Yes inaonekana ya kitoto lakini kuna mantiki ndani yake. Ingalikuwa mtu huyo kavaa barakoa yenye bendera ya Tanganyika hilo lingekuwa jambo kubwa na si dhani Rais angelikubali.
Swali, ikiwa ni Rais wa JMT ikiwemo Zanzibar, kwanini zisitumike nembo na alama za JMT?
Kuna kitu hakipo sawa, ukizungumzia Utanganyika ni haramu, unataka kuvunja muungano.
ukizungumzia Uzanzibar hilo ni halali na sawa, ni watu na eneo special
Mambo haya ni madogo sana lakini jiulize kwanini yanachukua sura kubwa kuliko yalivyo!
Jibu ni moja kuna tatizo ! Kuna manung'uniko yanayopuuzwa ya Wadau wa muungano.
Kuna manung'uniko kama yale ya Rais AH Mwinyi na G55. Historia inaweza kujirudia na kwa hakika, kama muungano utavuka salama miaka mitano ijayo basi utakuwa salama miaka 50 ijayo.
Kuna njia ya kunusuru hali, katiba mpya , Tanganyika ya machogo irudi kwa ajili ya Machogo!
JokaKuu Pascal Mayalla