Huyo Nyerere anayelaumiwa ndie aliyeleta huu mfumo wa vyama vingi licha ya wengi ndani ya chama chake kuupinga, na bila huo mfumo kuwepo sidhani hata huyo Lissu leo kama angekuwa anajulikana kama alivyo.
Lissu anapoendelea kwa kuzungumzia "utakatifu wa Nyerere" hapa anachoonesha ni mihemko yake tu, huu utakatifu hauna uhusiano wowote naye, ni mchakato uliopo kati ya Nyerere [RIP] na Kanisa Katoliki.
Kama Lissu anamuona Nyerere ana dhambi basi atuoneshe aliye mtakatifu ni yupi tumjue, Lissu ana tatizo la kutochagua maneno wakati wa kuzungumza, anatawaliwa na mihemko ndio maana anapokutana na kiongozi mwenye hasira za karibu, anamuadhibu.