Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni jambo linalowezekana

Naendelea kuwapa mrejesho ndugu zangu mradi wangu unaendelea kuku wale wale waliokua wanalalia nmewarudishia mayai kwa awamu ya pili na tatu Hawa wengine nmeacha watage tu pia Kuna kitu nmejifunza kupitia Hawa kuku wa kienyeji ukimuachia nje azurure atataga kila siku na ukiwa unamfungia utagaji wake unakua ni wakusua sua sana
CHINI NI PICHA ZA VIFARANGA AMBAO WANAKARIBIA 200 SASA WA MWEZI MMOJA NA WA WEEK MOJA
PURE KIENYEJI.
 
safi mkuu. pia mcheki jamaa anaitwa mzee chicks yuko Uganda utaokota maarifa zaidi

Sent from my SHV45 using JamiiForums mobile app
 
Nataka niingie kwenye hii project by the end of this year. Nina shamba kubwa like heka zaidi ya ishirini na kuna bonde pia pembeni ya shamba. Changamoto zangu ni moja, shamba liko mbali na mm. Ni lazima nimtafute shamba boy wa kuangalia shamba na mifugo. Na pili ndani ya shamba nataka nilime mahindi na mazao mengine so hofu yangu ni kuku kula hayo mazao sasa sijui ntafanyaje hapo wadau. Lkn natamani sana kufuga kuku
 
Chagua kufuga au kulima
 
Mkuu piga kazi hao wote wanaosema utashindwa mara nyingi hawajawahi kufuga hata kuku 50 kwahyo usitoshike waliofuga wanajua
 
Akikupa gharama ya chakula utazimia
 
mifugo hailali, tunailazimisha kwa kuwaweka gizani, lakini watakiwa wale day & night kama broiler vile
 
Jiongeze mwaga maji majani yatachipua kuku watakula utawahudimia kwa muda mfupi tu halafu watajitafutia wenyewe.
 
Shamba boi aive kwelikweli ktk suala la ufugaji kuanzia chanjo kwa wkt na usafi wa vyombo na banda kwa wakati pia muda mwingi awepo site.

Pili anza na wachache hata tetea 30 jogoo 4 ili usome upepo wataongezeka wenyewe mdogomdogo usitumie gharama Sana kuwanunua.

Ingia gharama kuwatengea uzio wao ili wasiharibu mazao Yako,mabanzi/wire au Jenga ukuta Kabisa hii itasaidia pia kudhibiti vimelea vya magonjwa (biosafety)
Zaidi kumarisha ulinzi fuga mbwa ili kudhibiti vicheche
All the Best
 
Asante sana mkuu kwa ushauri huu mzuri. Nitaufanyia kazi
 
Mimi nimekuwa nawafuga kwa muda mrefu, nime maintain idadi ya 50, hawatakiwi kuzidi hapo. Na ni kwa ajili ya matumizi yangu tu nyumbani na familia. Nimeshindwa kabisa kutumia hawa wa kisasa kwa chakula. Kwa idadi kubwa nadhani gharama ni kubwa sana isipokuwa nadhani wataalamu wanaweza kushauri namna bora ya kupunguza gharama hasa chakula. Wakiwa free range ni nzuri zaidi. Unakuwa unaongezea kidogo tu hasa vifaranga ili wakue haraka kidogo.
 
Chakula kitakutoa jasho maana wanakula sana na hawakui haraka mpaka miezi 6 or so! Hutaweza!
Tatizo mnapenda kila kitu kukatishaga watu tamaa yan kijinga kuku wana faida kama huwezi kufuga waachie wenzako wafuge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…