Bado unachanganya maana ya "kuhitaji" na "kuamuru". Kuamuru si lazima kuwe na uhitaji wa anayetoa amri.
Kwa hiyo kama kuamuru si lazima kuwe na uhitaji wa anayetoa amri, Hiyo
amri inajitoa yenyewe tu, pasipo yeyote wa kuitoa?
Amri inawezaje kujitoa yenyewe pasipo kutolewa?
Mwalimu anaweza kumwamuru mwanafunzi asome, lakini si kwa sababu mwalimu anahitaji kusoma kwa niaba yake; ni kwa faida ya mwanafunzi.
Una elewa maana ya kuamuru?
Kuamuru ni kutoa amri. YAANI kushurutisha.
Na huyo anayetolewa amri hana uhuru wala hiari ya kupinga au kukataa.
Ndio maana ya amri, kuamuru.
Mwalimu anaweza kumshauri mwanafunzi asome. Na mwanafunzi ana uhuru na hiari ya kuchagua kusoma ama kutokusoma.
Mwalimu akiamuru mwanafunzi asome, mwanafunzi anakuwa hana hiari wala uhuru wa kukataa au kupinga. Kwa sababu ni Amri. Mwanafunzi ameamrishwa.
Sasa wewe unachanganya mara faida za kusoma wakati huelewi hata tofauti kati ya kuamuru na kushauri.
Pia, hata daktari anaweza kutoa maagizo ya matibabu, si lazima iwe "ushauri" tu. Mgonjwa ana uhuru wa kukataa, lakini ukweli wa ushauri au agizo hauondoki.
Agizo ni amri.
Ushauri si amri.
Daktari haagizi.
Daktari anashauri.
Ndio maana utasikia watu wakisema,
Madaktari wanashauri watu wapunguze Pombe.
Na sio
Madaktari wana agiza watu wapunguze pombe.
Daktari HATOI agizo.
Daktari ANATOA ushauri.
Do you understand?
Una elewa Kiswahili?
Kwa mtazamo wa dini, amri ya Mungu ya kuamini si kwa sababu Mungu ana upungufu unaojazwa na imani ya mwanadamu, bali kwa sababu mwanadamu ndiye anayehitaji uhusiano na Muumba wake.
Mwanadamu anahitaji wapi huo uhusiano na huyo Mungu?
Mimi ni mwanadamu na wala sihitaji huo uhusiano.
Wewe huo uhusiano na huyo Mungu, Unauhitaji kwenye nini?