Barelawyer
Senior Member
- Oct 11, 2012
- 197
- 71
Nina mpango wa kuanza kufuga kuku wa kienyeji mwishoni wa mwaka huu. Lakini hii biashara kwangu ni sawa na usiku wa giza, kama wanavyosema kila kitu kina mwanzo.
Ninaomba kujuzwa ni incubator ya aina gani inaitajika? Na incubator ya aina moja inaweza kutumika kwa mayai ya kuku wa kienyeji na kisasa(broilers).
Dhumuni nina taka kuanza kutafuta used kwenye auctions.
Waungwana,
ninafikiria kuanza rasmi ufugaji wa kuku wa kienyeji,
eneo ninalo!
lakin sasa linapokuja lile wazo la ugonjwa wa mdondo ambao huwaathiri kuku mara uingiapo ndipo ninapoishiwa nguvu!
kwani mara uingiapo huondoa kuku wengi sana!!
nilishwahi kushuhudia mahali fulani!
Je, kuna namna yeyote ya kuudhibiti huu ugonjwa?
NAOMBA UFAHAMU KWA MWENYE UZOEFU NA HAWA KUKU.
kwangu mimi navyojua ni nimashine ya kuangua vifarangaincubator ni nini? Naomba kujuzwa..
Mkuu Kubota mbona umetuachia njiani mkuu...
Tunaomba hii knowledge ya kujenge mabanda ya kufuga maeneo makubwa mfano hekari kumi...
Tuko pamoja sana mkuu....
Mkuu majukumu mengi tu lakini kila mara lazima nichungulie huu uzi...Mkuu asigwa ulipotea kabisa jamvini kwetu, ngoja naweka sawa picha na michoro maana picha na michoro zinaongea maneno zaidi ya maelezo matupu, afu mvua zikizidi ile biashara ya mkaa inachanganya sana, mgodi unatema kiaina. Nitaleta somo hilo punde. Tuko pamoja.
Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa
Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-
Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.
Habari wadau, pole na majukumu
wakati tunamsubiri Kubota ngoja tuandae na maswali pia, mimi naomba kujua kuku wanaofugwa kwa kuachiwa nje lakini wanapewa nyongeza ya chakula wanahitaji eneo ukubwa kiasi gani kwa kuku kama 200-1000
Weekend njema
Liverpool ndugu yangu nashukuru kwa kunikumbuka.tuko pamoja ktk shule hii iliyoanzishwa na mwalimu Kubota.ubarikiwe sana ndugu yanguasigwa
Kubota
Mama timmy
Mama Joe
Nawasalimu wote katika jina lake Bwana wetu Yesu Kirsto aliye hai na hata sasa!