Nakushauri:Habari za jioni wakuu,
Nina imani humu wote ni great thinkers.
Ninaomba mnisaidie mawazo wakuu mimi ni binti mdogo tu 24 lakini nimechoka na Kazi za kuajiriwa na ukizingatia kipindi hiki kigumu ajira hakuna nimekuwa na mawazo ya kujiajiri hasa biashara ya urembo wa wanawake niwe napitisha maofisini lakini the thing is sina uzoefu na that kind of business na pia sijui pa kuanzia.
Capital sio tatizo ila tatizo naomba mawazo yenu wakuu pa kuanzia au ambapo naweza pata huo mzigo ili nianze kusambaza.
Asanteni
Nashukuru sana mkuu kwa mawazo yako yaani umeongea kama ulikuwa kwenye mind yangu juu ya bidhaa nayotaka kuanza nayo.Kwa haya maelezo yako hapa dada wewe tayari umeshapiga nusu hatua, cha msingi ni kumalizia tu hiyo hatua iliyobaki. Nakushauri
1. Vipodozi utavipata kutoka kwenye maduka ya jumla ya vipodozi ambayo yamejaa pale Kariakoo mtaa wa Msimbazi. Kuwa makini sana na vipodozi feki, vilivyopigwa marufuku na visivyosajiliwa
2. Andaa business card, begi la kubebea vipodozi vyako na mifuko ya kuwawekea wateja wako bidhaa utakazowauzia
3. Sana sana lenga kuuza. Utaanza kukopesha mtu akishakuwa mteja wako tayari na ashaanza kukuingizia faida kiasi. Pia utakopesha watu ambao una uhakika nao sio wasumbufu na wale ambao watakuwa referred na wateja wako wengine
4. Vipodozi vipo vya aina nyingi sana. Lakini ambavyo vitaweza kukutoa haraka kwa hapa Dar ni Perfume, Deodorants na Lotion. Changamoto ni kila mteja kutaka perfume au deodorant au lotion ya aina yake, na tofauti na zile ambazo wewe unazo. Hapa utakuwa unachukua order na kumuahidi kumletea huyo mtu siku inayofuata, na usikose kumpelekea.
5. Jenga network nzuri kwa ajili ya biashara yako. Jichanganye sana na watu na omba watu hao wawajuze watu wengine kuhusu wewe na wakusaidie wewe kuwafikia watu wengine. Chukua namba za wateja wako na wafahamishe ukiwa na mzigo mpya, bidhaa zingine na hata ukiona muda mrefu umepita hawajanunua chochote.
6. Anza na vipodozi vya bei ya wastani (Sh 5,000/= - 20,000/=). Hivyo wateja wake ni wengi zaidi na mzunguko wake ni mkubwa zaidi
7. Wasome vizuri na kuwa makini na wateja wako. UKICHEKA NA NYANI UTAVUNA MABUA
Mimi nafanya biashara ya uzuri, urembo na vipodozi. Ingawa kwa mtindo mwingine.
Nakutakia kila la kheri!
Biashara ya urembo ni pana kidogo cjui unataka kudeal na vitu gani Zaidi? AnywayWanaJF ninawasalimu.
Naomba msaada kwa wale wanaoijua vema biashara ya urembo na vipodozi, ni wapi naweza kupata mzigo wa jumla kwa bei rahisi, je naweza nikaanza kwa mtaji kiasi gani ukiondoa gharama za fremu, kwa mnaojua naomba mnisaidie.
Ahsante ndugu umenipa mwanga to the maximum lengo langu ni kudeal na vipodozi na hizo chain, bangili, hereni na sio nywele!Biashara ya urembo ni pana kidogo cjui unataka kudeal na vitu gani Zaidi? Anyway
Kama upo dar ukienda Kariakoo pale ule mbezi/Kimara uraona maduka mengi ya nywele (rasta na weavings) pamoja na vipodozi vya aina zote. Pale utapata vitu hivyo kwa bei ya jumla. Kisha ukifika jengo la Simba, vuka upande wa pili wa barabara utaona mtaa Fulani unaingia pale opp na hilo jengo (Sifahamu jina la mtaa). Huo mtaa utaona maduka mengi ya urembo (cheni, hereni, bangili, s/tight, lipstics na mazaga zaga karibia yote ya urembo wa kina dada kwa bei za jumla.
Nadhani nimekupa mwanga kidogo.
Vyote unavyotaka vinapatikana maeneo hayo kaka. Hata leo nimeenda kuchukua mzigo. Ukiwa tayari unaweza kunicheki inbox naweza kukuelekeza vizuri hata kukupeleka kama nitakuwa na muda.Ahsante ndugu umenipa mwanga to the maximum lengo langu ni kudeal na vipodozi na hizo chain, bangili, hereni na sio nywele!!!
Ahsante sana!
Nitajitahidi jamaa angu saivi niko mbeya nikija Dar ntakushtua.Vyote unavyotaka vinapatikana maeneo hayo kaka. Hata leo nimeenda kuchukua mzigo. Ukiwa tayari unaweza kunicheki inbox naweza kukuelekeza vizuri hata kukupeleka kama nitakuwa na muda
Nitajitahidi jamaa angu saivi niko mbeya nikija dar ntakushtua....!!
Mkuu vinauzwaje hivyo vipodozi mkuu.Mkuu nicheki nina baadhi ya bidhaa za duka la vipodozi naziuza. duka la wife analifunga na kufanya biashara ya ufugaji..so tunauza bidhaa za hilo duka kwa bei ya chini pungufu hata bei za jumla kariakoo.
Mkuu vinauzwaje hivyo vipodozi mkuu
Ajabu Wanawake Wengi Wanazipenda!Halafu jiandae kisaikolojia kwa upande wa vipodozi kuhusu kuexpire na mikikimikiki ya TFDA, hawa wako sensitive sana katika biashara hizo, wanaingia hadi dukani kutafuta vipodozi haramu mfano karolait,na hizo haramu ndio zinauzika kinoma, inabidi ukiweka uuze kama.bange