Ufalme wa Mungu upo ndani yenu – Luka 17:21

Kama Mungu HAHITAJI kuaminiwa, Wewe nani alikuambia umuamini?

Mungu hakuniomba kwa sababu ananihitaji; ameniamuru nimwamini kwa sababu mimi ndiye ninayehitaji uongofu na wokovu. Mwalimu hahitaji mwanafunzi afaulu kwa manufaa yake, bali mwanafunzi ndiye anayenufaika. Hivyo usichanganye haja ya Mungu na haja ya mwanadamu.
 
Mnadai Mungu HAHITAJI kuaminiwa.

Sasa nyie mnayemuamini aliwaomba mumwamini?

Au mnajipa kazi ambayo hata hamjaombwa na wala huyo Mungu mnayemwamini HAHITAJI?

Mungu ameamrisha watu wamwamini. Si kwa sababu anawahitaji, bali kwa sababu wanamhitaji Yeye. Mzazi hamwambii mtoto asome kwa faida ya mzazi, bali kwa faida ya mtoto. Hivyo, amri ya kuamini ni kwa manufaa ya mwanadamu, si kwa upungufu wa Mungu.
 
Ulisema Mungu HAHITAJI kuaminiwa.

Si ndio?

Kama Mungu HAHITAJI kuaminiwa, Atakuamuru vipi umwamini wakati anajua hahitaji kuaminiwa?

Kama Mungu HAHITAJI kuaminiwa, Kwa nini akuamuru umwamini?

Huku si kutaka kuaminiwa?

Na uliseme yeye hahitaji kuaminiwa?

Huoni Contradictions kwenye maelezo yako?
 
Mungu ameamrisha watu wamwamini. Si kwa sababu anawahitaji, bali kwa sababu wanamhitaji Yeye. Mzazi hamwambii mtoto asome kwa faida ya mzazi, bali kwa faida ya mtoto. Hivyo, amri ya kuamini ni kwa manufaa ya mwanadamu, si kwa upungufu wa Mungu.
Kama Mungu HAHITAJI kuaminiwa, Kwa nini aamrishe watu tena wamwamini?

Kama kitu hukihitaji, kwa nini uamrishe watu wakufanyie?

Wakati unajua huhitaji kitu hicho.
 


Hakuna contradiction. Unachanganya "kuhitaji" na "kuamuru."

Mungu hahitaji kuaminiwa ili awe Mungu. Lakini anaamuru watu wamwamini kwa manufaa yao, si kwa manufaa yake.

Mfano rahisi: Daktari hakuhitaji unywe dawa, lakini anakuamuru unywe ili wewe upone, si yeye.

Vivyo hivyo, kumuamini Mungu hakumwongezei chochote Mungu, na kutomwamini hakumpunguzi chochote. Faida na hasara vinamrudia mwanadamu, si Mungu.
 
Mnadai Mungu HAHITAJI kuaminiwa.

Sasa nyie mnayemuamini aliwaomba mumwamini?

Au mnajipa kazi ambayo hata hamjaombwa na wala huyo Mungu mnayemwamini HAHITAJI?
Wewe unaishi katika theories za watu ila sisi ambao ufalme wa Mungu upo ndani mwetu tunaishi katika uhalisia(reality) We endelea na hizo fallacies zako na mimi niendelee kuamini kuwa nikifa nitaenda mpaka 7 dimension Robert Heriel Mtibeli
 
Hakuna contradiction. Unachanganya "kuhitaji" na "kuamuru."
Utaamuruje kitu ambacho hukihitaji?
Mungu hahitaji kuaminiwa ili awe Mungu. Lakini anaamuru watu wamwamini kwa manufaa yao, si kwa manufaa yake.
Manufaa gani?
Mfano rahisi: Daktari hakuhitaji unywe dawa, lakini anakuamuru unywe ili wewe upone, si yeye.
Daktari haamuru mgonjwa kunywa dawa. Bali anatoa ushauri tu kwa mgonjwa. Kwamba ili aweze kupona, anatakiwa kunywa dawa.

Maamuzi ya kunywa au kutokunywa ni hiari ya mgonjwa.

Si amri.
Vivyo hivyo, kumuamini Mungu hakumwongezei chochote Mungu, na kutomwamini hakumpunguzi chochote. Faida na hasara vinamrudia mwanadamu, si Mungu.
 
Wewe unaishi katika theories za watu ila sisi ambao ufalme wa Mungu upo ndani mwetu tunaishi katika uhalisia(reality) We endelea na hizo fallacies zako na mimi niendelee kuamini kuwa nikifa nitaenda mpaka 7 dimension Robert Heriel Mtibeli
Unaishi Duniani hapahapa.

Unatumia Jamii forums ya Maxence Melo kama mimi.

Halafu unasema unaishi kwenye ufalme wa Mungu?

Hizo dini zilishawapumbaza akili zenu.

Mnadhani kuna maisha mengine sehemu nyingine, tofauti na hapa duniani.

Endeleeni kuota.
 
Neno la Mungu ni kama upanga
 
Kama ndo hivyo hakuna aliye sahihi hata wewe usiyeamini uwepo wakel maana akili yako imelishwa matango pori tu
 
Yaani wewe huwezi niforce nimuamini huyo Mungu wa atheist maana naye ametokana na stori za kina Stephen Hawking kwahiyo huna jipya
 
Kama ndo hivyo hakuna aliye sahihi hata wewe usiyeamini uwepo wakel maana akili yako imelishwa matango pori tu
Usahihi unakuja kwa ushahidi, uthibitisho na ukweli ulio na logical consistency.

Huyo Mungu mnayemwamini yupo kwanza hamjathibitisha uwepo wake.

Mnaamini tu bila uthibitisho.

Na kuamini unaweza hata uongo na hiyo ni haki yako na uhuru wako wa kikatiba.

Lakini ukianza kudai hicho unacho kiamini ni ukweli lazima utoe uthibitisho wenye ushahidi, logic na reasoning.

Lazima utoe facts zisizo na contradictions wala inconsistency.

Sio kuleta hekaya zenu za vitabuni zisizo na kichwa wala miguu, mara kikapanda kikashuka!
 
Utaamuruje kitu ambacho hukihitaji?

Manufaa gani?

Daktari haamuru mgonjwa kunywa dawa. Bali anatoa ushauri tu kwa mgonjwa. Kwamba ili aweze kupona, anatakiwa kunywa dawa.

Maamuzi ya kunywa au kutokunywa ni hiari ya mgonjwa.

Si amri.

Bado unachanganya maana ya "kuhitaji" na "kuamuru". Kuamuru si lazima kuwe na uhitaji wa anayetoa amri.

Mwalimu anaweza kumwamuru mwanafunzi asome, lakini si kwa sababu mwalimu anahitaji kusoma kwa niaba yake; ni kwa faida ya mwanafunzi.

Pia, hata daktari anaweza kutoa maagizo ya matibabu, si lazima iwe "ushauri" tu. Mgonjwa ana uhuru wa kukataa, lakini ukweli wa ushauri au agizo hauondoki.

Kwa mtazamo wa dini, amri ya Mungu ya kuamini si kwa sababu Mungu ana upungufu unaojazwa na imani ya mwanadamu, bali kwa sababu mwanadamu ndiye anayehitaji uhusiano na Muumba wake.
 

Ni kweli kwamba madai yanahitaji ushahidi. Lakini tunatofautiana kwenye aina ya ushahidi unaokubalika.

Katika masuala ya Mungu, watu wengi hawadai ushahidi wa maabara kama wa kemikali, bali wanajadili hoja za kifalsafa: kwa nini kuna kitu badala ya kutokuwepo kitu, chanzo cha ulimwengu, mpangilio wa sheria za asili, na msingi wa maadili.

Pia, kusema "hujaona ushahidi" si sawa na kusema "hakuna ushahidi". Kutokukubali hoja fulani ni tofauti na kuthibitisha kutokuwepo kwa Mungu.

Mwisho, hata msimamo wa kutokuamini ni msimamo unaohitaji hoja. Swali ni: ni maelezo gani yanaeleza ukweli wa uwepo wetu kwa ufanisi zaidi?
 
Neno la Mungu ni kama upanga
Maneno yanayodaiwa kwamba ni ya Mungu ni mengi sana.

Kuna Biblia ya wakristo wanadai ni neno la Mungu.

Kuna Rastafar Bible ya Rastafarians.

Kuna Quran ya waislamu wanadai ni neno la Mungu.

Kuna Torah ya wayahudi wanadai ni neno la Mungu.

Kuna The Vedas ya wahindu wanadai ni neno la Mungu.

Kuna Tripitaka ya wabudha wanadai ni neno la Mungu.

Kuna The Guru Granth Sahib ya wasikhism wanadai ni neno la Mungu.

Kuna The Kojik ya washinto kule Japan na wao wanadai ni neno la Mungu.

Sasa kati ya vitabu vyote hivi, Neno lipi ni Neno la Mungu kweli?

Najua utasema Biblia kwa vile ndivyo ulivyo aminishwa tangu utotoni mwako.


Vivyo hivyo, Ungezaliwa kwa wayahudi ungesema Torah ndilo neno la Mungu, Ungezaliwa na kulelewa kwenye Uislamu ungesema Quran, Ungezaliwa kwa wahindu, Ungesema The Vedas.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…