Nakushauri nunua mashine ya kutotolesha vifaranga Mkuu, ili kufikia hiyo idadi kwa muda mfupi uliowekea malengo, itakupasa kununua mayai kutoka kwa wafugaji wa uhakika mfano mashirika ya masista.
Unaweza kufikisha kuku hadi 3000 ndani ya huo muda lakini utaweza kwa kuwa na mashine ya kutotolesha vifaranga.
Ukiwa na mashine ya mayai mfano 520, itakuchukua miezi minne tu kufikia idadi kubwa ya vifaranga na hapo tegemea.kila mzunguko wa mayai 520 kupata vifaranga 400 imara yaani wale.vifaranga walioanguliwa siku ya 18 hadi 20 hao wa siku ya 21-22 huwa ni miyeyusho wanaugua na kufa hovyo.
Chakula kwa kuku wa kienyeji sio mtihani sana kama una shamba na unafahamu namna ya kuzalisha wadudu. Pia kwa aina hii ya ufugaji unatakiwa kununua chakula kwa shehena sio kagunia kamoja ka kilo 100 bali gunia 10 za kilo mia yaani ukinunua ni tani kwenda mbele.
Hilo shamba tenga kwa wavu mara nne yaani kama ni eka moja tenga nusu eka 4 kisha uwe kila wiki unawafungulia eneo moja huku mengine unanyeshea na kuotesga mchicha na kuweka mbolea ya mifugo kuleta wadudu na kukuza majani.
Uzuri kuku wa kienyeji 2000 mfano wanalala sehemu ndogo sana, pawe tu na hewa yakutosha na vichanja vya kulalia.
Baada ya muda chagua kuku wako kwa ajili ya kutaga mayai ya kuangua na hao utawatenga waishi kivyao na majogoo yao, ila kwa sasa focus kuipata hiyo idadi na kuwauza nusu baada ya kuona wana ukubwa na uzito mzuri.
Kila la heri Mfugaji, ila tambua jambo moja unahitaji mtaji wa pesa na muda.