Tetesi: Ufisadi: Inasemekana kila mwanakikundi wa ngoma kutoka Bagamoyo walioenda Marekani matumizi kwa siku ni milioni 3!

Tetesi: Ufisadi: Inasemekana kila mwanakikundi wa ngoma kutoka Bagamoyo walioenda Marekani matumizi kwa siku ni milioni 3!

Cha ajabu zaidi mpiga ngoma mmoja ni afisa utamaduni wilaya fulani na kuna mkata viuno ni afisa mapato wilaya fulani
 
🇹🇿 Milioni tatu ni fedha ndogo sana kwa mtu aliyelipwa kwa safari nje ya nchi

🇹🇿Ugonvi wangu ,hivi vikundi vya mjini vimeua kabisa utamaduni wa nchi yetu

🇹🇿 Kuna wale wazungu wa scandnavia ambao huja mjini kwenye hivi vikundi huchanganya madude yao kuanzia mavazi na mifumo ya ngoma na kuleta kitu tofauti kabisa

🇹🇿 Ngoma za utamaduni za sasa hazina tofauti na kwaya au bongo fleva

🇹🇿 Ngoma unavaa sare za nguo, nyingine zenye ujumbe kama T- shirt, ngoma unaimba muda mreefu kuna tofauti gani na kwaya?

🇹🇿 Ngoma ninazozifahamu mimi manju na kundi lake wakivamia jukwaa watoto wadoga lazima walie

🇹🇿 Naona siku hizi hata matarumbeta yamekuwa sehemu ya ngoma zetu na ndio yanapokea wageni kuwaonyesha utamaduni wetu😀

🇹🇿 Nchi ya Tanzania yenye utajiri wa utamaduni ambao hutunzwa na kuhifadhiwa kwenye ngoma za kienyeji sasa wana hatudumishi kwa mashindano ya ngoma kama zamani kuanzia umishumta na mashindano yaliyokuwa yanaandaliwa na wizara

✅Ndugu zangu tuliwahi kushuhudia ngoma zinazochezwa na kundi la MWANALYAKU la Magu mkoani Mwanza?

✅ Tuliwahi kushuhudia ngoma za MAWINDI kutoka Singida wakiwa wamevalia full maleba?

✅ Tuliwahi kushuhudia MGANDA WA KIKUTU kutoka Morogoro na MGANDA wa Nyasa?

✅ Tuliwahi kushuhudia ngoma ya UKALA kutoka kule Tanga?

✅ Tuliwahi kuona ngoma ya MAGUNO YA JESHI kutoka kule shinyanga?

✅ Tuliwahi kushuhudia kikundi cha NYOTA NJEMA kutoka ukerewe?

✅ Tuliwahi kushuhudia SINDIMBA original kutoka kushini wanaovaa nguo za jadi na kubeba mifano ya wanyama kama komba, kuvaa mangongoti na kuzungusha viuno kama feni na sii hizi sindimba za kisasa zilizochanganywa na uskandnavia zinazochezwa na vyuo vya utamaduni na vikundi vya mjini

🙆‍♀️ Nchi tumepoteza utamaduni, inatokea mtu akienda nje ya nchi anashindwa hata kujua kabila lake wanavaaje, inabidi ajifanye mmasai sasa kituko kwa sababu anaiga dressing inamshinda mwanaume anavaa mavazi ya kike kumbe wana mifumo yao? Dini nazo tumezipokea vibaya na sasa tunajifanya ni wazungu na waarabu
 
View attachment 2193728

Hapo juu ni picha ya kikundi cha ngoma kutoka Bagamoyo walioambatana Samia huko Marekani.

Duru zinatabanaisha kila mwana kikundi ameidhinishiwa kitita cha milioni 3 kama matumizi yake awapo huko hiyo ni pamoja na gharama za hotel.

Ikumbukwe gharama zote hizo ni kwa muda wa wiki mbili.

Nb: Karibu Tanzania nchi ambayo bodaboda ukimtazama tu anawasha pikipiki 😄!
Diamond anaingiza sh ngapi kwa wiki mbili?
Wacha nao wale keki ya taifa...
Wewe kama umefikisha umri wa kustaafu na hujajenga, pole sana...
 
View attachment 2193728

Hapo juu ni picha ya kikundi cha ngoma kutoka Bagamoyo walioambatana Samia huko Marekani.

Duru zinatabanaisha kila mwana kikundi ameidhinishiwa kitita cha milioni 3 kama matumizi yake awapo huko hiyo ni pamoja na gharama za hotel.

Ikumbukwe gharama zote hizo ni kwa muda wa wiki mbili.

Nb: Karibu Tanzania nchi ambayo bodaboda ukimtazama tu anawasha pikipiki 😄!
Fursa Yako utaipatia umoja party endelea endelea kupambana pambana Kwanza,mambo maruzi hayahitaji haraka kitureal🤸
 
Mbona mwendazake alikuwa anahamisha ikulu kwenda chato na watu kibaoooo....!
Acheni nongwa mwacheni mama.
Halafu anakaa mwezi plus! Kipindi cha COVID alikaa Chato zaidi ya miezi 2 kundi nzima.
 
sasa 3MIL pamoja na hotel kwa siku USA kuna tatizo gani? .... huoni kama wakirudi watakuwa na salio la kutosha mfukoni ambalo watalileta huku beach kidimbwi na kugawana na wazalendo wengine...
Bronx,Brooklyn,Queens kuna hotel za kawaida kabisa na unafika town kirahisi...
 
Hapo juu ni picha ya kikundi cha ngoma kutoka Bagamoyo walioambatana Samia huko Marekani.

Duru zinatabanaisha kila mwana kikundi ameidhinishiwa kitita cha milioni 3 kama matumizi yake awapo huko hiyo ni pamoja na gharama za hotel.

Ikumbukwe gharama zote hizo ni kwa muda wa wiki mbili.

NB: Karibu Tanzania nchi ambayo bodaboda ukimtazama tu anawasha pikipiki 😄!
Punguza wivu 😆😆😆
 
Umeniwahi. Kwa exchange rate ya Leo wanapata Dola 1300 tu. Wakijifanya kula misosi kama ya home watarudi na mabegi tupu. Menu za misosi ukizikuta utadhani ni pesa kiduchu tu. Ukizibadilisha kuwa madafu hautakula. Jambo lingine ni Inflation marekani Iko juu kidogo.
Hiyo ml3 ni poket maney tu,hotel na vingine vyoote ubalozi ulishamaliza,
 
Hapo juu ni picha ya kikundi cha ngoma kutoka Bagamoyo walioambatana Samia huko Marekani.

Duru zinatabanaisha kila mwana kikundi ameidhinishiwa kitita cha milioni 3 kama matumizi yake awapo huko hiyo ni pamoja na gharama za hotel.

Ikumbukwe gharama zote hizo ni kwa muda wa wiki mbili.

NB: Karibu Tanzania nchi ambayo bodaboda ukimtazama tu anawasha pikipiki [emoji1]!
Mimi kama Msanii wa fani kabisaa ninaona hii post imelenga kuchafua bila facts za msingi.
 
Hapo juu ni picha ya kikundi cha ngoma kutoka Bagamoyo walioambatana Samia huko Marekani.

Duru zinatabanaisha kila mwana kikundi ameidhinishiwa kitita cha milioni 3 kama matumizi yake awapo huko hiyo ni pamoja na gharama za hotel.

Ikumbukwe gharama zote hizo ni kwa muda wa wiki mbili.

NB: Karibu Tanzania nchi ambayo bodaboda ukimtazama tu anawasha pikipiki 😄!
Ni pesa ndogo sana hio kwa wiki mbili wamedhulumiwa sana, God forbid , its unfair kbsa Million 3 Marekani kwa wiki mbili hela mbuzi kbsa hio.
 
Kuna watu tutakufwa bila kuiona US, sasa wewe unakwenda kwa kukata mauno tu - upewe nini hapa duniani maana hapo si utakata hadi yabenjuke !!

Hongereni sana, sisi wengine tunapasikiaga tu huko, ila mil 3 kwa trip ya wiki mbili ni hela kidogo sana, wenzenu wanapewa dola 2,000 kwa siku kama mlikuwa hamjui.
 
Kama zinawafikia hao wasanii binafsi naona ni ndogo kwa kuwa huwa hawabahatiki kula kwa urefu wao.
 
Hapo juu ni picha ya kikundi cha ngoma kutoka Bagamoyo walioambatana Samia huko Marekani.

Duru zinatabanaisha kila mwana kikundi ameidhinishiwa kitita cha milioni 3 kama matumizi yake awapo huko hiyo ni pamoja na gharama za hotel.

Ikumbukwe gharama zote hizo ni kwa muda wa wiki mbili.

NB: Karibu Tanzania nchi ambayo bodaboda ukimtazama tu anawasha pikipiki 😄!
Sasa kabla ya kuwaza wanafisadi ebu njoo na majibu kuwa fedha ni za nani. Inawezekana unapaza sauti kumbe fedha ni za mzungu wabunifu wa Royal Tour.
Sidhani kama fedha za Royal Tour ni za umma wa Tanzania. Kama ndiyo nishawish kwa kuleta bajeti na approval procedures...
Asante!
 
Sasa ulitegemea wawekewe kiasi gani na huo ni msafara wa raisi wa nchi na sio msafara wa diwani wa buza kwa mparange... Lazima waishi kwa standard ni level ya juu M3 peaa ya kawaida kwa siku kulingana na hadhi ya uraisi na shughuli yenyewe
 
Back
Top Bottom