Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Biashara ya vipodozi minimum uwe na hata 1.5 ili uwe na sort angalau mbalimbali za vipodozi.
Kutaka angalau kujaza jaza duka. Atleast uwe na 3milion.
Chimbo hilo jamaa kalitoa zuri sana.
Kwa vipodozi vinavyotrend
1. Wix za director joan.( yupo kinondoni, na tandale)
2. Esta dalali (sinza madukani)
3. Sacques “sachko” ( sinza mabatini/kijitonyama)
Ukiweka hizi utapata sana, changanya. Kwa mtaji wowote. Hawa wana vitu. Na arrangement zao zitakufanya ujue biashara ya vipodozi inataka nini zaidi na wanatoa ushauri. Maana wao ni wauzaji wa jumla na rejareja.

Sasa wale watu wa mambo mengi. Wa kuanzia 4-10m akili mtu wangu. Tafuta mzigo kwa ushauri ili upate kitu kizuri na chenye faida ila bila hivo. Utabaki unauza kila siku, ila upo pale pale. Alafu wenye walianza na mitaji midogo wanakufikia chap.(akili mtu wangu)

Wix haina soko kwa sasa rafiki

Kuna Viera na La vista

Sachque anauza vitu bei ghali wateja watakukimbia hivyo vitu vya Sachq unavipata Sinza kwa Panda Sourcing au Berogenge[emoji28][emoji28]

Kkoo kuna mtu anaitwa Faiz anavile vya High quality vya kubutulia bei.
 
Wix haina soko kwa sasa rafiki

Kuna Viera na La vista

Sachque anauza vitu bei ghali wateja watakukimbia hivyo vitu vya Sachq unavipata Sinza kwa Panda Sourcing au Berogenge[emoji28][emoji28]

Kkoo kuna mtu anaitwa Faiz anavile vya High quality vya kubutulia bei.
Hivi kwa nini lakini unaiponda wix?Yaani jamani
 
Wix haina soko kwa sasa rafiki

Kuna Viera na La vista

Sachque anauza vitu bei ghali wateja watakukimbia hivyo vitu vya Sachq unavipata Sinza kwa Panda Sourcing au Berogenge[emoji28][emoji28]

Kkoo kuna mtu anaitwa Faiz anavile vya High quality vya kubutulia bei.
Panda ni mtu na nusu nakumbuka sakata lake na sanchq la snail
 
Me huwa napenda sana kufanya hii biashara asante kwa madini ila tatizo mtaji wangu ni laki 6 nitaweza kweli kutoboa? Coz naona wengi wanaeleza mtaji uanzie angalau M1 na point.
 
VIPODOZI [emoji116][emoji116][emoji116]

Anzisha Biashara ya Vipodozi Kiulaini Kabisa:- Mwanzo huu hapo. Unapotaja biashara ambazo watu huendelea kupiga pesa hata kama uchumi umedorora basi lazima utataja vyakula,Nk kwanza lakini kama ukiambiwa uongeze bidhaa nyingine hapo basi ongezea na vipodozi, hasa vya wakina mama.

Mwanamke lazima asuke, apake mafuta na ajipulizie perfyumu ndio atajiona yupo tayali kutoka kwenda ibadani, kazini, kutembea au hata kujibrand tu. Hivyo basi mahitaji ya vipodozi siku zote yapo juu na ukianzisha biashara hii ukiwa na malengo, uvumilivu na displini basi itakutoa na mchakato wake ni mwepesi kabisa. Endelea kusoma.

Ukifika Bigbon ya Kariakoo kama unatokea fire, vuka barabara, hayo majengo ya mbele yako ukiyazunguka au ukiingia ndani kupitia uchochoro wowote unatokea kwenye himaya ya vipodozi. Ingia kwenye hilohilo jengo la mbele yako. Eneo hilo zamani yalikuwa yanapaki madaladala ya kwenda Sinza na Ubungo na sasa hivi kuna kituo cha mwendo kasi pia.

Kwa kulia kuna mtaa wa Mafia ukishuka nao pia utaanza kukutana na maduka ya vipodozi. Kwa kushoto kuna barabara ya (Pemba) na Jangwani pia hayo ni maeneo ya vipodozi na nywele

Lakini sio tu nywele dizaini zote na vipodozi utavikuta hapa kwa bei ya jumla na rejareja lakini mazagazaga yote ya urembo utayakuta hapa, lipstick, rangi za kucha, perfyume, body freshener, mafuta ya lotion, ya mgando, ya nywele, scrub na kila kitu kinachohusiana na urembo na mambo ya saluni za wanawake.

Kama unamtaji wako na unandoto ya kuanzisha biashara ya vipodozi basi kabla hujafikiria kwenda china au dubai au Zambia anzia hapa. Kupata nywele za Brazilian sio lazima uende Brazil, utazitkuta hapa pia.

Ukiwa na pesa ya mtaji mdogo tu wa kawaida unaweza kufunga mzigo wa maana tu na kurudi nao kwenu kufungua biashara ya ndoto zako sababu hapa yamejaa maduka yanayouza jumla na rejareja. Kama umenunua nywele au mafuta mtaani kwako kuna uwezekanao mkubwa nywele au mafuta hayo yamenunuliwa hapa na muuzaji mwingine wa duka la jumla ambae kamuuzia aliyekuuzia wewe.

Kuuliza bei na ku bargain ni kitu muhimu sana hapa, usinunue vitu kwenye duka la kwanza utakalokutana nalo, utatakiwa uwe mjasiri wa kuuliza bei na kuondoka bila aibu ukiwa mkavu kabisa na kuuliza duka linalofuatia na linalofuatia. Usiishie kwenye maduka ya nje ingia na frame za ndani uone na kuuliza. Mfano, Mafuta ya American dream ambayo mitaani yanauzwa elfu 40 na zaidi kwenye hili soko la vipodozi yanaazia elfu 25, ingawa maduka mengi watakuambia elfu 30.

Hii inamaanisha kuwa kuna wenye maduka hapo wanauza jumla nao wananunua kwa wenzao hapohapo wanaongeza cha juu kidogo na wao pia wanauza kwa bei ya jumla. Mfano nywele zinaitwa coco ambazo mtaani huuzwa 1,500 humo utazikuta kwa 800 mpaka 1,350, na cha kufurahisha zaidi wadada wanaokimbia gharama za kusuka saluni za mitaani huenda kusukia hapo hapo. Ndio, wasusi ni wengi sana pia mitaa hiyo, unanunua nywele kwa bei ya jumla na kusukwa hapo hapo.

Kukupa uhakika kuwa hauingii chaka utaona kwenye maduka makubwa kuna mafurushi mengi na makubwa ya mizigo ya vipodozi inayonunuliwa na kufungwa kwenye mabox na viroba kwa ajili ya kutuma mikoani na maeneo mengine ya mji wa Dar. Kwahiyo wakati wewe utabaki unajiuliza maswali ninunue au nisinunue utaona wenzio wanafungasha na kupeleka kwenye malori.

Wauzaji wa hapa wanapataje hivyo vipodozi na nywele? Kwa mfanya biashara mdogo usijipe hii presha subiri mpaka ukue kwanza lakini kwa mfanyabiashara mkubwa ni kua kuna wachina wana magodown ambapo unatakiwa uweze kuchukua kiwango kikubwa sana kwa wakati mmoja.. [emoji1666]
Hao wachina nawapatajenisaidie kupata connection nahao wachina
 
Naskia ishu ni mtaji maana vimafuta vya wadada bwana. Niliombwa na mpenzi wangu nipitie duka la vipodozi nimchukulie mafuta. BEI nlokuta mi niliacha maana niliona huu ni ufujaji hela huwezi ninunulisha kikopo kdg kama cha mafuta ya Baby Care eti 20,000 sikumchukulia kwakweli nilienda mwambia nimekosa.

so Tukirudi kwenye mada Mtaji ndo tatzo maana mafuta kama hayo ya 20k bei ya jumla sidhani kama ni chini ya 10k sasa kimafuta kinauzwa 10k utanunua vingap uviweke dukani?

Na hawa wadada akija trip ya kwanza kakuulizia Ukamwambia HUNA ya pili HUNA ya tatu HUNA basi huyo mteja anakuhama...Kuna mtu alinambia Kwa haraka haraka ki duka cha kawaida kabisaaaaaaa cha urembo Hapo ushalipa Kodi kila kitu ni Mtaji tu BASI isiwe chini ya 5M kama upo serious kweli na hii biashara.

Ila kama unataka kutest hujiamini hata 1M unaanza.
No, kwa mtaji wa 1M huwezi fanya biashara hii ya cosmetics!
Mzigo wa 1M ukifungashiwa, unaishia kwenye maboksi matatu tu ya size ya kati, na unaweza kuishia kwenye vishelfu tisa tu vya duka lako. Chukua mfano duka lako dogo lina jumla ya shelfu 30 tu, je utatumia mtaji wa kiasi gani kujaza hilo duka? Hapo bado hujajaza mzigo kwenye makabati.
 
Habarini wadau na m2 hapa out of rent nawaza kufungua duka la vipodozi ambalo litajaza lenyewe iwapo litakuwa linaweka faida.
  • Je, m2 kwa kuanzia inatosha?
  • Je, vipodozi gani vinatoka kwa wingi?
  • Je, faida zake na hasara ni zipi?
Msadaa tafadhali.

Au kama mtu ana idea nzuri ya biashara ya ufugaji anipe.

========
Kwa maoni zaidi soma uzi huu:Duka la Vipodozi-Ushauri na Muongozo wa kuanzisha
 
Ingia tu mzee utajua ukouko M2 hela ndogo usiogope kuipoteza ingia ujione watu watakudanganya maana kwa M2 ni mtaji wale machinga wanatembeza na toroli
 
ingia tu mzee utajua ukouko M2 hela ndogo usiogope kuipoteza ingia ujione watu watakudanganya maana kwa M2 ni mtaji wale machinga wanatembeza na toroli
We unaona m2 ndogo sio bhasi sawa acha niongeze ifike 5 ninunue mkoko wakulia totozi
 
Hapo kikubwa ujue aina za ngozi na matunzo yake. Hapo utapata wateja wengi.Lakini ukilenga tu kununua na kuuza ,hapo uwe na mtaji mkubwa zaidi ya hapo
 
M2 inatosha kabisa nenda duka la jumla kila bidhaa unachukua Pc mbili mbili.
 
Mnaboa sana.
Mkipewa fedha ya kutoa ushauri, fedha mnakula then hamfanyi chochote!
Unatazamia kupata mtaji na kufikiria biashara ya kufanya au tayari umepata mtaji ila bado unaifikiria biashara ya vipodozi?
Leo nakuandikia wewe kwa ajili ya kukupa mwangaza kidogo wa namna ya kuanza na gharama zake.

FAIDA YAKE IKOJE?
Biashara ya vipodozi (duka la reja reja) iko wazi moja kwa moja haina mambo ya siri wala mambo ya nyuma ya pazia. Unaandaa chumba na kuweka makabati pamoja na shelves, kisha unapanga vipodozi vyako aina mbalimbali (Losheni, body spray, mafuta, sabuni, shampoo na kadhalika) na kuuzia wateja wako watakaokuja kununua.

Wewe unanunua kutoka maduka ya jumla kwa bei ya jumla, kisha unauza kwa wateja wako kwa bei ya reja reja. Bei ya reja reja = bei ya jumla + faida. Mara nyingi faida = 10% hadi 50% ya bei ya jumla.

Kwa hiyo kwa mfano ukinunua losheni kubwa ya NIVEA kwa Tsh 10,000 wewe unatia faida ya 20% ambayo ni sawa na Tsh 2,000 kisha kuuza losheni hiyo kwa bei ya reja reja = bei ya jumla + faida = Tsh 10,000 + Tsh 2,000 = Tsh 12,000.

Kwa hiyo unakua umenunua kwa Tsh 10,000 na kuuza kwa Tsh 12,000 hivyo kupata faida ya Tsh 2,000; ukiuza makopo 50 kwa mwezi unapata faida ya Tsh 100,000.

Kwa hiyo kwa kifupi ni kwamba faida huwa kati ya 10% hadi 50% ya bei ya kununulia mzigo wako, kutegemea na bidhaa husika. Kuna mwezi unaweza kununua mzigo wa Tsh 3,000,000 na kupata faida ya Tsh 400,000; na kuna mwezi unaweza kununua mzigo wa Tsh 3,000,000 na kupata faida ya Tsh 600,000.

Ila kwa ujumla biashara ipo na faida yake ni nzuri. Cha msingi uwe na wateja wa kutosha na uwauzie bidhaa nyingi au za thamani kubwa. Chagua eneo zuri la kuweka duka lako, ukifeli location utapata tabu sana.

Location ndo kila kitu. Usijiweke kwenye ushindani usiouweza, usijiweke pasipo na wateja wanaoziweza na kupenda bidhaa zako, usijiweke eneo lisiloruhusiwa, usijiweke mbali kiasi cha wateja wako kufikiria mara mbili mbili kama waje kwako au waangalie sehemu nyingine tu.


MTAJI KIASI GANI UNATAKIWA?
Mtaji unategemea na gharama za eneo lako, ukubwa wa duka na vipodozi utakavyoanza navyo. Tsh 4,000,000 hadi Tsh 8,000,000 inatosha kuanzia.
MTAJI = Gharama za kukodi na kuandaa duka + gharama za vibali, vyeti na leseni (halmashauri + TBS + TRA + Brela) + gharama za kununua vipodozi + mawasiliano na usafiri + gharama za kujitangaza + Bili za maji na umeme + michango ya serikali za mitaa/kijiji+ Akiba + Mengineyo.

Kwa mahesabu ya chini (Eneo la mjini) Inabidi uwe na angalau Tsh Millioni Nne (Tsh 4,000,000). Ikiwa chini ya hapo itabidi utumie akili nyingi sana na mbinu mbadala nyingi nyingi, ila ikiwa zaidi ya hapo maisha yako yatakuwa rahisi zaidi na duka lako litakuwa zuri sana.

So cha muhimu ukiwa na mtaji anza kuupangilia vizuri kabisa utautumiaje kuanza biashara yako. Panga mapema kabla hujanunua kitu chochote wala kulipia chochote. Ukihitaji ushauri na kupanga pamoja unaweza kucheki na mimi nitakusaidia: 0788179686 | afyazaidi@gmail.com

JINSI YA KUANZA BIASHARA
Kusanya taarifa za kutosha na ujiridhishe vya kutosha kabla ya kuanza biashara hii maana kuna baadhi ya mambo ambayo umewahi kuyasikia yanaweza yasiwe kweli au yasiendane na mazingira yako wewe. Ukishakuwa na taarifa za kutosha na kujiridhisha kwamba upo fit basi sasa unaweza kumalizia kujipanga, kujiandaa na kuanza.
  • Weka mtaji wako tayari
  • Tafuta sehemu ya kuweka duka lako
  • Wasiliana na TBS upate uhakika kwamba hapo duka lako litakubaliwa
  • Lipia kwa mwenye jengo na pata mkataba
  • Kama hauna TIN nenda ofisi za TRA ukiwa na mkataba, kitambulisho cha Taifa na barua kutoka serikali za mitaa kwa ajili ya kupatiwa TIN (TIN ni bure, ila unaweza kushauriwa kulipia kabisa makadirio ya kodi yako ya robo mwaka)
  • Nenda ofisi za TBS kwa ajili ya kupata kibali cha duka la vipodozi (Utalipia ada ya kibali)
  • Nenda ofisi za halmashauri ukiwa na Copy ya kataba, kitambulisho chako, TIN na kibali kutoka TBS kwa ajili ya kupatiwa leseni ya biashara (Utalipia ada ya leseni)
Ukiwa na TIN ya TRA, Kibali cha duka la vipodozi kutoka TRA na leseni ya biashara kutoka Halmashauri hapo sasa utakuwa tayari kufungua duka lako na kuanza biashara.

UMEIPENDA KWELI?
Kama umeipenda kweli biashara hii basi kila la kheri. Ni nzuri na ukiifanya kwa moyo na akili utafanikiwa.
Ukihitaji maarifa zaidi, business plan, list ya bidhaa, kupangilia matumizi ya mtaji, kuelewa changamoto, support na mambo mengine mengi nipigie au nitumie meseji/email nitakupa maujanja.

UKIHITAJI USHAURI NA MUONGOZO MZURI
Anza kutuma meseji yenye neno BIASHARA YA VIPODOZI kwenda namba 0788179686 kisha utapokea dondoo na mambo mengine mengi ya muhimu kuyafahamu.
Karibu sana AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS!
0788179686 | afyazaidi@gmail.com | Afyazaidi | Nyumbani



View attachment 1832871
 
Back
Top Bottom