua mambo ya kisiasa ndani ya chadema.
Mm napata shida kuona wewe unaegemea upande mmoja wa Mbowe? Sijui kama unajua unavyozidi kumtetea Mbowe ndivyo thamani yako ya kuwa mwandishi inashuka?
Watanzania na wanachadema wategemea ww uwachambue vizr kabisa in and out Mbowe na Lisu, kwa kuangalia mazingira ya siasa za Tanzania za sasa, mahitaji ya watanzania kwa sasa, utekaji, mauwaji, ufisadi, wambie watanzania mazuri ya Mbowe, na mabayake ,mazuri ya Lisu na mabaya yake, Kazi ibaki kwa wapika kura ndio waamua yupi atatuvusha kwa sasa. Ww umeonyesha (umbowelism). What if Lisu akishinda au let say Mbowe hagombei, na Lisu amekuwa mwenyekiti utaenda kujificha wapi? Maana unamponda Lisu wakati Mbowe hajasema chochote. Najua ww ni state intelligent ya Mbowe unajua Mbowe anagombea. But time we will tell the truth.
 
Mbona kila siku tunaambiwa kuhusu mapungufu ya Mbowe ? Mfuasi wa Mbowe ni lazima ataamini kuwa bila yeye CDM itayumba. Hivyo hivyo mfuasi wa mtu mwingine ataamini kuwa panahitajika damu mpya ili CDM iendelee kuthaminiwa na hatimae kuchukua dola. Wote hao watafanya kila juhudi kuonyesha mapungufu ya wenzake wanaoshindana nae. Wanachama na wale wenye dhama watawapima na kumpigia kura yule anayeonekana anawafaa. Ndio siasa. Kitu muhimu ni kuhakikisha kuwa watu hawachafuani kiasi cha kushindwa kufanya kazi pamoja baada ya uchaguzi. Wagombea wote ni watu muhimu sana kwa chama chao.

Amandla...
 
Hoja zao ni nzito sana kuliko uwezo wa wako wa kuchanganua mambo.
Sasa hapa ndiyo umeandika nini? Kwa kuwa urais ni unpredictable ndiyo maana hampo serious nao? Ndiyo maana mnachagua mtu asiye na uwezo ili akagombee kwa tiketi ya Chamma?

Wewe huna uwezo wa kumfundisha yeyote siasa, hata kujifundisha mwenyewe haufai.

Kwa hiyo, kwa kuwa urais ni unpredictable, so nafasi nyingine kama za ubunge na nyingine zote za kugombea huwa ni unpredictable ndiyo maana huwa hampo serious nazo na hata tuhuma kwamba mnaenguliwa kwa kutojaza vizuri form ni za kweli sababu nyi lengo lenu kubwa ni kujenga Chama na si kushinda chaguzi za nje ya Chama?
Hata tuhuma za kuibiwa kura maana yake leo unatwambia huwa si za kweli .

Kwani hadi sasa mnapojiita na kuitwa Chama kikuu cha upinzani huwa ni kigezo gani kinatumika? Siyo ushindi ambao hupatikana kupitia chaguzi mbalimbali za nje ya Chama?

Hivi unajisikiliza kweli kabla ya kuandika au vitu vinajiandika vyenyewe?
Kwamaoni yangu Lissu hana sifa na ubora wa kuongoza chama kulingana na mapungufu yake mengi sana ambapo mengine niliyaeleza katika makala ile,
Tafadhali tuonyeshe hayo mapungufu yake. Katika yale Makala yako hakuna ulichoweza kuonyesha zaidi ya kurukaruka na kuleta visa vya kubuni

Kama kuna wapambe wa dola, utakuwa ni mwendawazimu kusema na kujaribu kuaminisha watu kwamba Lissu ni Mpambe wa Dola kuliko Mbowe. Tnamheshimu Mbowe, ila kwa jinsi wapambe wake mnavyokuja itabidi mkabiliwe kwa namna hiyo mliyokuja na hapo haitajalisha nani ataathirika vipi. Si mnajifanya hamnazo? Endeleeni kuja hivyohivyo.
Dola inatulazimisha tufanye kosa la karne kwa kumuondoa Mbowe ili wao wanywe mvinyo kwa furaha pale Mbweni na Viunga vyake! Hatutafanya kosa hilo, sahauni kabisa!
Dola gani inayoshirikiana na Lissu kumuondoa Mbowe wakati kama tutaamua kuichukua hoja kipumbavu kamnavyoibeba basi ukweli ni kinyume chake. Ukweli uliopo ni Mbowe aliyechomolewa gerezani kimezengwe akiwa anakabiliwa na kesi ngumu, na alichomolewa na dola hiyohiyo unayoisema halafu pasipo kushinda kesi akabebwa kutoka gerezani na kupelekwa moja kwa moja Ikulukuonana na rais. Baada ya hapo Chama kikaingizwa kwenya maridhiano ya kipumbavu kabisa ambayo yalipelekea kukipoteza mazima.
Lissu huyuhuyu alionekan ndiye pekee aliyeyapinga maridhiano yale, akapiga kampeni ngumu na kali huku Mbowe akipiga kampeni za kuyasifu kabla baadaye na yeye kuungana na Lissu.
Kisu hakionjwi kwa ulimi!
Sijui ingekuwa Lissu ndiye ametolewa gerezani pasipo kushinda kesi mngekuwa mnasema nini leo, ingekuwa Lissu pasipo Chama chake kujua ndiye ametolewa gerezani na kupelekwa moja kwa moja Ikulu naamini mngemaliza yote kwa kuandika.
Wale COVID19 ingekuwa ni chini ya uongozi wa Lissu, kwa kwelli hadi nyimbo mngetunga na ku record albam kabisa
 
Una udhaifu wa kudhani ukiweka maneno ya kiingereza kwenye maelezo yako ndio yatafanya usemacho kuwa bora, ama kwa mtazamo wako hiyo ndio akili😂 Nasisitiza kuwa Magufuli hakuwa kiongozi mzuri, kiongozi mzuri ni yule anayefuata katiba itakavyo, sio atakavyo yeye. Na Magufuli hakuwa mfuata katiba bali mpenda sifa. Unaweza kuweka maneno ya kiingereza ili kuongeza mikogo kwenye utetezi wako, na kufanya mahaba yako kuwa ndio akili, lakini habari ndio hiyo.
 
Mwaka wa 20 Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA, hiyo ni mali yake binafsi inayomuingiza utajiri.
 
Uchanga wa Lissu ni upi? Ni wapi Lissu ameshambulia wenzake?
 
State intelligent ndio nini?

Hauoni wewe pia unafanya kosa lile lile unalomshutumu Yeriko kulifanya? Mbowe hajatangaza kugombea lakini wafuasi wa Lissu wengi walianza kumshambulia badala ya kujenga hoja ya kwa nini mtu wao anafaa kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Aidha, kwa nini mipango aliyoainisha yataisogeza mbele Chadema. Hivyo ndivyo ilipaswa kuwa lakini watu wamehamia kwenye matope.

Naamini kuwa Lissu alipoamua kugombea cheo hicho alijua kuwa kuna watu watampiga madongo. Atakapogombea urais, haya ya Yeriko yataonekana cha mtoto. Inabidi avumilie na ajirekebishe pale ambapo kweli ana mapungufu. Akifanya hivyo kweli atastahili kuwa Mwenyekiti na Rais wa nchi yetu.

Amandla..
 
Hicho chama hakina Mwenyekiti kwa muda mrefu chagueni kiongozi wa kuwaongoza huyo mwingine akiitwa kula Pilau Ikulu anasahau malengo ya Chama chake na ndie aliekigawa Chama kwa muda mrefu sana..
 
Chawa wa Mbowe mnatia aibu sana bora mngekaa kimya tu mkaacha demokrasia ichukue mkondo wake kama wanachama wanamtaka Lissu basi atakuwa mwenyekiti siyo umekaa umeshiba bamia zako huko unasema sisi, wewe na nani mlikaaa mkaona Lissu hafai? Semea tumbo na fursa zako unazopata kwa conection za Mbowe basi siyo unabana pua eti mumeona, wewe na nani ?
 
Na ya kifaransa!

Amandla...
 
Chawa Promax, Huu muda mnautumia kuandika hizi takataka tungeungana twende mashambani huku tukalime tuongeze uzalishaji.
 
Ukiona kiongozi kakaa muda mrefu kwenye uongozi, anapopata mpinzani ili aachie hiko cheo. Na maneno yanakuwa mengi na kumpinga sana huyo ajaye.
Basi jua kuwa, hapo kuna ulaji na maslahi makubwa sana. Pia kuna madudu makubwa, hawataki wengine wayajue.

Sisi tusio na vyama, wenye kupenda haki kote. Mbowe ni muda wa kupumzika, ije fikra mpya na mawazo mapya. Chadema ya sasa haina jipya, ipo kama nusu kujifia na nusu haijulikani.

Labda mseme ni chama boya, kilianzishwa kuwahadaa wananchi, kuwa kuna upinzani Mkuu Tanzania. Zaidi ya hapo, anahitajika Mwenyekiti mpya. Kila mwenye akili timamu, hawezi pinga hili. Ila wenye maslahi yao watapinga.
 
Uongozi sio katiba bali ni dira ya kiongozi.

Dira ya kiongozi ni ilani ya chama chake kwenye uchaguzi.

Tunaposema asilimia kubwa ya wachangiaji wa jukwaa la siasa hata siasa zenyewe hawazijui we mean.

Katiba ndio dira ya nchi; hata unaweza sema ni vipi Magufuli alivunja katiba zaidi ya hadithi.

Embu sema lini Magufuli hakuheshimu katiba zaidi ya hadithu tu (huna huo uthibitisho).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…