Ufafanuzi wa kina kuhusu Utatu Mtakatifu: Je, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni Mungu watatu?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Kuna watu wanaojiuliza: “Kama Mungu ni mmoja, kwa nini Wakristo husema kwamba kuna Baba, Mwana na Roho Mtakatifu? Je, wanaabudu Mungu watatu?"

Kabla ya kujibu swali hilo ngoja nieleze nafsi ya mwanadamu ni nini. Ukiielewa nafsi ya mwanadamu itakuwa rahisi kufahamu vizuri nafsi tatu za Mungu au Utatu Mtakatifu.

Maandiko yanatuonyesha kuwa mwanadamu ana sehemu tatu kuu: nafsi, roho na mwili.
“Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.” (1 Wathesalonike 5:23)

Nafsi ni utu wa mtu unaojumuisha akili, hisia na mapenzi; roho ni kiini cha ndani kabisa kinachowasiliana na Mungu na mwili ni sehemu ya nje inayoonekana.

Nafsi ni sehemu ya kati ya utu wa mwanadamu, inayomfanya afikiri, aamue, na ahisi. Mifano ya kibiblia:
“Nafsi yangu inamhimidi Bwana...” (Zaburi 103:1)
“Nafsi yangu imejaa huzuni...” (Zaburi 119:28)

Maandiko hayo yanaonesha kuwa nafsi ni sehemu hai ya mtu, yenye utambulisho wa kipekee.

Mwanadamu ana nafsi moja tu. Je, Mungu naye ana nafsi moja kama mwanadamu? Jibu ni hapana. Mungu sio mtu kama sisi. Yeye ni wa kipekee, anazo nafsi tatu bila kuwa miungu watatu kwa sababu Uungu hauna mipaka kama ubinadamu.

Hebu tuangalie sasa kwa kina Utatu Mtakatifu au Nafsi tatu za Mungu mmoja:

Katika Biblia, Mungu amejifunua katika nafsi tatu tofauti:
1. BABA ni Mungu. “Neema na amani zitokazo kwa Mungu Baba…” (Wagalatia 1:3)
BABA ni nafsi ya kwanza, chanzo cha mpango wa wokovu. Baba anapenda, anatuma, anasema...

2. MWANA (Yesu Kristo) ni Mungu. “Naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... akafanyika mwili.” (Yohana 1:1,14). MWANA ni nafsi ya pili ya Mungu. Alifanyika mwili, akafa kwa ajili yetu. Anaongea na Baba, anaomba...

3. ROHO MTAKATIFU ni Mungu. “...kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu...Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu..."
Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu. Anafundisha, anaongoza, anaonyesha mapenzi ya Mungu. Hutoa vipawa kama apendavyo (1 Wakorintho 12:11)

Je, hizi Nafsi Tatu ni miungu watatu? Hapana! Mungu ni mmoja, lakini ana nafsi tatu zenye ushirikiano mkamilifu. Sio miungu mitatu, bali ni Mungu mmoja aliye hai kwa namna tatu tofauti.

Ukisoma Mathayo 3:16–17 utaona kuwa wakati wa ubatizo wa Yesu, Yesu alikuwa ndani ya maji (Mwana); Roho Mtakatifu akashuka kama hua na sauti ya Baba ikasikika ikitokea mbinguni. Hapo Nafsi tatu zilitenda kazi kwa umoja, lakini ni Mungu mmoja. Nafsi za Mungu huongea kati yao bila mipaka.

Naamini umeelewa sasa kuwa Mungu sio kama mtu mwenye nafsi moja. Yeye ni Mungu mmoja aliye na nafsi tatu za Uungu: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

1 Yohana 5:7
"Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni: hao ni Baba, Neno na Roho Mtakatifu. Hawa watatu ni umoja.”

Haya hapa Maandiko mengine yanayofunua Utatu Mtakatifu, yaani Mungu ni mmoja lakini mwenye nafsi tatu:
Baba ni Mungu (Yn 6:27, 1 Kor. 8:6),
Mwana(Yesu Kristo) ni Mungu (Yn 1:1, Yn 20:28, Tito 2:13, Ebr. 1:8),
Roho Mtakatifu ni Mungu (Mdo 5:3–4, 1 Kor 3:16–17)
 
Lini utatufundisha ufugaji wa kuku mama mtu
Nashukuru kwa hitaji lako zuri. Waambie wanaopenda mada za kiuchumi wagonge "like" comment yako.

Ila nikifundisha ufugaji wa kuku usichukie nikiweka na vifungu
Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!" (Luka 13:34).

Injili ina-fit kila mahali hata kwenye ufugaji wa kuku wa mayai 😎
 
Mfano mwingine wa utatu mtakatifu Kwa ufafanuzi wa kibinadam tunaweza chukulia mfano
1. boss (Manager) akiwa ofisini, atafanya shughuli za kuongoza uzalishaji na kuitwa boss au CEO na watendaji wake.
2. Huyo huyo boss ana mke anayemwita mume na kutekeleza majukumu yake nyumbani Kwa mkewe
3. Huyo huyo boss ana watoto anaowajibika nao kama baba yao na majukumu yake ni kama mzazi

Kwa iyo Mungu ni mmoja katika nafsi tatu zinazotenda kazi tofauti ila lengo likiwa kuponya, kufariji, kulinda dhidi ya mwovu (Adui) na kufundisha yaliyo mema
 
Hii inaitwa circular reasoning!
Yaani source ya hoja yako ( claim)!, ndio huo huo ushahidi (evidence) !

This is a logical fallacy!
Truth Matters
Do you really understand what Circular Reasoning means?
Circular reasoning is when a claim uses itself as its own proof, for example: “The Bible is true because the Bible says so.” This becomes a logical fallacy only if someone is trying to prove something to a person who does not already accept the Bible as authoritative. But if both the speaker and listener already accept Scripture as a reliable foundation, it is not circular, it’s simply consistent reasoning within a shared belief system.

Is the Trinity Doctrine Based on Circular Reasoning?
Not at all. Within Christianity, we don’t use the Bible to “prove” to unbelievers what they reject, we teach what the Bible reveals to those who believe it. The Trinity is not based on one verse, but on the full revelation of Scripture. Christians believe in the Bible as God's word. So, quoting Scripture to explain a Christian doctrine (like the Trinity) is not circular reasoning, it is explaining what we believe from our trusted source.

Can Spiritual Truths Be Proven Outside Scripture?
Spiritual truths are not measured by laboratory tests or philosophical reasoning alone. They are revealed by the Spirit of God. According to 1 Corinthians 2:14, the natural mind does not accept spiritual things because they are spiritually discerned. So trying to validate the doctrine of the Trinity without Scripture would be like trying to explain color to someone who refuses to open their eyes!!!!
 
Mungu ana Nafsi moja tu,nje na hapo ni Dogma tu.
isaya 45:23
Mimi nimeapa kwa nafsi yangu(SIO KWA NAFSI ZANGU), ninachotamka ni ukweli, neno langu halitarudi nyuma: .

NA HAKUNA UTATU KATIKA BIBLIA.
 
Truth Matters
Do you really understand what Circular Reasoning means?
Circular reasoning is when a claim uses itself as its own proof, for example: “The Bible is true because the Bible says so.” This becomes a logical fallacy only if someone is trying to prove something to a person who does not already accept the Bible as authoritative. But if both the speaker and listener already accept Scripture as a reliable foundation, it is not circular, it’s simply consistent reasoning within a shared belief system.

Is the Trinity Doctrine Based on Circular Reasoning?
Not at all. Within Christianity, we don’t use the Bible to “prove” to unbelievers what they reject, we teach what the Bible reveals to those who believe it. The Trinity is not based on one verse, but on the full revelation of Scripture. Christians believe in the Bible as God's word. So, quoting Scripture to explain a Christian doctrine (like the Trinity) is not circular reasoning, it is explaining what we believe from our trusted source.

Can Spiritual Truths Be Proven Outside Scripture?
Spiritual truths are not measured by laboratory tests or philosophical reasoning alone. They are revealed by the Spirit of God. According to 1 Corinthians 2:14, the natural mind does not accept spiritual things because they are spiritually discerned. So trying to validate the doctrine of the Trinity without Scripture would be like trying to explain color to someone who refuses to open their eyes!!!!
If the Holy spirit is individuality,then who is spirit of the holy spirit?.
 
"...mungu wa dunia hii[shetani] amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo"
(2 Wakorintho 4:4-6)
WAKATI MMOJA, SIKU SI NYINGI TUTAYAFAHAMU HAYA YOTE ILIVYOBORA

Tuombe,

Hmmm

=== Konsayansi ===
...

Basi ndiyo yawa, kile ambacho hunukuliwa kuhusu Shauri la Yesu kuzungumza khabari za kwenda Juu mbinguni, kwa baba, ni muktadha akilifu wa UJAMII-IMANI-TUMAINI; ambavyo Udugu ndiyo 'Mahusiano ya Kinguvu' yenye kujinasibu na 'Ushirika wa Kiroho'. Hili lafanya 'Sala na Kazi' ni jambo linafungamana na kulandana na 'Makusudi Bora na yenye Kheri' kwa maendeleo ya Kweli ya Jamii / Taifa kwa kuwa 'Haki' ni ufunguo wa Amani ya Kweli na 'Riziki kwa Mafungu' -- mafungu ya Stahiki za 'Kujituma-Kuwajibika-Kutumikia'.

Yesu kuzungumza khabari za kwenda Juu Mbinguni ni metafo ya 'Sala na Kazi' ilivyo ni muktadha akilifu wa 'Metafanusi'; ambavyo kwenye TRIZANIAMU hujitokeza kama kitovu cha Mizania ya 'DHAMIRA' na 'MIONGOZO'. Hili lafanya ule UTATU MTAKATIFU katika jamii si chochote bali ufungamanifu na ulandanifu wa (1) Siasa za Nchi : Mizania ya Mwana, (2) Uweza wa Jamii : Mizania ya Mama, (3) Mipango ya Muda mfupi na Mirefu ya Ustawi wa Jamii : Mizania ya Baba...

Mizania ya "Mwana" ilivyo ni Ulali kwa Trizaniamu katika Ulandanifu wa 'Mambo ya Siasa za Nchi' ni muktadha akilifu wa Sifa-Tabia-Hadhi ya mwanajamii / Wanajamii kwenye 'Kujisikia' na 'Elimu / Upeo wa Kiakili na Maarifa / Maarifu'; ambavyo 'KUJITAMBUA (OX)' ndiko kunakoyakinisha (1) Uweza wa Kimafikara na Hisia, na (2) Utayari wa mwanajamii Kujipangia-kujiamulia-Kujiongoza mapito yake ya Kimaisha. Hili lafanya KUJICHAGULIA ni jambo linalowezekana kwa yeyote kwa kadiri ya Uweza wake kujipima / kujitathmini , kimawazo, ile dhamiri na tafakuri ya matendo yake kwa wakati, na kumbe huku 'Kumbukumbu-Uzoefu' kuwa ni ufunguo wa nasibu ya yeye kuishi kwa mazoea ama kujiongeza ili kuyamudu mambo ya 'Nafsi' -- katika fizikia ama / na metafizikia ya mambo...

Mizania ya "Mama" ilivyo ni Ulali kwa Trizaniamu katika Ulandanifu wa 'Uweza wa kujichagulia kazi' ni muktadha akilifu wa sifa-Tabia-Hadhi ya mwanajamii / Wanajamii kwenye 'Kufaa Miundo Fulani ya Kiutendaji' na 'Uwezo wa Kutenda Mambo kwa kadiri ya Miundo / Mifumo'; ambavyo 'UNASABA(OY)' ndiyo unaoyakinisha (1) Dhana ya Ujamii -- iwe labda UTAIFA / Ukabila /Ukoo n,k, na (2) Wajibu wa kivitendo kwa ajili ya MAISHA-KUISHI-UISHO ili kuifaa 'Matriksi'. Hili lafanya KUJICHAGULIA ni jambo linalowezekana kwa yeyote kwa kadiri ya yeye KUSHAWISHIKA na Mifumo ya Maisha yenye Kutawala Mapana ya Ujamii wake -- Iwe kwa Mwangaza wa Kweli ama Mwangaza wa Uongo / Hadaa / Hila n.k na kumbe huku 'Kumbukumbu-Uzoefu' kuwa ni egemeo la NIA yake kuishi sawa sawa na 'Uongo / Ujinga' ama 'Ukweli / U-JUA-ji' wa Mambo...

Mizania ya "Baba" ilivyo ni Ulali kwa Trizaniamu katika Ulandanifu wa 'Mipango na Makusudi ya Wakati hata Wakati' ni muktadha akilifu wa Sifa-Tabia-Hadhi ya mwanajamii / Wanajamii kwenye 'Kudhamiria Maendeleo na Ustawi Bora Zaidi' na tena 'Kufuatisha Miongozo Bora kwa Sheria na Kanuni za Mambo' ilivyo ni 'Uono Mifumo'; ambavyo 'METAFANUSI(OZ)' ni kitovu cha 'Ibada na Sala' ya UTU --ibada na sala kwa vile Maendeleo na Ustawi Bora Zaidi daima ni mambo ya "Subira"... Hili ndilo lafanya 'Dini' ni kichocheo cha msingi kwa ajili ya Kujumuisha UTU wa Jamii yeyote, kila jamii ina 'DINI' kwa kuwa muktadha akilifu wa 'Mila-Destruri-Jadi', katika jamii yeyote yenye haya--Duniani ama Sayarini Kokote kule Ulimwenguni, si chochote bali 'Dini'...

Basi ndiiyo yawa, TRIZANIAMU si chochote bali 'MIZANIA MARA TATU' kwa ufraktali wa 'DHAMIRI / DHAMIRA' ya mwanajamii / wanajamii wowote kisomoni; ambavyo 'Jamii-Wakati-Machaguo ya Kitaasisi-Matukio' ni dhahiri ya MAISHA-KUISHI-UISHO kwa kadiri ya Usentienti-Konsayansi-Nuru ya Ufahamu. Hili lafanya kile ambacho kwenye mapokeo ya Ukristo hufahamika kama UTATU MTAKATIFU si chochote bali nasibu ya sifa-tabia-Hadhi ya kukadirisha 'Sura na Utukufu wake Mungu' katika MAISHA-KUISHI-UISHO wetu Duniani / Kwenye 'Matriksi'...

Kwa kadiri ya sisi kufanyika na Konsayansi, Nuru yetu ya Ufahamu inaweza kujichagulia 'Ushetani' ama 'Umalaika' kwa wakati kwa kuwa (1) Kushawishika Kwetu, na pia (2) Nia zetu, daima huandamwa na (A) 'Nuru ya Kweli' : "Mwangaza Kristu", ama (B) 'Mbalamwezi ya Nyota na Mwezi' : "Mwangaza Gizani wa Lusifa"; ambavyo UTASHI ni KUJICHAGULIA kujua (Uzima wa Matriksi Lusifa / Shetani ) ama ku-JUA (UZIMA wa MATRIKSI KRISTU) na kumbe Wema na Uovu ni mambo ya 'Dhamiri' na 'Nguvu' ili kuyakinishi muktadha akilifu wa Kumbukumbu-Uzoefu ilivyo ni Fadhila na Rehema za 'ROHO MTAKATIFU'... Hili lafanya UTATU MTAKATIFU ndiyo 'Vekta Udhamirifu' kwa chochote na vyote -- iwe ni vibaya ama vizuri, kwa kuwa kila kitu kimefanyika kwa UTATU MTAKATIFU katika Uimajinishi wa 'Mfano Wa-Ke'...

Kwa kadiri ya sisi kufanyika na Konsayansi, Nuru yetu ya Ufahamu inaweza kufuzu 'Nuru ya Kristu' ama 'Nuru ya Lusifa / Shetani' ili kuakisi MAISHA-KUISHI-UISHO ulio ni 'Mbingu / Pepo' ama hata ' Kuzimu / Kuliko Laanika'; ambavyo ule usemi kuwa 'Kufa ni Faida' na 'Kristu ni kuishi' si chochote bali shauri la 'KUJICHAGULIA' katika kitovu cha Metafanusi ya UZIMA WOTE. Hili lafanya lile Shauri ya Yesu kwenda kwa Baba, aliye ni baba yetu aliye Mbinguni, si chochote bali metafo ya Undugu katika 'Nuru ya Kristu'... Mambo ya 'Imani ya Injili'...

Kwa kadiri ya sisi kufanyika na Konsayansi, Nuru yetu ya Ufahamu inaweza kutubakiza kwenye 'Himaya ya Lusifa / Shetani' ama ' Ufalme wa Mbingu / Kristu " kwa kuwa 'Dhambi' si chochote bali ule muktadha akilifu wa kukosa mwangaza sahihi wa kimifumo kwa ajili ya UTU, AKILI na UZIMA na basi kupelekea kudumu katika "Ulimwengu wa Dhambi na Mapatilizio yake : Karma "; ambavyo Mbinguni ama /na Kuzimu, kiufundi ni mahala popote tunapoishi huku tukidhihirisha UKUU KIROHO ama ANGUKO KIROHO kwa kuwa vyote viwili Ushetani ama Umalaika ni sifa-tabia-hadhi ya kujichagulia Msimamo wa Kimaisha kiwakati. Hili lafanya Ushetani ama Umalaika vyote viwili ni fanusi za Utendaji kwa Mashauri ya Kiroho/Uadilifu, Maadili na Miiko -- vitatu vinavyoyakinisha 'Kuinulika Kwetu Kiroho' ama 'Kukwama kwetu Kiroho'...

Kwa mintarafu ya haya, Sala ya Bwana aliyofundisha Yesu si chochote bali mafungu ya dhamiri na nia ili kuleta mageuzi katika maisha yetu -- kusudi tuweze kugeuza mambo ya nchi ilivyo ni 'Maisha-Kuishi-Uisho' yawe 'Mapya' na tena yawe ni yenye kuakisi 'Usafi wa Mambo ya Mbingu' ilivyo ni Utukufu Wake Mungu -- Mungu / CHANZO SENTIENTI katika UTATU MTAKATIFU; ambavyo Amani-Haki-Udugu-Uhuru ni daraja ya matendo kwa ajili ya TORATI. Hili lafanya kufuzu mafungu makuu manne ya dhamiri, ilivyo ni kujichagulia, ni kutimilisha 'Mapenzi yafanyike Duniani, Kama Mbinguni'... Na hili ndilo khasa ufunguo wa 'fumbo la Imani ya Injili'...

Kwenye 'Utaasisi wa Dini', haya ndiyo yanayofanya 'Katekisimu kwa Muumini wa Ukristo' kuwa na mafungu matatu ya Shauri:- (1) Kutafuta Kumjua Mungu (Kupitia Usafi wa Moyo na Upendo), (2) UTATU MTAKATIFU (Intelijensia ya Kujisikia katika Matendo ya Shiriki zenye Nguvu : Liturujia), na (3) Maisha katika Kristu ( Sala na Kazi : Kudhihiri Utukufu na Nguvu katika Maisha na Kujitoa katika yale yote yenye sifa-tabia-hadhi ya 'Unyoofu' na 'Mapenzi Mema' kwenye Jamii : Dhamma)...

...​
 
Bible ina ambiguities nyingi sana.
inajicontradict sana.

Mimi ni mkristo.ila msimamo wangu ni huu MUNGU ni mmoja....hana ubia wala ushirika na yeyote.

Kuna tofauti ya MUNGU na mungu.
Yesu ni mungu na sio MUNGU.
 
Naomba kuuliza je mama yake yesu naye ni Mungu au?...Ahsante mtumishi
 
Mungu ni mmoja tu anayejidhihirisha katika Nafsi tatu: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Maria ni mwanadamu tu kama sisi. Ndio sababu katika uzi huu niliandika kwamba tusimuombe Maria. Pale alipo hivi sasa hana uwezo wa kuwasiliana na Yesu kama wakati alipokuwa hai.
Soma pia uzi huu
 
Bible ina ambiguities nyingi sana.
inajicontradict sana.

Mimi ni mkristo.ila msimamo wangu ni huu MUNGU ni mmoja....hana ubia wala ushirika na yeyote.

Kuna tofauti ya MUNGU na mungu.
Yesu ni mungu na sio MUNGU.
Chonde chonde, acha kumdhihaki Yesu kwa kumwita jina la shetani, ambaye ndiye mungu wa dunia hii
 
Mfano mwingine wa utatu mtakatifu Kwa ufafanuzi wa kibinadam tunaweza chukulia mfano
1. boss (Manager) akiwa ofisini, atafanya shughuli za kuongoza uzalishaji na kuitwa boss au CEO na watendaji wake.
2. Huyo huyo boss ana mke anayemwita mume na kutekeleza majukumu yake nyumbani Kwa mkewe
3. Huyo huyo boss ana watoto anaowajibika nao kama baba yao na majukumu yake ni kama mzazi

Kwa iyo Mungu ni mmoja katika nafsi tatu zinazotenda kazi tofauti ila lengo likiwa kuponya, kufariji, kulinda dhidi ya mwovu (Adui) na kufundisha yaliyo mema
Kwa hiyo kwa nafasi yako ya boss hiyo ni nafsi yako ya kwanza; kama mume ni nafsi ya pili; kama baba ni nafsi ya tatu au ni wewe yule mmoja katika majukumu tofauti? Mfano wa kijinga!
 
Kuna watu wanaojiuliza: “Kama Mungu ni mmoja, kwa nini Wakristo husema kwamba kuna Baba, Mwana na Roho Mtakatifu? Je, wanaabudu Mungu watatu?"

Kabla ya kujibu swali hilo ngoja nieleze nafsi ya mwanadamu ni nini. Ukiielewa nafsi ya mwanadamu itakuwa rahisi kufahamu vizuri nafsi tatu za Mungu au Utatu Mtakatifu.

Maandiko yanatuonyesha kuwa mwanadamu ana sehemu tatu kuu: nafsi, roho na mwili.
“Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.” (1 Wathesalonike 5:23)

Nafsi ni utu wa mtu unaojumuisha akili, hisia na mapenzi; roho ni kiini cha ndani kabisa kinachowasiliana na Mungu na mwili ni sehemu ya nje inayoonekana.

Nafsi ni sehemu ya kati ya utu wa mwanadamu, inayomfanya afikiri, aamue, na ahisi. Mifano ya kibiblia:
“Nafsi yangu inamhimidi Bwana...” (Zaburi 103:1)
“Nafsi yangu imejaa huzuni...” (Zaburi 119:28)

Maandiko hayo yanaonesha kuwa nafsi ni sehemu hai ya mtu, yenye utambulisho wa kipekee.

Mwanadamu ana nafsi moja tu. Je, Mungu naye ana nafsi moja kama mwanadamu? Jibu ni hapana. Mungu sio mtu kama sisi. Yeye ni wa kipekee, anazo nafsi tatu bila kuwa miungu watatu kwa sababu Uungu hauna mipaka kama ubinadamu.

Hebu tuangalie sasa kwa kina Utatu Mtakatifu au Nafsi tatu za Mungu mmoja:

Katika Biblia, Mungu amejifunua katika nafsi tatu tofauti:
1. BABA ni Mungu. “Neema na amani zitokazo kwa Mungu Baba…” (Wagalatia 1:3)
BABA ni nafsi ya kwanza, chanzo cha mpango wa wokovu. Baba anapenda, anatuma, anasema...

2. MWANA (Yesu Kristo) ni Mungu. “Naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... akafanyika mwili.” (Yohana 1:1,14). MWANA ni nafsi ya pili ya Mungu. Alifanyika mwili, akafa kwa ajili yetu. Anaongea na Baba, anaomba...

3. ROHO MTAKATIFU ni Mungu. “...kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu...Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu..."
Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu. Anafundisha, anaongoza, anaonyesha mapenzi ya Mungu. Hutoa vipawa kama apendavyo (1 Wakorintho 12:11)

Je, hizi Nafsi Tatu ni miungu watatu? Hapana! Mungu ni mmoja, lakini ana nafsi tatu zenye ushirikiano mkamilifu. Sio miungu mitatu, bali ni Mungu mmoja aliye hai kwa namna tatu tofauti.

Ukisoma Mathayo 3:16–17 utaona kuwa wakati wa ubatizo wa Yesu, Yesu alikuwa ndani ya maji (Mwana); Roho Mtakatifu akashuka kama hua na sauti ya Baba ikasikika ikitokea mbinguni. Hapo Nafsi tatu zilitenda kazi kwa umoja, lakini ni Mungu mmoja. Nafsi za Mungu huongea kati yao bila mipaka.

Naamini umeelewa sasa kuwa Mungu sio kama mtu mwenye nafsi moja. Yeye ni Mungu mmoja aliye na nafsi tatu za Uungu: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

1 Yohana 5:7
"Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni: hao ni Baba, Neno na Roho Mtakatifu. Hawa watatu ni umoja.”

Haya hapa Maandiko mengine yanayofunua Utatu Mtakatifu, yaani Mungu ni mmoja lakini mwenye nafsi tatu:
Baba ni Mungu (Yn 6:27, 1 Kor. 8:6),
Mwana(Yesu Kristo) ni Mungu (Yn 1:1, Yn 20:28, Tito 2:13, Ebr. 1:8),
Roho Mtakatifu ni Mungu (Mdo 5:3–4, 1 Kor 3:16–17)
Hii imejibu maswali mengi niliyokuwa nayo, lakini hapo kwenye 1 Yohana 5:7 mbona anasema wako watatu badala ya kusema ziko nafsi tatu?
 
Ubarikiwe Saana Nimekuelewa Mungu ni Mmoja ila Ana Nafdi tatu 🙏
 
Back
Top Bottom