Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Nina mpango wa kuanza kufuga kuku wa kienyeji mwishoni wa mwaka huu. Lakini hii biashara kwangu ni sawa na usiku wa giza, kama wanavyosema kila kitu kina mwanzo.

Ninaomba kujuzwa ni incubator ya aina gani inaitajika? Na incubator ya aina moja inaweza kutumika kwa mayai ya kuku wa kienyeji na kisasa(broilers).

Dhumuni nina taka kuanza kutafuta used kwenye auctions.


incubator ni nini? Naomba kujuzwa..
 
Waungwana,
ninafikiria kuanza rasmi ufugaji wa kuku wa kienyeji,
eneo ninalo!
lakin sasa linapokuja lile wazo la ugonjwa wa mdondo ambao huwaathiri kuku mara uingiapo ndipo ninapoishiwa nguvu!
kwani mara uingiapo huondoa kuku wengi sana!!
nilishwahi kushuhudia mahali fulani!
Je, kuna namna yeyote ya kuudhibiti huu ugonjwa?
NAOMBA UFAHAMU KWA MWENYE UZOEFU NA HAWA KUKU.
 
Waungwana,
ninafikiria kuanza rasmi ufugaji wa kuku wa kienyeji,
eneo ninalo!
lakin sasa linapokuja lile wazo la ugonjwa wa mdondo ambao huwaathiri kuku mara uingiapo ndipo ninapoishiwa nguvu!
kwani mara uingiapo huondoa kuku wengi sana!!
nilishwahi kushuhudia mahali fulani!
Je, kuna namna yeyote ya kuudhibiti huu ugonjwa?
NAOMBA UFAHAMU KWA MWENYE UZOEFU NA HAWA KUKU.


USHAURI UMEPATA KIJANA:

Kubota
Mama Joe
gutta
Mama timmy

Kwa heshima naombeni ushauri wenu kwa huyu member wajamen!
 
Last edited by a moderator:
kuna post humu iliandikawa na kubota ikifuatilia mwanzo hadi mwisho miamia tatizo lako litakuwa kushney post hiyo unaweza kuitafuta tittle yake inasema"zijue mbinu zangu za ufugaji wa kuku"
 
Habari wadau, pole na majukumu
wakati tunamsubiri Kubota ngoja tuandae na maswali pia, mimi naomba kujua kuku wanaofugwa kwa kuachiwa nje lakini wanapewa nyongeza ya chakula wanahitaji eneo ukubwa kiasi gani kwa kuku kama 200-1000
Weekend njema
 
Mkuu Kubota mbona umetuachia njiani mkuu...
Tunaomba hii knowledge ya kujenge mabanda ya kufuga maeneo makubwa mfano hekari kumi...

Tuko pamoja sana mkuu....

weka kuku6 pamoja na jogoo kwa sqm1 ya kulala na sqm3-4 za kurandaranda na kula kwa kuku haohao
 
Last edited by a moderator:
kubota pamoja na wadau wengine wote waliochangia "mungu awabariki" kwa mada zenu nzuri zenye manufaa kwa watanzania na taifa kwa ujumla maana hii zaidi ya shule!
 
Nmemkubali Mageti. Sihitaji degree ya ujacriamali. Ki2 ambacho nmetafuta kwa muda nmekuta nmetengewa humu na nmefarijika sana. Be blessed...
 
Mkuu asigwa ulipotea kabisa jamvini kwetu, ngoja naweka sawa picha na michoro maana picha na michoro zinaongea maneno zaidi ya maelezo matupu, afu mvua zikizidi ile biashara ya mkaa inachanganya sana, mgodi unatema kiaina. Nitaleta somo hilo punde. Tuko pamoja.
Mkuu majukumu mengi tu lakini kila mara lazima nichungulie huu uzi...

Bado nasubiri kwa hamu hizo nondo ulizoahidi kuzimwaga hapa.....
 
Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa

attachment.php


Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-

Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.








Mkuu Nakusalimu,japokuwa Uzi huu ni wa Miaka Mingi na Mimi ndiyo kwanza nauona nimevutiwa sana!! Tafadhali naomba na mimi unitumie hiyo database yako!! Natanguliza
Shukrani za Dhati!!
 
Mama Joe Hujambo lakini? Huku tu wazima wa afya njema!

Wazo lako nami nategemea majibu mazuri toka kwa wadau wenzetu!

Habari wadau, pole na majukumu
wakati tunamsubiri Kubota ngoja tuandae na maswali pia, mimi naomba kujua kuku wanaofugwa kwa kuachiwa nje lakini wanapewa nyongeza ya chakula wanahitaji eneo ukubwa kiasi gani kwa kuku kama 200-1000
Weekend njema
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru mkuu Kubota, mbinu ya JELA na kuweka alama kwenye mayai imenisaidia saaana, naendelea kuitumia.
 
Wakuu nimerejea tena kwenye story yangu. Poleni kwa kuwa kimya kidogo siku hazifanani ndugu zangu, kunawakati kichwa kinachanganywa na ishu za maisha kiasi kwamba unakosa hata appetite ya kuandika, si mnajua jamani hata ng'ombe akichanganywa na stress utowaji maziwa hushuka! Tuko pamoja leo kumekucha saafi mood iko safiii !!

Kwanza naomba niwabandikie picha hizi za mabanda yangu. Haya ni mabanda niliyokuwa nikitumia wakati huo!! Sikujenga kwa kutumia material za gharama. Ni ujumbe wangu kwamba huhitaji mtaji mkubwa sana kuanzisha ufugaji wa kuku wa kienyeji, hasa kwa wanaoishi maeneo yapembezoni ambako miti na nyasi zinapatikana kirahisi hakuna sababu watu kuishi katika umasikini uliopitiliza. Vifaa vilivyotumika kujengea mabanda yangu ni nyasi, miti, udongo kwa ajili ya matofari ya matope, mianzi kama fito, mianzi pia niliitumia kutengenezea dirisha, bati chakavu sana kwa ajili ya mlango, mabanzi (maganda ya magogo) kutengenezea fremu za mlango na madirisha, chicken wiremesh kwa ajili ya madirisha.

Kibanda kinachoonekana kwa karibu ilikuwa ni kwa ajili ya vinyoya, uwezo wake ni kulala kuku 150, kibanda cha katikati nilitumia kama store pia wakati mwingine nilikuwa nawahifadhi majogoo maana wakiwa wengi hawapandi kwa ajili ya kupigania mitetea kwa hiyo ilikuwa ikitokea hivyo ninawakuzia humo kabla sijawauza, cha mwisho juu (hakionekani vizuri) ni kibanda chenye chumba na sebule ambapo sebuleni ndiyo kuna viota vya kutagia na kuku wakubwa 120 hulala humo, chumbani ndiyo kuna viota 10 kuku wanaatamia na chumba kinafungwa waatamiaji wanawekewa maji na chakula humo chumbani hawatoki! Nitawaingizia mchoro mpate picha halisi. Pia ninawaingizia picha ya Nursery, kwa hiyo kama nilivyowaleza huko nyuma nilikuwa na nursey, jela, nyumba ya vinyoya, store na banda kubwa ambalo ndimo walimolala kuku wakubwa na chumba cha kutotoleshea vifaranga (natural incubator). Kumbukeni thread hii nimewalenga wale wasio na mitaji mikubwa. Wakuu nimerudi tena kwa nguvu mpya msikae mbali!!
 

Attachments

  • Banda 1.jpg
    Banda 1.jpg
    48.3 KB · Views: 372
  • Banda 2.jpg
    Banda 2.jpg
    51.4 KB · Views: 332
Mkuu kubota..kwanza shukran kwahii post..ubarikiwe sana...swali langu..nilipata habari kwa jamaa yangu eti ukitaka kuku asiatamie inapokuwa umefikia wakati wake unamtumbukia kichwa kwenye maji baridi!kuna ukweli wowote? Ahsante
 
Mkuu Kiteitei, nadhani kama umesoma thread yangu yote, mimi nilikuwa nikitumia njia ya JELA ambayo nimeielezea vizuri sana na ilikuwa inafanikisha kwa 100%, lakini pia namimi nilikuwa nikisikia habari ya njia ya maji kwa kumtumbukiza kuku mzima mzima ndani ya maji. Kuna Mkuu Dafo aliwahi kuchangia thread hii huko nyuma aliandika kuwa njia ya kuzamisha kuku kwenye maji ni njia mbadala wa JELA, na alisema kwamba njia hiyo inafanya kazi vizuri. Kwa hiyo Mkuu Kiteitei iliyobaki ni wewe sasa kufanyia kazi utaalamu huo ili kuona ukweli mwenyewe maana mimi binafsi sijajaribu kuona ubora wake ukilinganisha na mbinu yangu ya JELA. Tuko pamoja Mkuu!!
 
Back
Top Bottom