Habari wanaJF
,
Tafadhali kwa wale wasiopenda jina hilo hapo juu samahani sana.
Mimi nimefuga nguruwe, nilianza nikiwa niko chuo kikuu mwaka wa pili pale UDSM kwa mtaji wa shilingi 500,000/=
Nilianza kujenga zizi kwa shilingi laki tatu tu na nikanunua makinda ya nguruwe mawili jike na dume kila mmoja sh. @40,000 (mradi niliufungua nyumbani mkoani Kigoma). Fedha zilizobakia nilitafuta mfanyakazi wa kuwalisha hao nguruwe. Nilimlipa sh. 40000 kwa mwezi. Kati ya laki 5, zilibaki 80,000 ambazo nilianza kwa kunulia chakula cha nguruwe.
Baada ya hapo nguruwe niliwapandisha wakazaa watoto 10. Kati ya hao madume yalikuwa 4 na jike 6. Baada ya hayo makinda kukua sikuuza makinda ya jike. niliamua kupanua mradi hivyo nilipanua zizi! Hapo ilikuwa baada ya miezi tisa tu.
Baada ya kupanua mradi niliuza madume 3 nikanunua vyakula (maharage yaliyooza na mashudu) ya kulishia nguruwe waliobakia.
Baada ya miezi 18 nguruwe waliongezeka baada ya kuzaa tena (yale majike 6 na dume 1). Nikaendelea kupanua zizi maana nilijikuta nina nguruwe 30. Kumbuka nguruwe sita wote walizaa. Mmoja makinda 6, mwingine 5, mwingine 5 mwingine 4 mwingine 7 na mwingine 2, na lile dume 1. Jumla nguruwe 30.
Nazidi kupanua mradi na chuo nimeshamaliza kwa sasa nasimamia mwenyewe!
Hakika kwa sasa mimi ni tajiri!
Amini usiamini mimi sio masikini tena!
siku njema.