Wadau naomba kuuliza bei halisi ya huyu kuku, sababu nimeona link ya 2013
huko Kenya anauzwa 2000kshs, (zaidi ya elfu 80 za kitanzania) pia nimeshakutana na watu humu wana-qoute zaidi ya laki kadhaa kwa kuku mmoja.. !!!
Sasa najiuliza kwanini huyu kuku ana bei kubwa hivi ?
- Je ni mtamu kuliko wengine ?
- Je ni sababu ya uadimu wake na kama ni adimu kwanini watu wengi wasijitahidi kumzalisha kama return ya investment ni kubwa kiasi hicho ?
- Je ni kweli nikiwa nao naweza kupata mteja kwa kutoa elfu 80 au zaidi kwa kuku mmoja ?, Na huyo mteja anamfanyia nini ? ni wa mbegu, uganga au kumla mchuzi ?
Maswali mengi najiuliza bila majibu..., sababu kama kweli wateja wapo na bei ndio hio inayotajwa..., maybe am in the wrong business, niambieni na mimi niweze kufaga hawa viumbe. Ingawa my business sixth sense bado inakataa this is too good to be true.