Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ni kweli sijatambua kwa uhakika majogoo ila kwa uzoefu wangu vinyoya wenye mkia mrefu na miguu mifupi ni tetea na wasio mkia na miguu mirefu ni jogoo. Hata hivi ninampango kuwauza majogoo kiasi nilete kienyeji halisi na wale chotara weusi kwani hawa ni ndugu nami kizazi hiki ninataka kiwe endelevu. Chakula wamekula starter wiki tano. Sasa wanakula finishet ila kwakweli wanakula na majani hasa niliyolima na mchicha tiunabadilishana na mbolea! Nafasi ipo wamenikimbia hili banda la bati hawajalizoea... Nafasi ipop pili hawa wataanza kutoka nje maana mvua zimeisha. Karibu tufuge Mukaruka
 
Wakuu wachangiaji wa thread hii asanteni sana kuendelea kushare uzoefu na utaalamu wenu. Hakika kunawakati ninasisimka sana ninavyoona watu wengi wakarimu wakipeana maarifa na ujuzi kiasi hiki. Hakuna kitu kinachowatia nguvu sana watu wanaotaka kujaribu ujasiria mali kama mnapobandika picha na kutoa feedback na updates za maendeleo yenu! Ninawashukuru sana wachangiaji wote kwa ukarimu wenu mkubwa, ninachowaomba tafadhari msichoke kuleta feedback na updates za ufugaji wenu kwa wale mnaoendelea kufuga. Heshima yangu kubwa kwenu mliodadisi sana na mliomwaga uzoefu wenu na updates bila kuchoka, kwa heshima yenu japo majina yenu mtayaona nimeyaandika kwa wino mweusi lakini kusema ukweli original script nimeyaandika kwa wino wa dhahabu, heshima kwenu: Mama Joe, Mama Timmy, Asigwa, Chasha, LiverpoolFC, Mzee Mukaruka, Guta, Dafo, Madago, Popiexo!

Ninawatajeni kwa majina wachangiaji wengine wote ambao nyie ndiyo mlioleta sababu ya kuzidi kunichagiza nisimulie hadithi hii bila kuchoka, bila nyie stori hii ingekuwa nikama nimechemka na ni kihelehele changu tu! Heshima yenu kubwa kwenu:Elias Sablaki, Posho za vikao, Muhinda, Betlehem, Njowepo, Mwakijule, Tongoni, Mabaghe, Mito, Chamakh, Chama2chama, Kamuzu, Masanilo, Mickymouse, Ariflardhi, mahesabu, Wilbert1974, PcMan, Apolonary, Repture Man, Lutayega, Ankojei, Madago, Zamaulid, mjamaica, Rashid Seif, Kababi, Penelope, Popompo, Baba JJ, Malamsha Shao, Kapistrano, Singo, Zipuwawa, Gefu, Mtugani wa wapi huyo, HP1, Mpita njia, chako change, Bluetooth, Blaki Womani, KVM, lutayega, Babarita, Shadow, Akohi, Rais wa Walalahoi, Amka wewe, ugolo wa bibi, maswi, exit, No Admission, Jatelo1, Somoche, Mzito Kabwela, Makala Jr, Mzamifu, Kituko, Fidel80, Yako, Nivea, Aza, Thedealer, Yatima, bht, noboka, Mkulima wa kuku, abam, yako, safari-ni-safari, gfson win, maamuma, Henge na bemg !!

Pia shukrani kwenu viewers ambao kwa wingi wenu hamchoki kusoma thread, tumieni mbizu hizi, hakuna sababu ya kukata tamaa ya maisha kwa wale wasiokuwa na ajira na mitaji, kuna jambo unaweza kufanya likakuinua kimaisha ikiwamo ufugaji wa kuku wa kienyeji!!

JF ni zaidi ya Chuo !!
 
Ni kweli sijatambua kwa uhakika majogoo ila kwa uzoefu wangu vinyoya wenye mkia mrefu na miguu mifupi ni tetea na wasio mkia na miguu mirefu ni jogoo. Hata hivi ninampango kuwauza majogoo kiasi nilete kienyeji halisi na wale chotara weusi kwani hawa ni ndugu nami kizazi hiki ninataka kiwe endelevu. Chakula wamekula starter wiki tano. Sasa wanakula finishet ila kwakweli wanakula na majani hasa niliyolima na mchicha tiunabadilishana na mbolea! Nafasi ipo wamenikimbia hili banda la bati hawajalizoea... Nafasi ipop pili hawa wataanza kutoka nje maana mvua zimeisha. Karibu tufuge Mukaruka

Asante Mama Joe na wadau wote wa JF hususani safu yetu hii ya Ujasiriamali. Tupo pamoja na niko darasani seriously kwa kufuatilia thread hii ya Kubota na ile ya Kichwa Mbovu. Natarajia kuanza hivi karibuni niko kwenye hatua za mwisho za kumalizia ukarabati wa banda. Najua kwa uwezo na mapenzi yake Mungu na watoto wake wa humu JF TUTASHINDA NA KUUSAHAU HUU UFUKARA WA BANDIA TUNAOAMBIWA.
 
Amen Mzee Mukaruka na wengine wote kwa kweli kutaja ni ngumu tuzidi kukumbukana hapa. kazi njema. Kubota, Chasha, Kichwa mbovu, Mama Timmy, Guta, Popiexo, Akohi, Narubungo, Malila, Pawaga, Kajansi, LiverpoolFC na wadau wengine wote barikiweni kwa michango yenu
 
Mama Joe, Mama Timmy, Asigwa, Chasha, LiverpoolFC, Mzee Mukaruka, Guta, Dafo, Madago, Popiexo,

Na wadau wote, Nashukuru kwa michango yenu nimekuwa nikifuatilia michango yenu katika post hii. Mimi bado ninatatizo la kuku kutotoa mayai yote bado naendelea na uchunguzi. Kama nilivyosema hapo nyuma nilikuwa natoa mayai ili kusublisha kuku waatamie kwa pamoja, matokeo yake katika kuku watatu wote kwa ujumla wao wakatotoa vifaranga 10 kati ya mayai 45! Awamu ya pili nikaamua kila kukuatakaye taga nisimtolee mayai na aanze kuatamia kwa wakati wake. kweli kuku wakwanza katotoa vizuri, kati ya mayai 12 katota 10 . Lakini alipofuata kuku wapili kati ya mayai 12 katotoa mayai 3 tu! bado sijapata jibu mpaka sasa nasubiria wingine watatoe nione namna gani kwani nimebadilisha mazingira ya kuatamia.

Otherwise wale walitotolewa wamekua vizuri mpaka sasa ninavinyoya 22 kimoja kilikufa, kimoja kilipatwa na ugojwa wa kuvimba kichwa nikatumia mafuta ya alizeti kama alivyoshauri kubota kimepona kabisa. lishe yao bado ni starter pia na majani ninawatupia. nategemea wale wa mwanzo 10 niwabadlishie lishe sasa maana wanawiki kama ya saba sasa. tutaendelea kujulishana mandeleo.
 
Habari wadau wote wa ufugaji kuku , mlipotea sana ili tunashukuru Mungu kila mmoja anarudi na jipya jema la kushare, asante kwa feedback za LiverpoolFC na vinyowa wengi, nashukuru sana Asigwa kutushirikisha mmea wa ajabu! Kubota tunashukuru kwa kushare uzoefu wako ktk kufuga kuku wa kienyeji, kifupi mimi nilishalemaa na wa kisasa nilihitaji sana ujuzi jinsi ya kufuga hawa wa kienyeji na nashukuru nimepata ujuzi na maarifa mengi. Nimepunguza na kuacha matumizi ya madawa ya kemikali na kuegemea zaidi kwenye organics au ya kienyeji kama walivyfundisha hapa. Kupitia JF pia nilihamasika kuanzisha kibustani hata sehemu ndogo za maua na pilipili mbuzi, hoho, mbogamboga, mipapai na mitopetope imekubali vizuri na hivyo kuchangia kama chakula na dawa kwa kuku. Ninaongezea milonge ingawa nafasi ni finyu kiasi nahitaji kutanuka sasa. Ukifuata mafunzo kupitia thread hii yaani kuna kunufaika kwingi. Mimi nilianza na chotara 246 tarehe 5/2/2013 na hadi sasa wamepona 240. Sita kwa kweli walikuwa dhaifu na walikufa wiki ya kwanza na ya pili. Nawawekea picha zao wakiwa vifaranga hadi sasa nimewagawa makundi mawili. Asante wote kwa moyo wenu wa kujitoa kujibu nilipokwama, Reti kwa vifaranga na Kubota kwa mchango wako mkubwa. Mbarikiwe
Dah nafurahi sana napoona mambo mazuri namna hii yanawekwa atika picha...yaani nakutamaniajeee...

Hongera sana kwa kuweza kukuza 240 kati ya 246 kwa kipindi choote cha miezi miwili maana dangerous zone ushaivuka, Hapo inabidi uanze kujiandaa kwa mazoezi ya mikono kwa ajili ya kuokota mayai....Hongera sana
 
Mama Joe, Mama Timmy, Asigwa, Chasha, LiverpoolFC, Mzee Mukaruka, Guta, Dafo, Madago, Popiexo,

Na wadau wote, Nashukuru kwa michango yenu nimekuwa nikifuatilia michango yenu katika post hii. Mimi bado ninatatizo la kuku kutotoa mayai yote bado naendelea na uchunguzi. Kama nilivyosema hapo nyuma nilikuwa natoa mayai ili kusublisha kuku waatamie kwa pamoja, matokeo yake katika kuku watatu wote kwa ujumla wao wakatotoa vifaranga 10 kati ya mayai 45! Awamu ya pili nikaamua kila kukuatakaye taga nisimtolee mayai na aanze kuatamia kwa wakati wake. kweli kuku wakwanza katotoa vizuri, kati ya mayai 12 katota 10 . Lakini alipofuata kuku wapili kati ya mayai 12 katotoa mayai 3 tu! bado sijapata jibu mpaka sasa nasubiria wingine watatoe nione namna gani kwani nimebadilisha mazingira ya kuatamia.

Otherwise wale walitotolewa wamekua vizuri mpaka sasa ninavinyoya 22 kimoja kilikufa, kimoja kilipatwa na ugojwa wa kuvimba kichwa nikatumia mafuta ya alizeti kama alivyoshauri kubota kimepona kabisa. lishe yao bado ni starter pia na majani ninawatupia. nategemea wale wa mwanzo 10 niwabadlishie lishe sasa maana wanawiki kama ya saba sasa. tutaendelea kujulishana mandeleo.
Mkuu kuhusu suala la kutotoa vifaranga wachache ningeshauri yafuatayo...

Kabla ya kuyatupa yale mayai yaliyobaki(mayai viza) ungeyakuchunguza hasa kwa mwanga wa tochi kuona kama yalikua na mbegu au lah. Siku zote kama mayai yana mbegu na yakalaliwa kwa muda fulani ukiyamulika huwa na rangi tofauti na yasiyo na kitu. Hii itakusaidia kujua kama mayai hayo hayatotoleshwi kwa sababu ya hitilafu za uatamiaji au hayakua na mbegu kabisa...

Kama ukithibitisha kuwa hayakua na mbegu basi kuna vitu vikuu vitatu vya kuchunguza kwa umakini sana....

  • Jogoo uliyenaye si machachari katika kufanya kazi(ie ni mzembe katika kupanda majike) yake au idadi ya majogoo ni ndogo hivyo hayakidhi idadi ya majike yaliyopo,,
  • Au Majogoo na matetea yana undugu wa damu, yaani yametoka kwa mama mmoja au baba yao ni mmoja au baba anawapanda watoto wake hali hii kitaalamu huweza kusababisha utotiaji wa vifaranga vichache sana na vikikua hundamwa sana na maradhi na vifo, na vikipona hukua taratibu sana(poor growth rate)....
  • Au Mbegu uliyonayo ina matatizo kwa ujumla hivyo unahitaji kutafuta mbegu nyingine
Lakini probability kubwa iko kwenye option ya kwanza na ya pili....
 
Mkuu Guta kwa huyu anaeendelea kuatamia hebu leoleo yapime mayai kwa kutumia tochi au bulb kama nilivyowahi kutoa mfano huko nyuma kuna picha. Leo leo ukipima utajua iwapo mayai yatatotolewa au la !! Inabidi uwe unayapima mayai kama nilivyokudokeza ili ijulikane ni hatua gani hayo mayai huwa yanakufa, labda ni matatizo ya urutubishaji! Huyo kuku ambae ametotoa vifaranga vichache sana huyo mfuatilie sana huenda ndiye mwenye matatizo! Labda tatizo ni mayai kuwa na hitilafu fulani!, hiyo yote itajulikana kwa kujua ni lini vifaranga ndani ya yai hufa! Ukitazama vizuri picha za upimaji wa yai na hatua za ukuaji wa vifaranga nilivyowawekeeni huko nyuma utafuatilia kwa vizuri na utupe feedback ili tuendelee kushauriana zaidi. Pima mayai kila baada ya siku saba, siku saba za mwanzo kama yako clear kama vile limetagwa leo ujue hilo halikurutubishwa, siku 14 yai linatakiwa lifanane na picha iliyomo humu niliyowahi kubandika, ukiona halieleweki eleweki livunje utaona majibu yake! Yai zima ukilivunja utaona ute mzuri na damu! Hiyo itazidi kukupa picha kuweza kuyaelewa mayai mazima na mabovu. Ikijulikana ni lini mayai yanakufa itakuwa rahisi kuelewa kinachosababisha.
 
Wakuu Asigwa na Kubota, ahsanteni kwa ushauri wenu. Kwa kweli sijayacheki kwa kutumia tochi. Nitafanya hivyo.

Kuhusu suala la jogoo sina uhakika sana na hilo, lakini kwa muonekano ni jogoo aliyechangamka sana na anatoa huduma ipasavyo sio mvivu, mpaka naona kama mitetea niliyonayo ni michache maana nina mitetea mitano, na kunakua na wawili au watatu kwa wakati mmoja wanaatamia. Kwahiyo kila wakati huwa na mitetea wasiozidi watatu linao wahudumia. Na mitetea wote hao nimewatoa katika source tofauti hakuna hata mmoja mwenye mahusiano na jogoo. Na kati ya hao mitetea kuna walio totoa vifaranga wengi kwa mara ya kwanza. Lakini bado nitaongeza jogoo la kisasa ili nipate breed nyingine iliyocrosiwa.

Nitayapima mayai ambayo yanaatamiwa, yana siku 10 kwa sasa, lakini kuna wakati niliwahi kuvunja mayai kama matano kati ya yale yaliyokuwa yameharibika sikumbuki uwino au idadi ila kuna mengine yalikuwa na vifaranga waliokuwa wamekufa na mengine yalikuwa na majimaji tu - nadhani hayakurutubishwa au yaliharibika katika hatua za mwanzoni.

Kwakweli ninashukuru kwa forum hizi naendelea kupatauzoefu mkubwa pindi nikizoea nataka nifuge kibiashara sasa.
 
Hongera Guta, inatia moyo kweli kutotolesha kwa njia ya mama ni ngumu unajitahidi sana, nadhani ufuate maelezo ya wadaua hapo juu ikibidi umuondoe kwenye kutotoa huyo kuku mwenye matatizo au uongeze jogoo.
Asante Asigwa kwa pongezi ni kweli kipindi wakiwa wadogo bila mama kuku ni tata ila ukijaribu inawezekana, tuombe tu mayai yatakuwepo mengi na kale mmea tukikapata dah itakuwa poa sana. Ila nahofia hayatakuwa fertilized haya ya kudondoka nasubiri feedback kwa yoyote atakayeyatumia hapa.
 
Nilijalibk kwa mara ya kwanza nikapata changamoto ya ugonjwa wa mdondo
 
Mimi ninataka kuanzisha mradi wa ufugaji kuku naomba ushauri

Mkuu Fajusa, nakuomba kwanza tafuta muda pitia usome uzi wote huu mwanzo hadi mwisho, kisha kuwa wazi ungependa ushauliwe kuhusu suala lipi hasa maana mambo ni mengi, na mengi tayari yameshazungumzwa humu na wachangiaji. Huu ni ushauri wangu kwako juu ya wewe unaetaka kuanzisha mradi wa kufuga kuku.
 
Nilijalibk kwa mara ya kwanza nikapata changamoto ya ugonjwa wa mdondo

Ugonjwa wa mdondo siyo tishio kwa vile kunachanjo yake. Dawa ni kuwapa chanjo kuku wako kwa wakati kama inavyoshauriwa. Hilo limeongelewa humu kwenye thread, ipitie upate na mengine mengi.
 
Mama Joe, Mama Timmy, Asigwa, Chasha, LiverpoolFC, Mzee Mukaruka, Guta, Dafo, Madago, Popiexo,

Na wadau wote, Nashukuru kwa michango yenu nimekuwa nikifuatilia michango yenu katika post hii. Mimi bado ninatatizo la kuku kutotoa mayai yote bado naendelea na uchunguzi. Kama nilivyosema hapo nyuma nilikuwa natoa mayai ili kusublisha kuku waatamie kwa pamoja, matokeo yake katika kuku watatu wote kwa ujumla wao wakatotoa vifaranga 10 kati ya mayai 45! Awamu ya pili nikaamua kila kukuatakaye taga nisimtolee mayai na aanze kuatamia kwa wakati wake. kweli kuku wakwanza katotoa vizuri, kati ya mayai 12 katota 10 . Lakini alipofuata kuku wapili kati ya mayai 12 katotoa mayai 3 tu! bado sijapata jibu mpaka sasa nasubiria wingine watatoe nione namna gani kwani nimebadilisha mazingira ya kuatamia.

Otherwise wale walitotolewa wamekua vizuri mpaka sasa ninavinyoya 22 kimoja kilikufa, kimoja kilipatwa na ugojwa wa kuvimba kichwa nikatumia mafuta ya alizeti kama alivyoshauri kubota kimepona kabisa. lishe yao bado ni starter pia na majani ninawatupia. nategemea wale wa mwanzo 10 niwabadlishie lishe sasa maana wanawiki kama ya saba sasa. tutaendelea kujulishana mandeleo.
Hongrera sana ndugu yangu kwa hatua Hiyo!kuku Kama walivyo wanadamu kuna kuku wazembe ktk kuatamia na hata kutunza Vifaranga.chunguza kuku wako vzr na ni lazima utagundua kuku anayelalia mayai vzr na vile vile utagundua kuku mlezi.hao ndo unaweza ukawawekea mayai wa kalalia na kutunza Vifaranga.Guta ndugu yangu si lazima kila kuku anayetaga apewe mayai kuatamia.mtafute mwenye sifa za kuatamia halafu utaona matokeo yatakavyokuwa mazuri.
 
ndio kwanza na mimi ninao kuku 30,wa kienyeji,hivyo nakusubili kwa ham.....
 
Hongrera sana ndugu yangu kwa hatua Hiyo!kuku Kama walivyo wanadamu kuna kuku wazembe ktk kuatamia na hata kutunza Vifaranga.chunguza kuku wako vzr na ni lazima utagundua kuku anayelalia mayai vzr na vile vile utagundua kuku mlezi.hao ndo unaweza ukawawekea mayai wa kalalia na kutunza Vifaranga.Guta ndugu yangu si lazima kila kuku anayetaga apewe mayai kuatamia.mtafute mwenye sifa za kuatamia halafu utaona matokeo yatakavyokuwa mazuri.

Ahsante sana Mama timmy kwa ushauri wako. Tatizo linakuja pale kwa mara ya kwanza kuku yuleyule alitoa matokeo mazuri lakini kwa mara ya pili matokeo yamekuwa kinyume, na ni kuku watatu wamekuwa na tatizo hilo. anyway tutaendelea kujulishana, nimebadili setup ya banda pia nataka kubadili jogoo. thanks,
 
Hongera Mkuu,
Nami nichangie jambo hapa
1.Jaribu pia kuangalia chakula wanachokula, (Mayai yaliyo bora, Kifaranga bora mwenye nguvu hutegemea sana chakula anachokula kuku mzazi)
2.Wakati mwingine mayai yanakuwa yamepatwa na vimelea vya magonjwa toka kwa kuku wanaotaga hivyo huletea vifaranga kufa kabla ya kuanguliwa au mara tu baada ya kuanguliwa.
3.Hifadhi mayai kwa umakini na ipasavyo

all the best
 
Ahsante Reti , Nami nimeanza kupatwa wasiwasi wa chakula ninatumia zaidi concentrate nachanganya na pumba za kawaida. Je ni sahihi?
 
Niko na mitetea kama kumi ivi ndo wanataga wakitotoa vitoto tuu ,vifaranga ntavitenga na mama zao na kuanza wafeed kama vifaranga wa kisasa ili mama zao waanze maandalizi ya kutaga tena.
Hii mbinu ikitick nitawapa feedbak.
Ugumu wa maisha unakufanya uwe creative hope 2015 kutakuwa na ahueni maan wananchi tumetelekzwa bei hakushikiki akina pride na finca nao wanabana vimkopo vidgo vidogo sana
 
Back
Top Bottom