Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni jambo linalowezekana

Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni jambo linalowezekana

Ndomana nmesema baada ya majaribio kadhaa kaka nikikuonyesha kuku wangu wa kienyeji wa miezi mitatu unaweza kukataa ukazani ni wa miezi 6View attachment 2739229
Basi nipe maujanja... Kama kuna wadudu wa kula wao kwa kujitafutia, then hiyo inawezekana without doubt.
Looks nice kuku wako.... nitakuwekea wa kwangu leo uone wa miezi 2, lkn kwa kula kweli kweli

Tatizo ni kuwa wasiposhiba hawatagi in time , watachelewa sana. sawa na bata, ninao around 25, wasiposhiba hawatagi kabisa.......
 
Kaka njoo nikufundishe kumlisha kuku wa kienyeji akifikia miezi 3 watu wanamshangaa au wanasema sio kienyeji
Hongera kwa ufugaji na pia hongera kwa lengo lako. Ninapenda sana kufuga kuku, tafadhali nifundishe hapa jinsi ya kumlisha kuku wa kienyeji
 
Kama eneo ni kubwa na salama wanajiokotea wenyewe.....unaongeza matakataka kidogo toka ma dampo ya sokoni..migahawani

.
Inawezekana ila unatakiwa uwe na eneo kubwa sana ili kutoa nafasi ya wao kuzunguka na kujitafutia vya ziada, kama ukiweza kurundika mbolea nyingi, nikisema nyingi namaanisha nyingi hasa! Rundo kubwa! Hapo watajitafutia wadudu na wewe utatumia gharama kidogo kwa chakula na baadhi ya mabaki huko sokoni. Zingatia eneo kuuubwaaa!
 
Practicality yake ndiyo ngumu. Ninafuga hao wa kienyeji kama 40 hivi. Chakula kinanitoa jasho. Kilo Moja ya mchanganyiko wa pumba, mashudu alizeti/ pamba, mahindi, lukina, dagaa ni elfu moja. Wakila kilo 5 a day for six months....na unauza unapata Nini?

Nina eneo kubwa kama nusu eka, lkn hakuna chakula maana ni jua hakuna wadudu wa kuokoteza. Mahotelini labda lkn na wenyewe watakuchoka unless unalipia matakataka hayo. Dampo huko siwezi...

Kibaya soko lake ni kama hakuna. Hapa kwetu mjini ni elfu kama sh 15-35...nani uswazi atoe Hela hiyo!

Nami nilivutiwa na story kama hizi, lkn Kuna shida kidogo Kwenye chakula. Magonjwa siyo kihivyo ukiwa makini na chanjo, vitamins, minerals etc etc
Chakula bora hupunguza changamoto za magonjwa ila kina gharama, kama unaweza kuchukua huko migahawani na kukikausha itapunguza risk ya maginjwa, pia mafuta mafuta na nyama au michuzi iliyochanganyika kwenye chakula inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko. Ukaribu na kuwajibika ni muhimu sana kuuzingatia
 
Mkuu bila shaka upo kwenye mazingira ambayo yanakubana lakini mimi nipo sehemu ambayo gunia la pumba linauzwa elfu12 na nje Kuna wadudu panzi na mchwa wa kutosha bora Ata mimi hua nawapa pumba kdg majirani zangu wao wanafungulia asubuhi na wanafungia usiku
Karibu
Hongera! Lazima utaona matokeo tofauti na hao jirani zako. Safi sana
 
Kumekua na kasumba juu ya swala Zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji kuonekana kama ni swala lisilowezekana yani kufuga kuku wa kienyeji mpk kufikia idadi kubwa yani 1000, 2000 au hata 3000

Baada ya majaribio kadhaa ya kufuga hawa kuku sasa rasmi nmeingia kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa mazingatio ya hali ya juu na mpk kufkia mwezi December nataka kua na kuku si chini ya 1000.

Nmeanza na makoo 35 na majogoo 6. Mpk sasa nina vifaranga zaidi ya 50 ambao nawalea kwa kutumia joto la taa na mkaa na makoo zaidi ya 7 yanayolalia mayai yasiyopungua 15 kwa kila moja

Rafiki njoo tubadilishane mawazo juu ya mradi wa kuku wa kienyeji pure.

View attachment 2738085View attachment 2738086View attachment 2738088
Hongera Mkuu
 
mbona nitashukuru. basi weka hapa wote tufaidike or else come inbox!

All in all, nimewafuga sana na sasa nina kama 50/40 or so.

Ulaji wao unatisha... nina vifaranga 30 vya wiki moja , vinakula kg 1 ya starter kwa wiki (kwa kuwabania)! which costs 2000 per kilo. Wakifikisha mwezi itakuwaje?
Afadhali utumie nguvu kubwa kwa vifaranga hapo mwanzoni Kisha utawabadilishia chakula hapo baadaye baada ya mwezi mmoja angalau ila hakikisha unazingatia chanjo mzee. Mimi nilifikisha kuku mia na hamsini kwa muda mfupi sana ila nilikuwa nazingatia sana chakula na utaratibu wa chanjo na dawa kwa ujumla. Kadri wanavyoongezeka na kuwa wengi ndiyo changamoto ya magonjwa inavyo ongezeka pia, so ni muhimu sana kuwa na nafasi ya kutosha ukizingatia ni kuku wa kienyeji pure
 
Mkuu, naomba utoe mchanganuo wa chanjo zinazohitajika na umri. Mfano, wakiwa na siku 3 labda wapate chanjo ya ugonjwa flani au kama una dawa pendekeza kabisa jina lake.
Ahsante
 
nalo hilo ni tatizo kubwa. Tena majirani ndio wezi....
Na hii ndiyo ilinifanya niache kwanza kwa muda. Mbaya zaidi wanaachia mifugo yao inachanganyikana na ya kwako na maisha yetu ya kitanzania kwenye eneo dogo inakuwa changamoto sana. Nilichojifunza ni kwamba kuku wa kienyeji wanaweza kufugika kwa idadi kubwa na wakakulipa kibiashara ila linahitajika eneo kubwa la kutosha na ni vizuri ukawa na mfugo mchanganyiko kama vile ng'ombe ili wapate ziada kutoka kwenye mbolea
 
Mkuu, naomba utoe mchanganuo wa chanjo zinazohitajika na umri. Mfano, wakiwa na siku 3 labda wapate chanjo ya ugonjwa flani au kama una dawa pendekeza kabisa jina lake.
Ahsante
Kwa uzoefu wangu mdogo nilifuatilia kulingana na ushauri wa dakitari, pia mengine najifunza mitandaoni kama hivi, mtiririko wa chanjo siwezi kukupatia hapa kwa haraka ila ukitafuta mwongozo kwenye mitandao utapata au kamuone dakitari wa mifugo, pia unaweza kutafuta baadhi ya vitabu vyenye elimu ya ufugaji. Zaidi sana ni kuzingatia usafi na banda bora. Pia kama upo pembezoni mwa mji ni rahisi kutumia dawa za asili zaidi na nimeona zina matokeo mazuri ya haraka ukilinganisha na hizi za dukani, changamoto ya dawa za asili ni vigumu kidogo kupata mahitaji ya kutosha ukiwa na kuku wengi. Dawa hizo ni kama mkonge, aloe vera, mlonge, mpapai, mlimao mwarobaini nk, zipo nyingi na zinatibu magonjwa mbali mbali
 
M
Na hii ndiyo ilinifanya niache kwanza kwa muda. Mbaya zaidi wanaachia mifugo yao inachanganyikana na ya kwako na maisha yetu ya kitanzania kwenye eneo dogo inakuwa changamoto sana. Nilichojifunza ni kwamba kuku wa kienyeji wanaweza kufugika kwa idadi kubwa na wakakulipa kibiashara ila linahitajika eneo kubwa la kutosha na ni vizuri ukawa na mfugo mchanganyiko kama vile ng'ombe ili wapate ziada kutoka kwenye mbolea
Mimi nina eneo kubwa kidogo , relatively kulinganisha na wenzangu kama 3/4 of an acre. Wao wana 20x15 metres eneo yao. Wanafuga, hivyo kuku wote ni kwangu.... nikiweka chakula wote wanakuja pale na wameshajua kuwa pale asubuhi kuna chochote. Wakifunguliwa tu wanajaa! Tuko majirani 3 lkn mmoja niyo shida. mwizi anawaiba kweli kweli! Nina ngombe pia na kama uivyosema kuna mafunza mle, lkn ni scrable kweli keli......

Matofali ya kujenga ukuta around my area si mchezo..... hida tupu kufuga
 
Ni jambo linawezekana kabisa ila Fanya mchakato upande azolla kupunguza garama za chakula kwa 80%
Azolla ikoje mkuu, mana hata mimi ninao zaidi ya mia. Kwenye suala la chakula ndo ishu napambana nayo
 
M

Mimi nina eneo kubwa kidogo , relatively kulinganisha na wenzangu kama 3/4 of an acre. Wao wana 20x15 metres eneo yao. Wanafuga, hivyo kuku wote ni kwangu.... nikiweka chakula wote wanakuja pale na wameshajua kuwa pale asubuhi kuna chochote. Wakifunguliwa tu wanajaa! Tuko majirani 3 lkn mmoja niyo shida. mwizi anawaiba kweli kweli! Nina ngombe pia na kama uivyosema kuna mafunza mle, lkn ni scrable kweli keli......

Matofali ya kujenga ukuta around my area si mchezo..... hida tupu kufuga
Hongera pia pole kwa changamoto. Nakushauri weka uzio wa muda mfupi wa makuti ya minazi huwa yanakaa zaidi ya miaka mitatu, pia pale panapotokea udhaifu una repair. Hii itakusaidia pia kuwa na faragha ya mifugo yako na kuepusha magonjwa.
 
Back
Top Bottom