Ufafanuzi wa CHADEMA Kuhusu Maazimio ya Kamati Kuu - Novemba 2013

Ufafanuzi wa CHADEMA Kuhusu Maazimio ya Kamati Kuu - Novemba 2013

Status
Not open for further replies.
Hivi huyo Zitto akihamia CCM atapewa huo uenyekiti wa CCM taifa? Au ametumika tu kama kondomu ambayo sasa imekwisha muda wake? Hayo mapenzi ya CCM atayaonja tena kweli?
 
Prof. Baregu hakufukuzwa ali alikuwa amestaff anafanya kazi kwa mkataba. Mkataba ulivyoisha hakuongezewa. Ni jambo la kawaida katika utumishi wa umma. Sikubaliani na matendo ya kitila lakini ni muhimu kutofautisha hizi scenario mbili.

point taken!
 
Wadau kwa mwenendo wa kinafiki wa dr kitila ni wazi kua amei aibisha jumuia nzima ya udsm,kama msomi mzima anakosa misimamo,anakua na ndimi mbili vipi kwa malayman? inatia hasira kuona mtu anaeitwa msomi anakua kinara wa kurudisha nyuma harakati za kuikomboa nchi yetu,tabia ya kinafiki ya watu dizaini ya kitila si ya kuichekea popote pale iwe cdm,ccm,cuf,nccr whatever.

UDASA imekua ikipwaya shauri ya mwenendo wa watu kama mkumbo,swali la kujiuliza ni hili kwa vipi prof baregu alitimuliwa udsm kwa sababu tu alikua cdm na kitila mpaka leo bado yupo ilihali ana faamika kua ni cdm? jibu nadhani umeshalipata.....mkumbo ameitia aibu jumuiya ya wasomi wa UDSM.
hivi balegu ameanza lini kuwa CDM,hakuanzia NCCR ya LYATONGA mbona hakufukuzwa kipindihicho ,tuache ukweli usimame,binafsi mpaka sasa sina la kusema manake sijasikia watuhumiwa wanasemaje
 
Ni ktk kutekeleza mpango wa wasira wa kuiua cdm ambopo wasaliti wangejiongezea kipato binafsi.
 
Magamba ya Sisiem yameungana na ngozi. Ukilivua tu umeua.
 
Kitila Mkumbo
Hata wewe Mheshimiwa?kweli kikulacho kiko nguoni mwako.



Mkuu Cheche, hata mi sikuamini macho yangu kwamba Daktari mzima, tena mwenye kipaji cha uongozi wa kariba ya Mkumbo afanye mafyongo haya! Kweli Kitila unaweza shiriki njama za kuzamisha matumaini ya watanzania?
Dhamira yako na ikusute milele kwa dhambi yako hii!


BRAVO CHADEMA kwa antivirus mliyo instal leo
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Huyu kitila zamani akijiita mwanasiasa, ni mganga njaa tu. No wonder, the majority of UDSM dons are quite defensive.
 

For all practical purposes, Zitto is finished! Kwishnei kabisa! So sad! Siamini iwapo ana options zozote za kufanya kujiokoa au hata kuipa tabu CDM. Na akivuliwa Ubunge basi itakuwa ni ‘coup de grace,' yaani pigo takatifu lakini bila shaka anaweza kuamua kuwa ‘Mbunge wa Mahakama,' kama vile walivyo wengine. Lakini pia anaweza kushinda tena kiti chake kwa kupitia chama chochote kile kingine.

Lakini tujadili kitu kimoja kwamba kuna pande fulani au watu fulani watakuwa wamepata pigo kwa kung'olewa Zitto kutoka vikao vya kamati kuu ya chama.

Natamka hivi kutokana na yalivyosikika na kuandikwa huko nyuma katika vyombo vya habari. Kwanza kabisa Usalama wa taifa (TISS) utakuwa umepata pigo kubwa kwani Zitto na Zoka walikuwa maswahiba. Tukumbuke kwamba wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010 gazeti la Mwanahalisi liliwahi kunasa mawasiliano kati ya wawili hawa, kwa kutaja namba za simu zilizotumika, muda nk.

Uswahiba wake na TISS ulikuwa kwa manufaa ya nani? Inafahamika kuwa TISS wamekuwa wakidaiwa kuhusika na mwenendo wa chaguzi kwa namna ya kuvihujumu vyama vya upinzani. Gazeti hilo baadaye lilifungiwa miezi mitatu kwa kuripoti habari za mawasiliano hayo.

Aidha mtu mwingine atakayekuwa kapata pigo kutokana na kuvuliwa nyadhifa Zitto ni JK. Alikuwa swahiba wake mkubwa sana. Tusisahau kwamba baada tu ya uchaguzi wa 2010 wakati Bunge lilikuwa katika mchakato wa kuchagua kamati za Bunge, hasa zile oversight committees kulitokea mzozo mkubwa Bungeni wakati Spika anna Makinda alipobadilisha tafsiri ya Kambi rasmi ya upinzani Bungeni kwa lengo kuinyima CDM uewenyekiti wa kamati hizo.

Baada ya kuona uwezekano wa CDM kukosa kabisa nafasi hizo gazeti moja (The Citizen, nadhani) liliripoti kwamba JK aliwasiliana na Anne Makinda na kumuomba ahakikishe Zitto anapata ile ile nafasi yake ya uwenyekiti wa POAC. JK alikuwa analipa fadhila kwa kazi nzuri ya Zitto? Hii ni kweli? Uswahiba wao ulikuwa kwa manufaa kwa CDM? Maswali magumu!




Mahusano yao yalikuwa siyo matakatifu -- yaani yalikuwa unholly alliance. Hawa watu wa TISS daima wamekuwa wakihujumu CDM kwa kuratibu mambo kadha ambayo hadi leo hii hayajapatiwa maelezo. Kikubwa ni bomu la Soweto. Ngoja tutege masikio tujue yatakayofumuka.
 
Naanza kukosa imani na CDM kwa hili tu they have made bad decisio kwa sababu ambazo zimeorodheshwa kama una akili zisizofuata mkumbo lazima ustuke!!
Samahani lakini huo ni mtizamo wangu tu!!
 
Kitila ni rafiki yangu kama Zitto .Wote ni wadogo zangu kwa umri .Ya Zitto nilisha zoea maana kila siku ilikuwa Zitto hadi unashindwa kujua lipi kweli na lipi siyo.Sasa la Comrade Kitila kwa kweli nimechoka mno .Hata la kusema sina .Kama alikiri kwenye barua yake hiyo it is also extreme .
 
CDM ni mfano wa kuigwa na hata wakishika dola watafanya maamuz magumu.

CCM ni mbumbumbu kwa sababu wanatoa siku 90 kwa waharifu mafisadi ndan ya chama zikifika, zikifika wanahamisha mada na kuleta polojo tu. ACHA TUAMUE tukiwa 10 strong its better 100 legelege
 
Thread kama hizi zinazidi kunikumbusha kuwa MAISHA NI SAFARI YA MUZIKI..... LET US SING TOGETHER.... GO GO. GO DHORTIE.... WE GONNA SIP BARCADI TONIGHT....
 
Chadema kipo kwenye Junction kuvuka au kutovuka Salama kunategemea Reaction ya Kina Zitto Kabwe!
 
Siasa njaaa msomi mzima unaendekeza njaa...! Ndo nyie ma dk na prof wa kibongo mna miradi ya kufuga kuku wa mayai
 
Kuondolewa kwa Zitto Chadema ni hasara kwa CCM maana waliwekeza sana kwake !
Lakini pia ni hasara kwake maana hatoendelea kutumika.
Na pia ni faida kwa yale mashirika ya umma aliyokuwa akiyakamua

Safi Sana mdogoanagu Richard! Short, concise, and to the point!
 
Kwa wingi wetu sisi wanachadema pamoja na mashabiki wa chadema. Kwa kuonyesha ya kwamba tumeibariki na kuyaeshimu maamuzi ya cc ya cdm iliyokaa kwa siku mbili mfululuzo,na kuweza kujadili swala la zito kama msaliti. Tumelipokea kwa mikono yote miwili,kwani tulikua tunasubiria kwa hamu kujua hatma ya msaliti ambaye ndiye alikua kirusi ndani ya chama.
Kwahiyo sasa tunawapongeza kwa kufanya maamuzi magumu. Kwa kudhihirisha pongezi zetu kweni na kuonyesha sisi kama sisi bado tupo imara na tunaendelea kujenga chama kwa njia yeyote iwezekanayo.

Wanachama wenzangu na mashabiki wa cdm,nawaombeni tuungane kwa pamoja kwa kulike ama kukomenti ili tuonyesha tupo imara na kuwatia moyo viongozi wetu waweze kututumikia katika kukijenga chama ili tuje kuchukua dola na kushughulikia wale wote wabadhirifu wa mali ya uma kama lowasa,kikwete na CO yake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom