Lazima ujiulize maswali machache tu
a) Kwa nini unaweka maranda?
b) Kwa nini unaweka magazeti?
c) Kwa nini unafanya cover kwenye madirisha kwenye banda la vifaranga na kuachia sehemu za kupitisha hewa?
Vitu hivi ni basic na lazima kila mfugaji aelewe maana ya kila hatua.
Malanda: tunapunguza phyical contact kati ya kifaranga na sakafu, by asumming sakafu ina ubaridi na pia inatuza bacteria kwa urahisi wakati wa unyevu. kwa ku apply malanda juu ya sehemu watayoishi vifaranga basi unapunguza contact hence kupunguza magonjwa kwa vifaranga / kuku.
Magazeti unaweka juu ya malanda, hasa kupunguza vumbi, wote tunajua vifaranga hukimbia kimbia na watatimu vumbi ambalo litawafanya waugue mafua - sasa ukiweka magazeti unapunguza case hii. hakikisha hakuna phisical contact kati ya kifaranga na sakafu, pia hakikisha banda ni kavu muda wote.
Utaziba madirisha kuweka joto la kawaida la vifaranga arround 35 - 38C. kama huna umeme (Dowans) kwa ajiri ya kuongeza joto basi unaweka kutumia chemli. Jiko la mkaa ni hatari kwani carbon inayotoka hapo inaweka kuwa sumu usipokuwa mwangalifu.
Mi si daktari wa mifugo ila majarida na vipeperushi vinasaidia sana. Madaktari wataongezea.