Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Nimejifunza sana....asanteni sana wachangiaji na wataochangia
kwa namna ya kujenga mawazo chanya.
 
Umefikia wapi?

Mtwa Mkulu naona leo unataka feedback tu.
Ni vzr kupata mrejesho nyuma ili tuweze kujifunza zaid ila sidhan kama kweli tupo serious na sidhan kama wengi watu humu ndani tunafanya biashara, kama nnayosema sio kweli kwann watu hawalete maendeleo ya biashara zao ili hali wameomba ideas humu Jf?
Sitegemei kama utapata jib nilishawahi kuuliza sikufanikiwa lkn sio sbb ya kukaa kimya tuendelee kuomba feedback
 
Huko kwenu ambapo kitoto cha nguruwe huuzwa sh 20,000 ni wapi? Ninampango wa kuanza ufugaji wa nguruwe shambani kwangu.
 
Huko kwenu ambapo kitoto cha nguruwe huuzwa sh 20,000 ni wapi? Ninampango wa kuanza ufugaji wa nguruwe shambani kwangu.

Mi nimeshangaa pia ila huu uzi ni wa 2009 ilikuwa ni sawa sasa hivi kitoto cha nguruwe ni 50000
 
Mpwa hii bonge ya deal hata mate yananitoka ila tatizo mimi imani yangu inaniambia nguruwe ni haramu kabisa. lakini hiyo hela naitaka tena sana tu.

Kula ni haramu,kufuga si haramu
 
Hii biashara huwa naitamani sana, mchanganuo upo vizuri ahsante
 
Naitamani sana hii biashara sema niko KILWA na huku kuna jamaa alijaribu kufuga akafa mara moja cjui walimsomea mambo flani?kiukwel natamani saaanaaaa saanaaa ila udini sasa
 
We ni Wakala wa sera ya JK ya Kilimo kwanza eeh?

Mbona hujaweka effect ya SWINE- FLU, ambayo inaweza kuwamaliza nguruwe wote kwa wiki 1?

Hiyo ni Risk tu!,km zilivyo risk nyingine na ukisema ufuate hivyo,kamwe huwezi kufanya lolote,maana hakuna mradi usiokuwa na risk au Uncertainty.
 
duuuh biashara nzuri hii nimejifunza kitu simamia mwenyewe tunaopenda dar duuh
 
Mambo yangu hayo
 

Attachments

  • 1448275318022.jpg
    1448275318022.jpg
    57.5 KB · Views: 235
Swine flu sio tatizo tropic countries tatizo ni pneumonia choma iron injection after three day then usafi
 
Habari wanaJF
,
Tafadhali kwa wale wasiopenda jina hilo hapo juu samahani sana.

Mimi nimefuga nguruwe, nilianza nikiwa niko chuo kikuu mwaka wa pili pale UDSM kwa mtaji wa shilingi 500,000/=

Nilianza kujenga zizi kwa shilingi laki tatu tu na nikanunua makinda ya nguruwe mawili jike na dume kila mmoja sh. @40,000 (mradi niliufungua nyumbani mkoani Kigoma). Fedha zilizobakia nilitafuta mfanyakazi wa kuwalisha hao nguruwe. Nilimlipa sh. 40000 kwa mwezi. Kati ya laki 5, zilibaki 80,000 ambazo nilianza kwa kunulia chakula cha nguruwe.

Baada ya hapo nguruwe niliwapandisha wakazaa watoto 10. Kati ya hao madume yalikuwa 4 na jike 6. Baada ya hayo makinda kukua sikuuza makinda ya jike. niliamua kupanua mradi hivyo nilipanua zizi! Hapo ilikuwa baada ya miezi tisa tu.

Baada ya kupanua mradi niliuza madume 3 nikanunua vyakula (maharage yaliyooza na mashudu) ya kulishia nguruwe waliobakia.

Baada ya miezi 18 nguruwe waliongezeka baada ya kuzaa tena (yale majike 6 na dume 1). Nikaendelea kupanua zizi maana nilijikuta nina nguruwe 30. Kumbuka nguruwe sita wote walizaa. Mmoja makinda 6, mwingine 5, mwingine 5 mwingine 4 mwingine 7 na mwingine 2, na lile dume 1. Jumla nguruwe 30.

Nazidi kupanua mradi na chuo nimeshamaliza kwa sasa nasimamia mwenyewe!

Hakika kwa sasa mimi ni tajiri!

Amini usiamini mimi sio masikini tena!

siku njema.
 
mtaji ilikuwa boom. hela tunayopewa chuoni. niliikusanya kwa mda wa mwaka mmoja tu.!
 
Back
Top Bottom