Ufaransa: Kwanini walinzi wa Rais Samia wanavaa Barakoa ya Zanzibar kwenye ziara ya Tanzania?

Kunauwongo sana juu ya chato,,hakuna kitu chaaana labda uwanja wa ndege
 
Ivi ile Tai, hakuna nguvu za Giza kwy Tai. Wengineo wanasema ile ni ............
yawezekana maana havuagi hiyo tai jamaa licha ya kwamba inamfanya aonekane kituko akibadilisha ni amevaa skafu
 
Wale walinzi labda ni Wazanzibari. Lakini nilikwenda Ikulu siku moja wakaniuliza kwa nini nimevaa barakoa nyeusi ambayo haifanani na nyingine. Sasa wao wamevaa hiyohiyo. But maybe this is not important. Isipokuwa in vizuri kunotice mambo kama haya. Inaonyesha you are observant.
 
Muungano ni suala lenye baraka na lenye tija kila siku. Watu hutafuta sababu za kuungana, udhaifu kwenye muungano hauwezi kukosekana.

Suluhisho sio kila upande kutanguliza kiburi chake na ufahari wa ukubwa wa eneo lake. Haya yote yanakuja kwa kigezo cha SSH kuwa mzenji.

JPM alivyokuwa anaipendelea Chato hakuna hata mmoja aliyekumbuka kuwa ipo Zanzibar. Tuondokane na kuendekeza chuki kwa kigezo cha tume ya Warioba na ya Nyalali.
 
Wazanzibar hawahawa waliowaleta mashehe wa uamsho bara ili wale msoto.
 
Tanganyika imeshakufa mkuu huko mtaani. Kama walishindwa kuifufua kina Jenerali Ulimwengu kipindi kile wakiwa na wabunge kwa kauli thabiti ya hayati Nyerere haupo uwezekano ikaweza kufufuka leo hii.

Ushauri wangu kwa Zenji ni kukuza sekta ya utalii kwa nguvu zao zote ili waweze kuondokana na hizi dharau humu JF.

Huu utanganyika wetu hauna mashiko, ni nchi inayoundwa akilini mwa watu kihisia zaidi, tukija katika kuifanya iwepo kiuhalisia haina kabisa misingi imara.

Masuala ya sultan ni ya zamani sana, wanaweza kujitegemea na kusimama wao kama wao.

SSH anavyozunguka huko nje ni kwa maslahi mapana ya JMT, hizi akili za kujitenga ni za kimaskini na zinachagizwa na chuki ambayo wenye akili wamekataa kuinunua.
 
Mbona sioni tatizo?
 
Una roho ngumu sana hadi barakoa inakutesa ukiizela wewe lazima uwe mchawi

Sent from my VFD 600 using JamiiForums mobile app
 
Reactions: Tui
Kwani zanzibar sio tanzania

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Hili ni kosa kubwa sana.

Huyo ADC kachemka.
 
Binadamu hamna jema kila kitu kibaya kwa huyu Mama na kwa kila Raisi aingiaye madarakani
 
Reactions: Tui
Huwezi kubadilisha Maji kuwa mafuta wala mafuta kuwa Maji Tanzania itabaki kuwa nchi na zanzibar ni sehemu ya Tz
 
kwa shida iko wapi hapo mjomba...........acha kukuza mambo
 
Reactions: Tui
Mama Yaoo si Mzanzibari

Kiuchumi wa blue ni wapii???
Ukijua hayo hutouliza swali

Mwisho

Mama yoo katokea wapi ,alipandia ndege wapii
 
Tanganyika imeshakufa mkuu huko mtaani.
Si kweli, fungua katiba ya Zanzibar, Sura ya kwanza ibara ya 2. '' Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania''
Haya ni maneno ya Katiba ya Zanzibar 1984 toleo 2010.
Nchi moja ni Zanzibar , nikuulize ya pili ni ipi ikiwa Tanganyika ilishakufa mtaani?
Kama walishindwa kuifufua kina Jenerali Ulimwengu kipindi kile wakiwa na wabunge kwa kauli thabiti ya hayati Nyerere haupo uwezekano ikaweza kufufuka leo hii.
Hoja hii ni nzuri sana. Wakati wa Mwalimu suala la G55 lilikuwa wazi na liliongelewa kwa uwazi.
Mwalimu alisema ''
Sera za CCM ni serikali 2, wanaotaka sera tofauti waondoke ndani ya chama kwanza ili wakazungumzie huko'' Hapa maana yake hakukataa hoja, alisema kuwa hoja iliyopo ni kinyume cha sera wanayo inadi. Mwalimu alikuwa na nguvu za hoja

Kumbuka kabla ya hapo kulikuwa na hoja ya Watanganyika kwenda Zanzibar kwa Passport. Tanganyika ikasema ikiwa ni hivyo, Wazanzibar waje na Passport. Mwalimu Nyerere aliitazama hoja akaona ina mantiki. Mwl akawasiliana na Jumbe na sharti liliondolewa mara moja.
Mwl hakuwalazimisha Wazanzibar bali Wazanzibar waliona hasara !

Ninachokiona sasa hivi ni tofauti kidogo. Hoja 'hoja zinapigwa rungu hazijibiwi'' kumbuka asilimia zaidi ya 80 ni ya kizazi kilichokuta muungano. Hofu iliyopo ni kuwa wajenga hoja kama Mwalimu, na wasikiliza hoja kama Mzee Warioba hawapo tena. Sasa tuna ''wasifiaji na wakujipendekeza''
Hoja ya anganyika inafukuta na siku Watanganyika wakisema enough is enough hakuna wa kuwazuia. Wao ndio wenye muungano kwa hali na mali. Kuna mahali nimesema, kwa jinsi nionavyo, na ninaweza kuwa wrong! muungano uki survive miaka 5 utadumu miaka 50. Trust me!
Ushauri wangu kwa Zenji ni kukuza sekta ya utalii kwa nguvu zao zote ili waweze kuondokana na hizi dharau humu JF.
Hakuna tatizo la Zanzibar kustawi! kuna tatizo la ustawi wao kupatikana kwa gharama za Mtanganyika na hapo ndipo mjadala ulipo. Zanzibar waende kukopa Trilioni 100 hakuna shida, lakini wakikopa bilioni 280 na kumtupia Mtanganyika mzigo kuna tatizo.
Zanzibr hata wakiuza visiwa hata Ikulu hakuna tatizo, lakini uuzaji wao usibebeshe mzigo Mtanganyika kwa njia yoyote ile.
Huu utanganyika wetu hauna mashiko, ni nchi inayoundwa akilini mwa watu kihisia zaidi, tukija katika kuifanya iwepo kiuhalisia haina kabisa misingi imara.
Katiba ya Zanzibar sura ya kwanza ibara ya 2 na katiba hiyo hiyo imetaja muungano mara 36.
Tueleze wanaJF, ni sheria ipi na ya mwaka gani imetamka kuwa ''Tanganyika imekufa?''
Lakini pia katiba ya mpito ya 1964 ilisema '' ...mambo yote ya Tanganyika yatakuwa ya JMT'' in other word Tanganyika is subsumed by URT. Since
Masuala ya sultan ni ya zamani sana, wanaweza kujitegemea na kusimama wao kama wao.
Ndicho tunataka! Wajitegemee bila kumpa Mtanganyika gharama. Kwasasa Zanzibar inachukua sehemu kubwa sana ya bajeti ya JMT kuliko eneo lolote la Tanganyika ikiwa na mchango SIFURI, zero, Nada, Nil katika muungano
SSH anavyozunguka huko nje ni kwa maslahi mapana ya JMT, hizi akili za kujitenga ni za kimaskini na zinachagizwa na chuki ambayo wenye akili wamekataa kuinunua.
Hoja ni kuwa muungano unageuka kuwa mzigo kwa Tanganyika. Kinachotakiwa na uwajibikaji wa Zanzibar katika muungano. Kuhusu chuki hakuna kitu kama hicho bali zipo hoja kama hizi
1. Nini mchango wa Zanzibar katika JMT?
2. Ikiwa Zbar ambaye ni mshiriki wa JMT yupo, Tanganyika yupo wapi na Zbar inajadiliana na nani?
3. Katika JMT, masilahi ya Tanganyika yanalindwaje na kusimamiwa na nani?
3. Tueleze tamko lililoua nchi ya Tanganyika na ni kwa sheria ipi
4. Kero za muungao zimemalizwaje na kwanini imebaki siri kubwa
5. Tume ya Jaji Nyalali, Jaji Kisanga na Jaji Warioba na maoni ya Wananchi zinataka serikali 3, tueleze ni utafiti au tume gani nyingine yenye maoni tofauti na hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…