Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji


Ebwana asante sana kwa kuendelea kuchangia uzi huu kwa kutupa knowledge za uhakika,mwalimu mmoja wa advance maujanja kama haya alikuwa akiita NONDO..Kwenye idadi nimepunguza naanza na 10
 
Nguruwe wanalipa, lakini uchanganye na maombi isije ikakupitia hii kitu wanaitwa swine feaver! Uliza watu wa rombo na moshi vijijini watakueleza vizuri. Mimi imenicost vibaya mwezi uliopita. Katika batch ambayo nilitarajia kupata walau milioni tano, nimeishia kuambualia milioni moja. Majirani zangu ndo usiseme. Kuna dingi kapoteza nguruwe 180, kila mmoja mwenye wastani wa bei ya sh 300,000,. Mbaya zaidi, hakuna tiba wala chanjo.
 
Hapo kwenye hilo shimo hapalowi au kuweka unyevu unyevu?

inapotokea unyevu umekuwa mwingi unatakiwa kuongeza either pumba za mpunga or randa za mbao , nakama ni kipindi cha kiangazi waweza weka majani makavu. hii inakuwa ndiyo kama kuosha banda, hivyo vyote vinapatikana bure katika mashine za kukoboa mpunga au kuranda mbao. chakuongeza ni kuwa chakula unachowapa kisiwe ndani ya maji mengi sana , kiwe cha unyevu au kikavu na maji pembeni , kwani kikiwa ndani ya maji hupelekea nguruwe kunywa maji mengi saaana na kisha kukojoa saana kiasi cha kulowesha zaidi chamba chake.
 
wasiwasi kidogo nilionao ni jinsi ya kulea piglet , kwani natarajia watazaliwa wengi kwa kipindi kimoja kifupi yaani february, na hasa ukizingatia upya wangu ktk fanii hii kidogo inanitia wasiwasi . ninachijiandaa kwa sasa ni chakula cha kutosha tu, hivyo ombi langu hapa JF kama kuna mwana JF mwenye uzoefu huo naomba anishauri nn chakufanya. maana matarajio ni nguruwe 15 kuzaa kipindi hicho na kama kila mmoja akizaa 6 hao ni 80 na kama ni 8 basi ni 120 hivyo nadhani utaiona changamoto nitakayokuwa nayo. mpango wangu ni kuwakuza wote , je mnanishaurije?
 
Aisee poleni sana..Hv huu ugonjwa kweli hauna hata chanjo?
 
Hongera sana mkuu.... watakuja tu wataalamu wa humu JF kukupa ushauri.... nimependa sana style ya ufugaji wako
 
Hongera sana fuchi kwa kuthubutu.ushauri wangu juu ya kulea hao watoto ni kwamba nenda katafute kijana mwingine wa ziada ambaye tayari ana uzoefu huo,unaweza kumpata kirahisi kupitia wafugaji hao hao waliokupa ushauri nwanzoni.

Kipindi hiki usiogope kutumia hela,tafuta huyo kijana kwa gharama yoyote hata kama ni kwa part time.
 
Hongera Fuchi
Umefika pazuri.
Kwa design hiyo ya ufugaji,ni lazima sana kuwepo mtu wakati wa kuzaa na siku zinazofuata baada ya hapo.Ni rahisi watoto kulaliwa na mama yao kwa sababu wkwa sababu ya mapumba.
Nashauri kuwa sehemu ya kuwaweka na wanyonye kwa uangqlizi mpaka watakapo pata nguvu za kutembea vizuri.
Wakatwe vitovu to about 5 cm mara wanapozaliwa na vichovye kwenye iodine.mazingira yako ni safi kwani watapata joto la kutosha
Wachome iron siku ya 2-3 na siku ya 21.mam alishwe chakula cha kutosha na watoto wakifikia week3 waanze kupata creep feed(chakula cha watoto).
Ukifanya hivyo watakuwa vizuri na kuacha kunyosha wakiwa wanakula vizuri.wakiachishwa wachomwe dawa ya minyoo
 


yah, naona hili ni wazo zuri linaweza kuwa ni suluhisho la wasiwasi wangu, nitafanya hivyo mkuu lakini pia nitaendelea fanya mawasiliano humu JF ili kama nitapata ugumu fulani tushauriane.
 

asante mkuu kwa ushauri nitazingatia yote, hasa hili la kukata vitovu nilikuwa sijaliwazia kabisa , nilidhani nao wanazaa kama ng'ombe au mbuzi bila usimamizi wa karibu saaana , kumbe mpaka kitovu wakatwe! hapo kweli nahitaji mtu mwingine mwenye uzoefu huo. asante
 
Gmosha,
Kwa yaliyokukuta.upo sahihi kuhusu maombi ,infact msaada wa Mungu unahitajika kwa kila jambo.usikatishwe tamaa,la msingi jifunze kwenye hilo then move forward.Hakuna business isiYo la risk.kila sehemu watu hufungua maduka na kufunga kwa sababu ya hasara lakini wapo wanaofanikiwa.kila business inakupa opportunity ya kupata hasara au faida!
JIM Rohn anasema😀o not wish for less problems,wish for more skills!
 


Ni kweli mkuu. Bado sijakata tamaa. Kwa bahati nzuri banda langu hawakufa wote. Wamepona kama kumi na mbili na wengine wana mimba. Natarajia hawa wataniwezesha kusonga mbele. Ni shughuli ambayo nimeifanya kwa miaka mitano sasa. Inalipa kama mambo yakienda shwari.
 
Nafurahi kusikia hivyo.so unafugia moshi kaka?tupo pamoja
 
Mr.Fuchi,
Tupo pamoja.either uajiri au upate mtu amuelekeze kijana wako.isio ngumu hiyo hata ww kama upo around waweza fanya.
Mi nipo interested kuona hiyo deep litter system ya mabanda yako.niliku pm naona hujapata muda wa kuona.
Nadhani ulisema unafugia mkambarani au sio?mi nafugia Maseyu mwendo kidogo kutoka mikese kama unakuja dar.
Nataka ku expand mabanda na nataka kujaribu hii deep litter system.
Mi nimeweka sakafu,jinsi mabanda yanavyo ongezeka usafi inakuwa labour intensive!nita appreciate kuona ww ulivyofanya

"No dream is too big but action brings dreams to reality"
 
Ebu pitia na post hii https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/42162-anza-hivi-mpwa-wangu.html. Naamini itakubust.
 

Nimependa ulivorespond...na kama umeeza react hiv kwa huyu basi hii ni dalili ya mafanikio na kua na busara!!! Keep on moving mkuu!!
 
Haya wajasiriamali na wafugaji NGURUWE document hii naamini ina msaada mkubwa sana na mzuri kwa wafugaji wanaoendelea na beginners like me.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…