Kumekua na kasumba juu ya swala Zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji kuonekana kama ni swala lisilowezekana yani kufuga kuku wa kienyeji mpk kufikia idadi kubwa yani 1000, 2000 au hata 3000
Baada ya majaribio kadhaa ya kufuga hawa kuku sasa rasmi nmeingia kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa mazingatio ya hali ya juu na mpk kufkia mwezi December nataka kua na kuku si chini ya 1000.
Nmeanza na makoo 35 na majogoo 6. Mpk sasa nina vifaranga zaidi ya 50 ambao nawalea kwa kutumia joto la taa na mkaa na makoo zaidi ya 7 yanayolalia mayai yasiyopungua 15 kwa kila moja
Rafiki njoo tubadilishane mawazo juu ya mradi wa kuku wa kienyeji pure.
View attachment 2738085View attachment 2738086View attachment 2738088