emma250,
Asante kwa maswali yako mazuri. Kwakifupi ni kwamba, moshi unawaathiri vifaranga kama ambayo huwaathiri binaadamu
kitu cha msingi unapaswa kuhakikisha kuwa yale majiko yanakolezwa nje ya chumba cha vifaranga yakishakolea vyema yanayaingizwa ndani hivyo yanakuwa hayana tena moshi lakini pia ni muhimu kuhakikisha kuwa unapata mkaa mzuri maana mikaa mingine inakuwa na matatizo ya kutoa moshi.
Majiko 4 yanatosha kwa kuku hao 1000. Vilevile unapaswa uwe na vyumba viwili tofauti vya kuwalelea vifaranga hao kila chaumba kibebe vifaranga 500 na baada ya mwezi mmoja wawekwe kwenye vyumba 4 tofauti kila chumba kikibeba kuku 250. Nyumba itakayotosha kuku hao 1000 inatakiwa iwe yenye ukubwa wa 15m kwa 8m, kisha utaigawa katika vyumba vinne vilivyo sawa.
Ukifuga kwa kufuata kanuni na misingi ya ufugaji bora vifo vinakuwa ni 5%. Ingawa bado inalipa kibiashara hata vifo vikifika 10% ya kuku wote walioagizwa. Vifo zaidi ya asilimia kumi ni ishara ya kukosa umakini katika uleaji na utunzaji wa vifaranga na hivyo kupunguza faida. Kama utafuata ushauri kutoka kwa mtaam aliyesomea taaluma ya mifugo bila shaka utafanya vizuri katika ufugaji wako wa kuku na hata faida ufugaji itaonekana.
Katika uleaji wa vifaranga huwa tunatengeneza chumba maalum kwa ajili ya kulelea vifaranga hasa katika zile wiki tatu za mwanzo ambapo vifaranga wanahitaji joto kwa kiasi kikubwa ili kuwakinga dhidi ya baridi. Chumba hicho huitwa brooder. Brooder inaweza kutengenezwa kwa sealing board inayojikunja au chumba cha kawaida kinaweza kutumika kama brooder isipokuwa zile kona za chumba zitapaswa kuondolewe kwa kutengeneza vibao maalum ambavyo vitaondoa kona, ukiwasiliana na mafundi selemala watakusaidia.
Bei ya trai moja ya mayai kwa sasa ni tsh 7500 kwa jumla na tsh 9000 kwa bei ya rejareja, itategemea pia na mahali ulipo.
Asante.
Aman
Asante kwa kunipa mwanga,
Nimeambiwa taa ya chemli unaweza ikatumika kwenye brooder kama source ya joto, je ni Kweli?
Kama nikweli unashauri taa ngapi kwa vifaranga 1000?
Unaweza ukarecommend suppliers wazuri wa vifaranga wa mayai hapa dar?