MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Ndg yangu katika Kristo umenena vizuri, utafanya utafiti. Wakati wautafiti wako na kushauri umuombe sana Mungu akusaidie na akupe ufahamu upate maarifa. Maneno ya Mungu yanatuambia kuwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Tena siku za mwisho kutakuwa na manabii wa uongo. Utawajuaje hawa manabii wa uongo,Yesu mwenyewe anatuambia kwa matendo yao. Sasa jiulize wakati wa Yesu hakukua na wachawi au misukule? Kwanini Yesu hakuhangaika na misukule?
Amina ndugu yangu, labda ningekuuliza unaamini kuna uchawi? na kupitia uchawi kuna watu wanakufa kichawi pia?
Pia nikupe angalizo msimamo wangu toka mwanzo ni uweza wa jina la Yesu na si kuzungumzia ukweli juu ya misukule ya kwenye huduma ya Gwajima (kwasababu sipo kwenye huduma yake kudhibitisha lakini siwezi kupinga tu bila kufata misingi ya Kiroho).
Mleta mada anapinga baadhi ya miujiza na kuita ni utapeli akidhani anamzungumzia mchungaji kama mchungaji na sio mamlaka ya jina la YESU.