Baada ya kutafakari nichangie nini naona nije hivi! Kinachoshangaza wanachadema wanashangilia Ccm wanalia!!! Hii inaonyesha jinsi gani chama hiki kimekosa watu wenye uwezo wa kufikiri.
Hata kama mkakati umetengezwa na ninyi ni uendawazimu kuonyesha hadharani kwamba ni wewe mchawi unayesikitikia matendo yako. Inawezekana kuna wanachadema wangemuunga mkono ZZK lakini kwa kuliliwa na adui zetu ni wazi manamuunguza mwenzenu.
Chama chetu ni imara sana, ninawahakikishia kitatoka ktk issue tukiwa washindi. Katika siasa upepo kuvuma vibaya au vizuri ni turufu! Tulilifuatilia kwa makini na tukajua ni wakati wa kufanya maamuzi.
Msilolijua ni kuwa tunazidi kuwa maarufu kwa kuendelea kutupa headlines, hasa katika maamzi magumu na ya msingi kama haya. Ni chama gani chenye uwezo wa kufanya maamuzi kama haya?