Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
thanks sana kwa post yakoHaya wajasiriamali na wafugaji NGURUWE document hii naamini ina msaada mkubwa sana na mzuri kwa wafugaji wanaoendelea na beginners like me.
Wapendwa katika kuhangaika mtandaoni nimepata kitabu hiki,naamini kitakuwa cha msaada mkubwa sana..
m2pe updates kwa waliojaribu inalipa kweli?
Mkuu siyo kila kitu mpaka waje watu washuhidie wee ndo uelewe. Kama unataka ingia nawe acha uvivu huo. Mbona mnachosha?
mpwa nashukuru sana kwa wazo zuri sana la biashara! wacha nikuze mtaji kwanza kwa kuanza na kilimo hapo itakapotimia mwaka 2015...Nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000
Banda la mabanzi=1,000,000
Chakula = 1,000,000
Dawa= 200000
After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,
utachakuwa vitoto jike 100,
mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000
After 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700
Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike)
Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500
1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka
Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
Welcome to the club
Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu.
Kila mwaka nalima Mahindi, alizeti, maboga ekari 30 kwa ajili ya chakula cha
Nguruwe tu.
nakupenda saana mpwa,
Natambua watu wengi ambao imani zao zinaruhusu wanatamanikufanya mradi wa ufugaji nguruwe wenye faida.Labda wengine wamejaribu bilamafanikio.Kwa uzoefu wangu ( refer thread yangu:Ufugaji na kilimo unalipa sana)hivi ndivyo waweza fanya kupata mfanikio.
1. Kwanza tambua hii ni agri-business,basi kama business nyingine inahitaiiusmamizi wa kutosha. Watu hudhani ukianzisha mradi na kuweka kijana wa kuwalisha basiunangojea faida tu. Ni vema ukaelewa mahitaji ya hao wanyama vema(chakula,usafi,malazi,tiba na jinsi ya kuzuia magonjwa) na wewe sasa ndiomwalimu wa herdman wako
2.Tambua faida inatokana na aina bora ya mbegu na malezi. Nia ni kuwaleawanyama wakue kufikia uzito wa soko wa muda mfupi.Kwa kawaida nguruwe huuzwakwa nyama akiwa na uzito kuanzia 50kg. Shambani kwangu huuzwa kuanzia miezi 5.
3. Waangalizi(herdmen) ni watu muhimu sana kwako.Ni lazima wafundishwe vizuri namaslahi yao yaangaliwe kwa makini.
4. Nguruwe akiugua atibiwe mara moja. Nguruwe ni mnyamaambae haugui kirahisi akilelewa vema unless kama kuna outbreak. Mara mojamojahuugua inabidi herdman awe na uwezo wa kugundua mapema na mnyama apewe tibamara moja. Ukiwalea vizuri muda mwingi wanahitaji chanjo tu za minyoo naukurutu
5. Nguruwe walishwe ration(balanced feed) sio pumba tu aumasalia ya jikoni. Tambua mahitaji ya chakula yanguruwe(protein,wanga,mafuta,madini,vitamin) na hakikisha mchanganyiko unaofaakwa umri wa nguruwe.Shambani kwangu chakula kikuu ni mahindi/mtama,pumba zamahindi na mpunga,mashudu ya alizeti, ambayo tunalima hapo shamba.Piahuchanganya madini (nguruwe mix) na mifupa/chokaa
6. Tambua gharama kubwa ya ufugaji ipo kwenye chakula (atleast 70%). Kwa wastani nguruwe mkubwa anahitaji 2kg/siku. Kwa hiyo kumleanguruwe mmoja hadi miezi 6 anahitaji 240kg(miezi 2 ya kwanza huwa ananyonya)
(a) ukininunuachakula ambacho tayari kimechanganywa gharama ni kama tshs 600/kg
(b) ukinunuavyakula na kuchanya mwenyewe gharama ni kama tshs.400/kg
(c) Ukilimavyakula na kuchanganya mwenyewe gharama ni kama tshs 150-250/kg
Utaona kama waweza kulima mazao kwa ajili ya mifugo wakogharama inapungua sana
7. Faida yako ipokwenye kuuza nguruwe wa nyama. Wanunuzi wa mbegu sio wengi na sio consistent. Kwa hiyo itakuchukua a minimum ya miezi 6kuanza kupata faida kutoka kwenye mradi wako.Huu ndio ukweli. Lengo ni kuuzaidadi fulani ya nguruwe Kila mwezi. Kwa mfano ingalau nguruwe 20 kila mwezi.Unadhaniunahitaji nguruwe wangapi kwa wakati mmoja kufanikisha hilo???
8. Soko la nguruwe ni kubwa na linazidi kukua. Walaji wengiwapo Dar es salaam. Waweza kuuza live hapo shambani au ukapeleka mwenyewemachinjioni inategemeana na soko lipo mbali kiasi gani. Nguruwe wa miezi 6 anawezakukuingizia tshs.200,000-300,000 kutegemea na namna ulivyouza na uzito
9.Unaanzaje kufuga kibiashara????
(a) Faida ndani ya miezi 6,na kuuza nguruwe 20kila mwezi
Nunua nguruwe jike wenye mimba uzaowa 2 ; wa2 mimba miezi 3;wa2 miezi 2 na wa2 mimba mwezi1,wa2 ambao ndiowamepandwa na wa2 wenye umri wa miezi 6. Nunua kwa mfugaji mwenye mbeguinayoanza kuzaa mapema. Ukinunua wa uzao wa kwanza namba inakuwa nguruwe 3badala ya Pia dume mzuri mwenye umri wamiezi 8au zaidi. Kwa namna hii kila mwezi nguruwe wa2(au 3) watazaa watotosio chini ya 20. Utaanza kuuza mbegu ndani ya miezi 2.Na baada ya miezi 6utauza nguruwe sio chini ya 20 kila mwezi kwa nyama!
Nguruwe jike mwenye mimba waweza kumpata kwatshs350,000-400,000
Mauzo 4-6m kila mwezi. Neti profit itategemeana na gharamaza chakula kama nilivyo ainisha awali.
Shambani kwangu tunawaachisha watoto kunyonya wakiwa na week6 na jike hupata joto na kupandwa tena ndani ya siku 3-7. Hivyo nguruwe wetuhuzaa mara 2.5 kwa mwaka.
Watoto huwauza wakiwa na miezi 2 kwa 45,000-60,000 kutegemeana uzito
(b) Kama utaanzakufuga nguruwe watoto wenye miezi 2?!
Ina maana utaanza kuuza baada ya mieziisiyopungua 10. Pia utahitaji kuwafanya nguruwe wako wapate mimba kwa groupsambayo inahitaji uzoefu wako na herdman. Utahitaji pia dume lenye umri wamiezi12 au zaidi. Pia kwa mtu anaeanza ufugaji inasumbua kidogo. Lakini ninafuu kidogo interms of upfront capital though gharama za ufugaji zinaWEZAkubwa.
Shambani kwangu kwa sasa nguruwe wa 2 au 3 wanazaa kwamwezi. Kuanzia November nguruwe 5-7watazaa kwa mwezi.
Hope hii itawasaidia watakaopenda kujaribu hii project
Mungu akubariki mkuu.
Ruhusa ya Paulo.Natambua watu wengi ambao imani zao zinaruhusu wanatamanikufanya mradi wa ufugaji nguruwe wenye faida.Labda