Fisadikuu;
Usikuwe Tomaso wa kila kitu mkuu. Mimi nimewahi kufuga nguruwe. Tena Landres, dume likakaa nami miaka 2 tu. Nikamchinja, akatoa kilo 240. Sikujui hunijui, sina haja ya kukudanganya
Mkuu,
Pamoja na kebehi zao, nakuunga mkono kuwa weye unajua unalo litenda. Nakuhakikishia kuwa, mimi ni mfugaji wa hicho kitu. Nina zaidi ya miaka 20 hakuna hata siku moja nimekosa kuwa na nguruwe 10m kwa banda langu.
Kifupi tu ni kwamba, nimejenga house, nimenunulia "magari", nimesomeshea watoto 3 wakafika chuo kikuu. Kama kuna mtu anayedharau mradi huo, atembee aone.
Nimewahi kufuga mpaka nguruwe 300 kwa mara moja
mkuu mangatara
hili ni jukwaa ambalo ni watu wengi hupata manufaa ..... Landres wengi hufikia 130-150kg kwa uzoefu wangu Wa hapa Tanzania tena wafugaji Wa Dar na pwani ..... kiuhalisia 200-250kg Caracas swine haileti ukweli .... hiyo nguruwe hata kusimama itakuwa ngumu
mkuu ningependa unipe uzoefu wako wanafika kilo 100, baada ya siku ngapi kwa mbegu nzuri ya kibiashara.
changamoto ya chakula chao ikoje kwa upatikanaji.
nimeona mara nyingi wakilishwa mabaki ya mimea je mimea inaweza kuwa chakula chao kikuu?
Mkuu,
Pamoja na kebehi zao, nakuunga mkono kuwa weye unajua unalo litenda. Nakuhakikishia kuwa, mimi ni mfugaji wa hicho kitu. Nina zaidi ya miaka 20 hakuna hata siku moja nimekosa kuwa na nguruwe 10m kwa banda langu.
Kifupi tu ni kwamba, nimejenga house, nimenunulia "magari", nimesomeshea watoto 3 wakafika chuo kikuu. Kama kuna mtu anayedharau mradi huo, atembee aone.
Nimewahi kufuga mpaka nguruwe 300 kwa mara moja
aha aha sasa ndani ya mwezi si hutakuwa huna hata nguruwe mmoja,acha uroho subiri wafike japo 200,tena location tofauti.utakumbuka maneno yangu siku ukikuta waha wenzako wameiba nguruwe wote hapo nyumbani
duuu kumbe bora kuandika uongo humu jf kuliko ukweli. mimi ndo nimefuga na ni nguruwe wangu sasa unakataa nini? bored.
nashukuru mkuu bluetooth kwa maelekezo murua ya kina pia.
naona unawapa chakula bora sana, nikupongeze kwa hilo. ningependa kuweka maswali ya nyongeza mawili; mpaka kufikia kilo wastani 80 anakuwa amekula kilo ngapi na thamani ya chakula chao ni kiasi gani kwa kilo.
natanguliza shukrani kwa muda wako.
Mkuu pleo ..... Kuna kitu kinaitwa FCR (Feed Convertion Ratio) katika ufugaji ..... hii inakokotoa ratio za chakula na bei katika muda fulani ..... naomba u-google hili somo utapata majibu haina tofauti na actual feeding practice
nashukuru kwa mwongozo nimepata 3 kwa mbegu, mazingira na chakula bora,
Ni sawa ila nguruwe mmoja kutoa kilo 200-250 ni uongo
Wandugu msibishe vitu msivyovijua, Mimi pia ni mfugaji wa pig, nilinunua mbegu toka Misheni Fulani huku kwetu, wanauzwa kwa kilo nguruwe Mzima anapimwa. Mwenye mimba 4500@ kg na asiye na mimba ni 4000@ kg.
Mimi nilimnunua mwenye mimba alikuwa na kilo 198, kwa 891,000/= na madume wao hapo wanafika kilo 200 hadi 250, ni wale wenye masikio yalolala kwa mbele, kitaalamu sijui wanaitwaje.
Nguruwe wa kilo 200? Nguruwe bora ni wale wa kilo 70-80 zaidi ya hapo mhhh. Anza huo mradi unalipa sana.
means kila siku unauza kilo 200-250 haibakii hata kilo moja????
nahisi huna hata nguruwe mmoja, ila una mpango mkakati wa kufuga hao nguruwe, kingine may be unajiliwaza kuwa zimebakia siku chache mwaka kuisha na nguruwe hujafuga na chuo umemaliza. ushauri wangu waache wazaliane
mimi siuzi kinda hata moja nimefungua baa yangu nauza nyama choma ya ngurue kilo sh. 10000. na vinywaji. na ngurue wangu ni wakubwa mno wanaweza kutoa hadi kilo 200 mpaka 250.
Nguruwe wa kilo 200? Nguruwe bora ni wale wa kilo 70-80 zaidi ya hapo mhhh. Anza huo mradi unalipa sana.
mtaji ilikuwa boom. hela tunayopewa chuoni. niliikusanya kwa mda wa mwaka mmoja tu.!