Wakati wa Nyerere ni wakati huo, na mfumo huo ulihitajika wakati huo. Hakuna sababu yoyote ya kuleta mjadala wa wakati tofauti tuujadili kwa wakati huu!Kumbe Nyerere hakuwa na demokrasia, alikuwa dictator mkubwa, eti huyo ndiye anakuja kuwa Mtakatifu!
Sikiliza kwa makini:
Swala la Utakatifu linamhusu kitu gani Lissu. Kama anataka kupinga utakatifu wa Nyerere aende mahala stahiki na ushahidi alio naye yeye.
Kupambana na Mwalimu hata katika enzi hizi bado inaonyesha upungufu mkubwa wa kifikra wa hawa watu. Lissu anayo mambo chungu nzima yaliyopo leo hii yanayohitaji kushughulikiwa; huo muda wa kujadili ya Nyerere yatamsaidia kitu gani.