Ufugaji wa kisasa wa Nyuki: Faida, Utaalam na Masoko

Vipi ukihitaji Nyuki wadogo inakuaje? Na mizinga 50 inaweza kuchukua eneo kiasi gani?

Eneo la square meter 1200 litatosha vizur kabisa na kubaki nafasi. Mizinga yetu haiihitaji kutundikwa juu ya miti, unaweza kuipanga katika stand au ukajenga bee house ya kuingia mizinga 50 yote


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu embu tupe faida za kufuga nyuki, je kama mie ni mfugaji mkubwa kabisa wa nyuki kwa mwezi ntakua naingiza shillingi ngapi?
 

Napata shida kidogo kukubaliana na mahesabu haya. assumption ni kwamba once utakapoweka mizinga yako 50, nyuki wataingia mara moja tena katika mizinga yote, Je katika hali halisi ndio ilivyo? mara ngapi watu mpaka wanahamisha mizinga baada ya kukaa mahala bila nyuki kuingia kwa muda mrefu? probably unisaidie kuna mbinu gani ya kuhakikisha nyuki wanaingia kwenye mzinga mbali na kupaka nta ndani ya mzinga! manake watundika mizinga wote hupaka nta ndani yake but still hukaa miaka nyuki hawajaingia.
 

Hiyo bei mbona imekaa kimbwiga mbwiga hivi? Ungeainisha bei ya kila kifaa badala.ya kuweka lump sum! Haiingii akilini eti nikihitaji mizinga 10 lazima na hivyo vifaa viwe 10, kwa jinsi ninavyoona kuna vifaa labda utanunua mara moja. Hiyo bei yako siyo halisi!
 
Sio lazma kusubiri nyuki waingie katika mizinga yote hamsini, ipo njia ya kuwezesha mizinga yote kuwa na nyuki kwa muda mmoja. Hayo yote utayafahamu ukifika ofisi zetu
 

Sio lazima ununue hiyo kit, ukiona huna mahitaji na vifaa vilivyopo ndan ya hiyo kit basi ni ruksa kununua mizinga pekee.
 
Sio lazima ununue hiyo kit, ukiona huna mahitaji na vifaa vilivyopo ndan ya hiyo kit basi ni ruksa kununua mizinga pekee.
Ndo maana mimi nikasema bei ilivyokaa kimbwiga mbwiga, sasa mkuu si ungeweka bei ya kitu kimoja kimoja? Ili iwe rahisi kwa mdau kuchagua vifaa anavyohitaji, sasa wewe unaweka milioni 3 jumla jumla tu!!
 
natumsini muwazima wa afya. wapendwa wanajimii forum, mimi naitwa simon nipo njombe. nina lengo la kufanya ufugaji wa nyuki sasa sina ujuzi wa kutosha. Kwahivyo nime kuja kwenu wana jamii kutafuta ujuzi hivyo naomba kama kuna mtu ana uzoefu au ujuzi huo
au anajua ni wapi naweza pata ujuzi huo naomba tuwasiliane kwa email.sregnald53@gmail.com
 

Habari ndugu yangu,

Naomba nichukue nafasi hii kujibu maswali yako japo ni ya muda mrefu ila inaweza kuwa faida kwako na kwa wengine ambao itakua mara yao ya kwanza kutembelea thread hii.

Majibu:
1. Nyuki wakubwa wana faida zaidi kwani zaidi ya kupata asali utapata mazao mengine ya nyuki kama pollen, propolis, beewax na royal jelly ambayo bei yake ni zaidi ya asali katika market.
2. Nchi yetu tumebarikiwa kwani tuna zaidi ya 33.2 hectares ambazo ni forests na woodlands mahususi kabisa kwa ufugaji wa nyuki, pia maeneo mengi ya nchi yana hali ya hewa nzuri hovyo kufanya uoto wa asili kuwepo muda mwingi.
3. Kuhusu swala la gharama inategemea na wewe umeamua kuwekeza kiasi gani cha pesa na una matajio ya kutaka kuwa unapata kiwango gani cha asali kwa mwaka.
4. Mizinga aina ya Langstroth ndo mizinga mizuri kwa ufugaji wa nyuki kwa faida kwani ni rahisi kuimudu na uzalishaji wake ni wa kiwango kikubwa sana. Una uwezo wa kuvuna hadi 20kgs kwa mzinga kwa kila mvuno. Tembelea website yetu http://www.centralparkbees.co.tz kuweza kupata mizinga hiyo na vifaa vingine muhimu.
4. Soko la asali ni kubwa kuliko uzalishaji uliopo, almost asilimia zaidi ya 50% ya asali inayozalishwa hutumika hapa nchini kwa viwanda vya vinywaji na binadamu.
5. Changamoto wanazokabiliana nazo wafugaji ni nying ila kubwa ni uwezo wa kumudu vifaa vya kisasa ili kupata product inayoendana na hitaji la soko, uelewa duni wa faida za nyuki katika maisha yetu ya kawaida ya kila siku, uelewa duni wa jinsi ya kujikinga na magonjwa na wadudu wanaoweza shambulia nyuki na kukupunguzia kipato.

Karibu.
 
Je kila sehemu unaweza fuga nyuki ama.kuna maeneo /mikoa maalum ya ufugaji nyuki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…