Kwa kusema kweli biashara ya vipodozi inalipa vizuri tu ukiielewa vizuri na kucheza vizuri na soko lako na biashara yenyewe kwa ujumla.
1. Nikiasi gani cha mtaji kinahitajika(minimum amount of capital) =
Inategemea na msuli wako. Ila minimum uwe na kama Tsh Millioni Saba Hivi (7,000,000/=) Hivi kwa maeneo ya mjini; i.e.
- Kukodi fremu = Tsh 100,000/= kwa mwezi, miezi 6 >> 600,000/=; dalali utajuana naye mwenyewe
- Kusajili TFDA = 150,000/=
- Leseni halmashauri = 80,000/=
- Kodi TRA kama Tsh 150,000/= hivi kwa mwaka, quarter 1 utalipia Tsh 37,500/=
- Kuweka mashelfu ya aluminium na vioo = 1,000,000/=
- Kabati la chini la aluminium na vioo = 400,000/=
- Vipodozi angalau vya kuanzia = 4,000,000/=
- Pesa ya kukaa standby kwa ajili ya kuongezea vipodozi watakavyokosa wateja = 1,000,000/=
- Pia uwe na akiba ya kuendelea kuishi na kuhudumia familia yako bila kudokoa pesa kutoka kwenye duka lako kwa angalau miezi 3 hivi
2.Ni vipodozi vya aina gani vyenye uhitaji mkubwa sana sokoni(consumer needs) =
Soko la vipodozi mara zote ni dynamic; leo wateja wako wanatumia Rinju, baada ya miezi 6 watakuwa wanatumia kitu kingine. Pia inategemea sana na eneo utakaloweka duka lako, kuna maeneo wananunua bei na kuna maeneo wananunua brand. Ukitaka kufanikiwa hapa ngoja wakati ukiwa tayari kufungua duka basi fanya survey maduka ya wenzako wamestock nini kisha nenda kwa duka la jumla la eneo lako mwambie unataka ufungue duka la rejareja na ununue vipodozi kwake, muombe akuambie vipodozi vinavyotembea kwa wakati huo na vipodozi gani vya kuwa navyo anyway. Kwa hiyo ukiwa tayari kuingia sokoni ndo utafiti hili
3.Ni vipodozi gani vina faida kubwa sana =
Vipodozi vyote vina faida kubwa sana. Faida inatokana na kasi ya kutoka kwa kipodozi husika na tofauti kati ya bei ya kununulia na kuuzia (profit margin). Kwa ushauri wangu ni bora uangalie mahitaji ya wateja wako kuliko faida. Unaweza kuweka vipodozi vyenye faida kubwa halafu vikawa havina movement kwenye location yako - utaangukia pua. Au unaweza kuweka vipodozi vya bei ya chini ambavyo wateja wako hawaviamini na wala hawavitumii.
4.Hasara ambazo unaweza pata = Hili nimekuwa nikiwafundisha sana watu wanaokuja kujifunza kwetu biashara ya vipodozi A-Z.
Zipo nyingi, ila karibia zote zinaepukika. Muuzaji kukuibia, adhabu za TFDA, adhabu za TRA, adhabu za halmashauri, vipodozi kuharibika, gharama za uendeshaji kuwa kubwa kuliko faida ghafi (gross profit) na kadhalika.
List ya vipodozi vilivyoruhusiwa kuuzwa na vilivyokatazwa kuuzwa zote zinapatikana kwenye tovuti ya TFDA:
www. tfda. go. tz (Toa hizo space)
5.Sehemu ya kuweka duka(Matter of location) = Location kama kawaida, wewe tu na ubavu wako; ila ukipata
mtaa wenye wakazi wengi au sehemu yenye movement nzuri ya watu - hususan akina dada basi umewin. Iwe ni njia ya kwenda university, mtaa wenye biashara ambazo wateja wake wengi ni wanawake, mtaani wanakokaa hao akina mama, mjini, sokoni nk. Zingatia sheria za TFDA, kuna baadhi ya maeneo hutakiwi kuweka duka la vipodozi (mfano karibu na kituo cha mafuta) hata kama kibiashara ni strategic location
(Please kabla ya kulipia fremu kaonane na TFDA, eneo lako lisije kukataliwa wakati umeshalipia)!
6.Sehemu nzuri ambayo naweza fungasha mzigo kwa bei rahisi sana( iwe nje au hata ndani ya nchi hapa mkoa wowote ule) =
Kariakoo is the best (ila usipokuwa makini inawezakuwa the worst)! Siku za kwanza nenda na mwenyeji tu hadi utakapomaster, vinginevyo utanunua kwa walionunua na hivyo kupata vipodozi kwa bei mbaya na kuuza kwa bei mbaya - kumbuka akina mama ni very sensitive kwenye suala la bei kwa hiyo ukiuza bei juu hata kwa tofauti ya Tsh 500/= tu basi watapita duka lako na kwenda kununua kwa jirani yako au hata mbali sana; unaweza kuhisi umerogwa, ila 500/= mwenzako anapata vocha!
Ila kitu kimoja - changieni maduka ya jumla ya mikoani kwenu. Kwa hiyo kama haupo Dar es salaam basi usinunue kutoka Kariakoo, tafuta maduka ya jumla hukohuko mkoani kwenu.
I am done & Out!
Ukihitaji kujua zaidi ya hayo basi karibu nitakupa darasa zaidi maana kuna mambo kama 21 hivi ambayo nitakufundisha kwa wiki 1 (Kila siku nitakufundisha mambo matatu makubwa) kuhusu kuanzisha, kusimamia na kuendeleza duka lako la vipodozi (Ila utanipodha soda mbili [emoji23][emoji23][emoji23] maana ni consultancy eti
🙂🙂🙂)
Viva JF!
AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS
0719326693 | 0743422883 | afyazaidi@gmail.com