Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko


Aman
Asante kwa kunipa mwanga,

Nimeambiwa taa ya chemli unaweza ikatumika kwenye brooder kama source ya joto, je ni Kweli?

Kama nikweli unashauri taa ngapi kwa vifaranga 1000?

Unaweza ukarecommend suppliers wazuri wa vifaranga wa mayai hapa dar?
 

emma250,
Supplier wazuri wa vifaranga wa mayai kwa Dsm na Kibaha ni mkuza, interchicks, na taasisi ya elimu kibaha. Na kwa kuku wa nyama Broiler Amadori Euro poultry Ltd.

Kuhusu kutumia taa za kandili au chemli kama source ya joto kwa vifaranga ingawa huwa inapendekezwa lakini sikushauri kwani kwani utafiti umeonyesha kuwa ufanisi wake katika kuleta joto ni mdogo sana hivyo hatari ya vifaranga kufa ni mkubwa sana. Labda kama zitatumika aina flani hivi za taa zinaitwa karabai sema tu huleta hasara kwenye upande wa matumizi ya mafuta.
 

Aman

Asante kwa majibu yako,

Hv kwa sehemu kama dar yenye joto kuna haja ya kuwapa vifaranga source nyingine ya joto kwa mchana?
 
Aman

Asante kwa majibu yako,

Hv kwa sehemu kama dar yenye joto kuna haja ya kuwapa vifaranga source nyingine ya joto kwa mchana?

emma250,
Kama joto litakuwa jingi hakutakuwa na haja ya kuwapa joto la ziada lakini ni muhimu kutazama mwenendo wa vifaranga hao, kama joto litakuwa la kutosha vifaranga watatawanyika chumba kizima bila kubanana, ukiona hali hii hunahaja ya kuwawekea joto la ziada lakini wakati wa asubuhi na usiku ni muhimu sana kuwawekea joto kutokana na hali ya baridi inayokuwepo wakati huo.
 

Shukran mkuu, nntakutafuta nikuwa na maswali mengine
 
Naombeni msaada wa dawa bora ya mafua ya kuku na macho kuvimba sana na kutoa vitu vyeupe...hii ni kwa kuku na bata mzinga.Asanteni
 


kuku wangu wanaanamia, wemanaharisha brown na nyekundu, nimeenda dukani nimeambiwa ni coccidiosis nikapewa ampolium, kuku wamekufa wengi sana wamekaribia 70 sasa, nimechanganuikiwa. dk mwingine akanitajia dawa nyingine, nimenunua kn kila asubuhi kwa siku tatu naokota kuku 24, 22. msaada tafadhali kuku ndio kwanza wana wiki saba.
 
Aman Ng'oma naomba mawasiliano yako simu, kuku wangu wamekufa karibu 100, kwa ugonjwa wa mapafu na ndui licha ya kua niliwachanja nashndwa kujua nlikosea wapi
 
Pole sana Englishlady,
Ndio maana nilisema toka awali kuwa kupata kile kitabu changu ni muhimu sana tatizo hizi lisinge tokea. Prevention ingefanyika toka mapema na kwamba kuku wangeendelea tu vizuri. Sasa ili kukusaidia vizuri ulitakiwa kutoa dalili zingine ambazo kuku wako wanaonyesha.Mfano kuku wagonjwa wanaonekanaje,mabawa yao yanakuwaje,wao wenyewe kwa ujumla wakoje?Pia ungeshituka mapema ungenipigia hata kabla hujakimbilia sehemu nyingine ungeokoa kuku wako.
Hebu sasa nipe haraka haraka hizo dalili zingine ili nikuambie tatizo na kisha nikupe ufumbuzi wa uhakika.
 
Aman Ng'oma naomba mawasiliano yako simu, kuku wangu wamekufa karibu 100, kwa ugonjwa wa mapafu na ndui licha ya kua niliwachanja nashndwa kujua nlikosea wapi

msungupendigwite;
Ugonjwa wa mapafu ya kuku!!,labda ni Infectious Coryza, hebu toa dalili zote ambazo wanaonyesha hao kuku wako ili nikuambie ni ugonjwa gani
 
Mkuu hongera sana kwa kazi ya kutuelimisha, nimekuwa nikikufuatilia toka mwanzo mpaka sasa. naomba msahada wako katika haya
1.Kitabu chako kwa Dodoma kinaweza patikana maduka yapi?
2. Naomba fomla ya kutengeneza chakula cha broiler kwani naexpirience ghalama ktk kununua chakula.
3.ningependa kujua kama kunashida yoyote kufuga broiler, layers na chotara katika eneo moja ila kwa mabanda tofauti?
natanguliza shukranI
 
Habari ya asubuhi Jamani.Samahani Nina Kuku wa kienyeji wakubwa baadhi wanataga Na wengine wameatamia. Sasa Leo ninaona katika kinyesi chao kuna mchanganyiko wa rangi nyeupe kama mtindi. Je, hili ni tatizo gani Na tiba yake ni nini?
 
Mimi nina banda la kuchukua kuku mianne(400) ningependa kupata maelekezo.nahitaji kufuga kuku wa nyama
ningependa ukanitumia contact zako tuwasiliane
 
Pia ninauza majogoo kwa bei nafuu 3500 tsh karibu,
Mimi nina banda la kuchukua kuku mianne(400) ningependa kupata maelekezo.nahitaji kufuga kuku wa nyama
ningependa ukanitumia contact zako tuwasiliane
 
Kwa wafuatiliaji wote wa uzi huu,
Wakati mwingine nakabiliwa na majukumu kidogo hivyo nakosa nafasi ya kuingia humu ndani,kwa wote wenye dharura tuwasiliane kwa mawasiliano yangu hapo chini ili kupata msaada zaidi
Aman Ng'oma,


A Livestock Based Project Consultant,

P.O BOX 1989,
Dodoma,
Tanzania.
Tel +255(0)767989713, +255(0)715989713,
+255(0)786989713
E-mail: amanngoma@gmail.com
 
Kwa wale wanaohitaji vifaranga vya kuku wa nyama (Broilers) inbox me
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…