Lugoba Investment
Senior Member
- Dec 5, 2013
- 180
- 188
Kaka though wengi wamechangia,nami pia nichangie kidogo.Mie nafuga for the past 8 months na nalima pia
1. Gharama kubwa ya ufugaji nguruwe ni chakula (about 80%) especially kama unafuga huku pwani. ni vema kama waweza kulima mahindi,matango,maboga,alizeti au hata mtama gharama zitashuka sana. Kwa sasa hv kama unanunua chakula kilichochanganywa (pumba pekee haitoshi,unahitaji madini,protein etc) ina average shs.600,000 per tonne.Nguruwe mmoja mkubwa anakula 2-3kg za hiyo complete ration. Ukichanganya mwenye (unahitaji formula) inaweza kuwa about tshs.400,000. Kama unalima hayo mazao hapo juu ni way cheaper.
Kwa hiyo nguruwe 20 watakula a minimum of 1200kg per month.upo kaka!!,Nguruwe 200 inakuwa=....
2.Band sio expensive sana lakini ukiwa nao wengi ni considerable cost! Banzi 1 wanauza 3000/-
3. Unahitaji kuwa na daktari wa wanyama karibu au ambae anaweza kutembelea regularly. Ukipata uzoefu haitakuwa mara kwa mara only unapokuwa na case za ugonjwa
4. Kwa mtu ambaye unaanza project hii naungana na ushauri wa kuanza na wa 5. Itakupa opportunity ya kupata uzoefu uzoefu ukiwa na wachache na waweza kuwamudu kirahisi unless kama utaajiri mtaalamu. Ukipata mbegu ambayo ni prolific hao watupa watoto wasipopungua 35! Ukiona mambo yanaenda vizuri baada ya miezi 6 waweza kuongeza wengine. Hiyo ya kuanza na wengi ni kama una mtaalamu au ww upo fulltime.
Pia nashauri kuanza na nguruwe wenye mimba za kwanza au pili. Tembelea wafugaji,chagua mbegu nzuri, then mwambie akupandishie. Wachukue nguruwe wakiwa na mimba za miezi 2 na dume mmoja wa miezi 8-12. Nguruwe huzaa baada ya miezi3 week3 siku 3. Unawanyonyesha piglets kwa 6-8 weeks halafu unawaachisha. Nguruwe huhitaji dume siku 5 baada ya kuachisha watoto kama alikuwa analishwa vizuri. Baada ya mwaka mmoja utakuwa na nguruwe zaidi ya 80. Karibu kaka.
Ebwana asante sana kwa kuendelea kuchangia uzi huu kwa kutupa knowledge za uhakika,mwalimu mmoja wa advance maujanja kama haya alikuwa akiita NONDO..Kwenye idadi nimepunguza naanza na 10