Ufalme wa Mungu upo ndani yenu – Luka 17:21

Roho mtakatifu katajwa hapo kwa jinsi ya fumbo ...tumia akili . Wenzako tuna akili kubwa sana ya logic ndiyo maana tunaweza kutambua mafumbo magumu ...

UFALME KUWA NDANI YA WATU NI KUJAZWA ROHO MTAKATIFU KWA WACHAMUNGU WAKE (YAANI KUWA NA ROHO MTAKATIFU ) Mtu mwenye roho mtakatifu maana yake ni Ufalme wa mungu umekaa ndani yake na mwili wake umekuwa hekalu takatifu la Mungu.
 


Kudai "ni fumbo" hakutoshi.

Fumbo nalo hutafsiriwa kwa muktadha wa maandiko, si kwa mawazo binafsi.

Yesu alikuwa anawaambia Mafarisayo, ambao hata kwa imani yako hawakuwa wamejazwa Roho Mtakatifu. Sasa unawezaje kusema "Ufalme ndani yenu" maana yake walikuwa na Roho Mtakatifu?

Ukishindwa kuoanisha tafsiri yako na muktadha, basi hiyo si exegesis; ni kuisomea Biblia mawazo yako.
 
Unataka uthibitisho wa hakuna.

Utathibitishaje hakuna?

Kitu kama hakipo, Utathibitishaje hakipo?

Mwizi akiiba na CCTV cameras zikimnasa kabisa akiiba, Utathibitishaje mwizi huyo hajaiba?
 
Unataka uthibitisho wa hakuna.

Utathibitishaje hakuna?

Kitu kama hakipo, Utathibitishaje hakipo?

Mwizi akiiba na CCTV cameras zikimnasa kabisa akiiba, Utathibitishaje mwizi huyo hajaiba?

Bado hujaona tofauti. Ukisema "sijapata ushahidi wa Muumba," huna mzigo wa kuthibitisha. Lakini ukisema "Hakuna Muumba," umefanya dai kuhusu uhalisia, na dai hilo linahitaji sababu.

Mfano wako wa mwizi umekosea. Tukio la wizi lina ushahidi wa moja kwa moja (CCTV). Lakini wewe unadai kwa uhakika kwamba hakuna Muumba wa ulimwengu wote. Umefanya uchunguzi wa kila uwezekano hadi ukafikia hitimisho hilo?

Kutamka "hakuna" si ushahidi; ni hitimisho ambalo linahitaji hoja.
 
Wewe mbona ubongo wako ni mbovu sana ..wewe umeeleza vyema kuwa kuna logic mbili
1)ufalme kuwa ndani yao
2)na ufalme kuwa kati yao.
Sasa hapa umeweka logic moja tu na kuihusisha na Mafarisayo ..yaani logic ya UFALME KUWA NDANI YAO (ambayo ndiyo nimekuambia ni kujazwa Roho Mtakatifu) ila ile logic ya UFALME KUWA KATI YAO UMEIFUMBIA MACHO wakati ulitaja mwenyewe ...sasa jibu langu kuhusu Mafarisayo ni kuwa ni kweli hao Mafarisayo ambao Yesu anawajibu hawakuwa na Roho Mtakatifu ndani yao hivyo wao UFALME ULIKUWA KATI YAO SIYO NDANI YAO
 

Sasa umebadili tafsiri katikati ya mjadala. Mwanzo ulidai "ndani yenu" ni Roho Mtakatifu, lakini ulipoonyeshwa kwamba Yesu alikuwa anawaambia Mafarisayo, ukakimbilia "kati yao."

Hiyo si hoja, ni kubadilisha tafsiri ili kuokoa dai lako. Chagua tafsiri moja na uithibitishe kwa muktadha wa maandiko, si kwa kubadili maana kila unapobanwa.
 
Dai lako la kuna muumba lina ushahidi na uthibitisho?
 
Soma
Hapana soma comment zangu toka nyuma nilikubaliana na wewe kuhusu hoja mbili ila nikakuambia kuwa hizo hoja mbili zote ni sahihi na Yesu alizikusudia hivyo ila hiyo niliyo jibu kuhusu Roho mtakatifu pekee ilitokana na swali lako ulilo lenga Roho mtakatifu . Toka mwanzo nimekuambia kuwa logic zipo mbili ..moja ndiyo yenye maana ya kujazwa roho mtakatifu
 
Dai lako la kuna muumba lina ushahidi na uthibitisho?

Swali lako halijibu nilichokuuliza.

Nilikuuliza utoe sababu za dai lako la "hakuna Muumba," wewe umebadili mada na kuuliza kuhusu dai langu.

Kama unaona dai la "kuna Muumba" halina ushahidi, unaweza kulipinga. Lakini hilo halifanyi dai lako la "hakuna Muumba" kuwa limethibitishwa.

Hoja mbili tofauti hazithibitishani kwa kuangusha nyingine.

Jibu kwanza dai lako, kisha tujadili langu.
 

Tatizo si kusema kuna "logic mbili." Tatizo ni kuthibitisha kwamba Yesu alikusudia maana zote mbili kwa wakati mmoja. Hilo bado hujalithibitisha kutoka kwenye muktadha wa Luka 17:20–21.

Muktadha unaonyesha Yesu alikuwa akiwajibu Mafarisayo kuhusu kuja kwa Ufalme wa Mungu, si kutoa mafundisho kuhusu kujazwa Roho Mtakatifu. Ukidai kuna maana ya pili, leta ushahidi kutoka kwenye maandiko, si madai yako.
 
Na wewe jibu kwanza dai lako ambalo halijathibitishwa.

Vinginevyo usirukie kuhesabu mbili wakati umeruka moja.
 
Jagina soma hii comment
 
Jagina soma hii comment

Hayo ni madai yako, si yanayotokana na muktadha wa Luka 17:20–21.

Umeongeza maana ya pili bila Yesu kuisema katika kifungu hicho.

Muktadha unaonyesha Yesu alikuwa akiwajibu Mafarisayo kuhusu swali lao la kuja kwa Ufalme wa Mungu, si kutoa fundisho kuhusu kupokea Roho Mtakatifu.

Ukidai Yesu alimaanisha yote mawili kwa wakati mmoja, onyesha ushahidi kutoka kwenye kifungu hicho.

Usiingize mafundisho kutoka sehemu nyingine halafu useme ndiyo maana ya Luka 17:21.
 
J
Je, katika vitabu vyote unajua nini kipo in Common vyote vinapoint kwamba kuna Creator of the Universe ambae ni Mungu Baba..
Mimi sihitaji kumuona Mungu physically niamini yupo ila yale anayotenda ambayo ni zaidi ya fahamu zangu anavyogusa maisha yangu na familia yangu sihitaji kumuona ndio niamini bali kwa yale atendayo kwangu ndio kinanifanya nizidi kumpenda, kumuamini na kuongeza nguvu ya Kumjua zaidi
 
Na wewe jibu kwanza dai lako ambalo halijathibitishwa.

Vinginevyo usirukie kuhesabu mbili wakati umeruka moja.

Unakwepa hoja.

Mimi sijasema dai langu halihitaji kujadiliwa. Ninachosema ni kwamba wewe pia umefanya dai la "hakuna Muumba."

Huwezi kukataa kujitetea kwa kisingizio cha "jibu lako kwanza." Kama unaamini hakuna Muumba, toa hoja zinazounga mkono dai lako. Kukwepa si ushahidi.
 
Sasa umekubali kuwa sikuchengesha maneno kwa kudai kuwa Mafarisayo wana roho mtakatifu...kwa sababu mimi sikusema kuwa Mafarisayo wana toho mtakatifu kama ulivyo nilisha maneno ....sasa kuhusu hoja ya logic mbili wewe mwenyewe ndiyo ulileta tena ni hoja sahihi kabisa ukukosea ila ulicho kosea ni weee kutia muhuri kuwa ni lazima iwe ni logic moja tu sasa swali langu kwako ni kwa nini wewe unadhani ni logic moja tu siyo zote mbili ? Je ulifikiri kwa kina ndiyo ukaja na itinisho kuwa logic hapo ni moja tu ...kinacho fanya utata hapo ni lugha za tafsiri ila kwenye lugha ya asili logic zote mbili zilikuwa ndiyo zimekusudiwa ..kuhusu ushahidi upo ndani ya biblia . Yesu anasema..wakutanikapo wawili au zaidi mimi nipo kati yao ..pia yesu anasema nitakuja kufanya makazi ndani yako ..ulimwengu aunijui bali wewe unanijua kwa sababu nakaa ndani yako...
Sasa hapa kilicho bora zaidi ni Mungu kuwa ndani yako kuliko kuwa kati yako...mfano tutizame kifa cha wanaisrael na mtume musa ...Mungu anasema nilikuwa kati ya waisrael.. ila tunajua kuwa waisrael wapo waliokuwa waovu katikati yao ila ndani ya musa mungu alikuwa ndani yake na ndani ya wachamungu wa kweli .. hivyo tunaona kundi moja tu la waisrael ila ndani yake wapo ambao Mungu yupo ndani yao na ambao mungu yupo kati yao.
 
Dai lako kwamba Kuna Muumba halina ushahidi wala uthibitisho.

Ni imani uchwara tu za vitabuni.

Full stop.

Usilete maelezo mengi hapa.
 

Bado hujathibitisha hoja yako. Umeleta mistari mingine ya Biblia na kuirudisha kwenye Luka 17:21 kana kwamba lazima iwe na maana ileile.

Huo si ushahidi; ni kuchanganya muktadha.

Swali langu ni rahisi: Ni wapi katika Luka 17:20–21 Yesu anasema alikuwa anafundisha kuhusu Roho Mtakatifu? Hakuna.

Muktadha wa kifungu hicho ni swali la Mafarisayo kuhusu kuja kwa Ufalme wa Mungu.

Ukitaka kudai kuna maana ya pili, uthibitishe kutoka kwenye muktadha wa kifungu hicho, si kwa kuazima mistari ya sehemu nyingine.
 
Wewe ulisema nimebadili hoja nimekuonyesha kuwa toka mwanzo nilijenga hoja zangu kwenye logic mbili ..... wewe unaleta ubishi mafii umesha elewa ukweli maana hata wewe ulieleza ila haukujua tu kuwa kuna Roho Mtakatifu katajwa sehemu ..kuhusu logic mbili ni swala la lugha hata katika kiswahili au kismarabu kuna hayo mambo sana ya lugha kukosa uzito sawa na lugha nyingine kwenye kufafanua mambo
 
Dai lako kwamba Kuna Muumba halina ushahidi wala uthibitisho.

Ni imani uchwara tu za vitabuni.

Full stop.

Usilete maelezo mengi hapa.

Kurudia "hakuna ushahidi" si hoja.

Wewe bado hujatoa sababu ya dai lako la "hakuna Muumba."

Kukataa dai langu hakuthibitishi dai lako.

Matusi kwa imani hayachukui nafasi ya ushahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…