Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Miezi miwili mbona mingi sana, wiki moja paka mbili inatosha.
mimi ni hapohapo akitotoa natoa vifaranga then namwekea mayai mengine... speed ya kuzaliana imekuwa kubwa sana
 
Boss embu weka timeframe vizuri tunataka kufaham inachukua muda gani mpk unawafikisha sokoni. Na picha kuonyesha hao kuku angalau tuwaone kwa muonekano
 
Habarini ndugu zangu poleni na majukumu naomba ushauri wenu kuku wangu wanataga mayai mengi kwa mfano anaatamia mayai 12 na anatotoa vifaranga wachache sana msaada wenu wapendwa wangu nini shida zaidi?
 
Hilo tatizo lilinisumbua sana kipindi naanza kufuga kuku solution ni hizi
1.Akikisha kuku wako anahatamia bila kupata bugudha ya kuku wengine hii inasababishwa endapo utakuwa na kuku wengi wanaokaa kwenye banda dogo.
2.Weka dawa ya kuua wadudu kwenye viota vyao coz wadudu husumbua kuku na kufanya asilalie mayai vizuri ..tumia dawa kama Akheri Powder n nzuri
3.Kuku wanapoanza kutaga uwe unatoa mayai na kuyaacha machache mwisho akimaliza chagua mayai mazuri ambayo yatafaa kuatamiwa muweke aanze kuraliaNB. Sio mayai yote yanakuwa na mbegu.
4.Sio kuku wote wanauwezo sawa kuangua vifaranga wengi chagua hata matemba kadhaa ambayo yapo vizuri kwenye kuangua vifaranga na yape kazi ya kuangau vifaranga mara kwa mara.
 
Unawezaje kutambua mayai bora?
 
tATIZO NI Soko mkuu...soko linapatikana wapi? ninao wengi tuuu ila sina pa kuwauza hawa kuku wa kienyeji na ni wakubwa Mnooo.
 
Wakuu
Mimi ni mfugAji mpya ndio nimeanza now sasa naomba kuuliza kuku Wa kienyeji huwa anachukua mda gani kuanzia anapototolewa mpaka kuanza kutaga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…