Ufugaji wenye tija huanza kwa kuchagua mbegu(breed) ya ngururuwe nzuri nashauri utafute large white au landrace(wenye masikio yaliyo lala) weupe ni vizuri kuchagua jike mwenye chuchu zisizo pungua 12,hii ni dalili ya kwanza ya mzao bora.
Ni vizuri kuwalisha nguruwe chakula chenye mchanganyiko wenye virutubisho vyote,mara nyingi vyakula tunavyolisha vinakuwa havina mchanganyiko wa virutubisho vyote hivyo wape madini na vitamin maalum za viwandani kama nguruwe/pig mix,pigboost,vikuzi(growth promoters)-kwa nguruwe wadogo kwa ajiri kumnenepesha na kuimalisha mifupa yake.Wakiwa wadogo kwa umri wa siku 3-5 wapigwe sindano ya kuzuia upungufu wa damu(irondextran),watakavyo kuwa wakubwa wapewe dawa za vitamin na minyoo kila baada ya miezi mitatu,pamoja na mambo mengine waliyosema wadau,banda ninashuri la mabanzi ambayo yanapatikana kwa wingi mikoa ya kusini kwa bei ndogo sana labda chini ya 200,inategemea na eneo ulipo.