Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Nimemuelewa sana mdau hapo juu ntatumia hii idea
ndugu tuwasiliane mimi nafanya iyo biashara kwa muda sasa.. nachanganya duka la dawa na vipodozi.. njoo tushauriane namna gani unaanza nitakupa list ya vipodozi k.koo maduka mazuri ya bidhaa OG nafahamu. na mengine tutaeleweshana mpka unasimama mwenyewee. nipo hapa 0713752709.. pia kuna makabati ma4 ya vipodozi au pharmacy ya aluminium nauza kama unahitaji uyaone. karibu
 
Naenda kafanye biashara utajifunzaga huko huko kuibiwa nako ni moja ya somo unalotakiwa kufaulu KILALAKHERI BINTI YANGU biashara ni kama ndoa Luna watu inawakubali na kuja watu wanasukumana ila wote wanandoa
 
Maswali mengi hapa ulitakiwa uwe na majibu kabla hujafanya maamuzi ya kodi na vingine

Btw wanakuja wajuzi
Acha roho ya wajumbe mkuu,
Jifunze kuwa positive kwa wengine,
Amethubutu let give her a support zaidi ya kubeza!!
 
Mkuu hayo ya wateja, na competition anayajua mwnyewe adi amefikia kuwa na wazo la kufanya iyo biashara na asifanye nyingine manake anajua fika namna ambayo atapata wateja, pongezi zake kwa kuwa na moyo wa uthubutu mana ata ukiwa na izo skills za entrepreneurship kibongo bongo bila mtaji utakufa ma materials yako kichwani...

Sis tumezoea ukipata mtaji kidgo ufanye ujasiriamali ili Ku manage na Ku maintain pesa yako ili badae ufanye kitu.. Mambo ya business plan sijui Ku calculate ma income ma nn sijui ni less applicable hapa. Otherwise umpe ushauri na sio kum criticize
 
we jamaa umeongea point kubwa sana, na zaid ya sana mtu akifikiria zaid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Eti wanaofundisha hawana hata genge la nyanya
 
Asante kwa maelezo yaliyoshiba vizuri mkuu
 
Naomba kushauriwa juu ya biashara ya vipodozi. Wazo langu ni kuuza mafuta ya kuondoa chunusi na makunyanzi usoni.

Naomba kufaamishwa ni mafuta gani mazuri yatayo pendwa na wateja. Nimewaza ili biashara yangu iwe ya tofauti nahitaji kupata mafuta ambayo ni mazuri na haya patikani Tanzania kwa wingi ili nisipate ushindani mkubwa kwenye soko.

Ninayo platform kubwa ya kutangaza biashara ,YouTube Facebook, Instagram nina watu walio ni follow na subscribers jumla 500k.

Naombeni ushauri na changamoto za biashara.
 
Vipodozi vipo vya aina nyingi tu, unachotakiwa kufanya ni kutafanya utafiti ili kugundua ni vipodozi vipi ambavyo vinaruhusiwa kuingia nchi na vinatoa matokeo chanya kwa mtumiaji(mteja)

Kuna vipodozi aina 933 ambavyo vimetambuliwa na kusajiliwa na mamlaka ya dawa vifaa tiba na vitendanishi (TMDA) zamani (TFDA) vya ndani na vya nje ya nchi, ambavyo havina viambato sumu aina ya hydroquinone na nyinginezo.

Vipodozi zimegawanyika katika makundi mbalimbali kama ifuatavyo;-
Krimu,losheni,nywele,jeli,pafyumu,dawa za meno,roll on, sabuni,shampoo, poda,vipodozi vya kunyolea (after shave),cleansers, na mafuta ya maji(oil).

Kila kundi katika vipondizi hapo juu lina majina yake, nitakupa mfano mdogo hapa chini;
Krimu; 4u cream, Almondo kesar, heel cream na clear tone
Losheni;Avon herbal care,elegance lotion na miss lotion.
Vipodozi vya nywele;coco vanila soft na L' oreal dark
Jeli; afro jelly,bossy jelly na far shower gels

Kifupi tu nimesemi vipo vipodozi vya aina nyingine tofauti tofauti kutoka kwa makampuni mbalimbali.

Lakini pia vipo vipodozi kutoka nje ambayo ni pendwa ila haviruhisiwi kuingia nchi kutokana na kuwa na viambato sumu, ambavyo watumuaji wengi hasa wanawake wanavipenda, vipodozi hivi vinatoka sana Congo, hivi ukijihusisha navyo vitakupa ugumu kuvipigia promo katika ukrasa wako.
 
Ahsante sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…