Hii njia inakuwa applied hata kwa nyuki wasiouma?
Nyuki walikuwepo kabla ya alizeti kuenea nchini kwetu, na kuna sehemu alizeti hakuna na nyuki wapo na wana asali bomba. Cha msingi sana kuwe na maua umbali usio pungua 4km kutoka kwenye mzinga. Nje ya umbali huo nyuki hupotea njia ya kurudia kwao. Kumbuka pollination theory.
Hakuna kipimo rasmi, ila mzinga ukiwa juu kama mita moja na kuendelea juu ni bora zaidi, hasa kwa usalama. Kuna wadudu,wanyama wadogo, maji pia yanaweza kuozesha. Kumbuka pia nyuki hukaa mashimoni !!! Maji ni muhimu sana ili wasitumie muda mwingi kutafuta maji. Ukiwa na kisima chenye maji na kiko wazi itakuwa vizuri, sio kisima kina kina kirefu, nyuki hawezi ingia huko kuteka maji, ndio maana wanapendekeza bwawa/ponds kwa sababu maji yako at ground level.
Mavuno hutegemea chakula na majira ktk eneo husika. Kuna sehemu wanavuna mara mbili kwa mwaka, may na november kama Iringa. sehemu nyingine mara moja, na kwingine hakuna kuvuna. Factor kubwa ni uwingi wa chakula na majira ya mwaka. Kukiwa na baridi na maua hakuna nyuki nao hawawezi kuwa na asali. Kwa hiyo waweza ona kwamba jibu la swali lako haliwezi kuwa sawa kwa kila sehemu. Kama msosi ni mwingi, ndani ya miezi mitano kitu kinajibu.
Asante sana mkuu Malila.
Kuna post hapo juu nimeuliza pia kuhusu nyuki wasiouma, labda unaweza kueleza kidogo management yake.
Pia ungeongezea ni aina gani ya mimea ipandwe kuzunguka eneo husika hasa kama eneo ni zaidi ya eka 40
Fuatilia link hizi mkuu;
https://www.jamiiforums.com/ujasiri...a-unapoanzisha-mradi-wa-ufugaji-wa-nyuki.html
Mkuu nina mswali mawili matatu mkuu...
Mzinga huo wa commercial unaweza kutoa lita ngapi kwa mwaka?? hasa ukizingatia kuwa uvunaji hufanyika mara mbili..
Je kama utapata eneo na ukaandaa kabisa bustani ya maua na maji ya kutosha je itaongeza uzalishaji wa asali???
Mkuu ni muda gani muafaka wa kulina asali? au miezi ipi? au kipi kiashiria sasa ni muda muafaka wa kulina asali?
Hii biashara ni nzuri sana je wapi naweza kipata mizinga kwa bei nafuu
Mzee wa Manzese,
Kuna jamaa wanaitwa THE HIVE LIMITED wamefungua ofisi yao Dar es Salaam maeneo ya Victoria (Jengo la Green Acres).
Wana vifaa vizuri sana vya ufugaji nyuki wa kisasa ikiwemo mizinga ya kisasa (langstroth hives), honey extractors, mavazi ya nyuki, smokers na vingine vingi. Pia wanatoa mafunzo ya ufugaji nyuki wa kisasa kama package ya Kit watakayokuuzia na wana soko la uhakika la asali yako yote utakayozalisha popote Tanzania.
Tembelea group website yao hapa chini:
The Hive Limited
Pia, nimeambatanisha kipeperushi chao kwa ajili ya kuona vifaa vyao na mawasiliano yao. Nafikiri nimetoa mwanga kidogo.
Shukrani na kila la kheri.
Asante sana kwa maelezo mazuri, ukisema ufugaji au shamba viwe mbali na watu unamaanisha umbali gani? Ndani ya shamba eka 10 kwa mfano katikati naweza kuweka mizinga au hapo bado watapata usumbufu?