Wakuu,
Mimi ninaishi Dar, nina eneo langu kama eka 20 hivi huko Mkuranga. Sasa nimedhamiria mwaka huu kuanza kufuga nguruwe, naombeni mnishauri baadhi ya mambo hapa.
1. Nina taka kujenga vyumba viwili, kimoja kwaajili ya kijana wangu wa kufanya hizo shughuli na kingine kwaajili yangu kwakuwa kila Ijumaa nitakuwa nina kwenda shamba na kurudi Dar Jumapili. Hivyo naomba kufahamu gharama za kujenga vyumba viwili kwa Mkuranga (roughly) kuanzia mwanzo mpaka iwe inafaa mtu kuishi itakuwa ni kiasi gani cha fedha? na ujenzi wa choo je itakuwa ni sh ngapi?
2. Nahitaji kujenga mabanda ishirini ya mabanzi kwa kuanzia yenye ukubwa wa mita nne kwa mita sita, je banda moja la ukubwa huo hutumia kiasi gani cha mabanzi? banzi moja jijini dar linauzwa sh ngapi? mabanda hayo nitayawekea zege, je chumba cha ukubwa wa mita nne kwa sita nitatumia sh ngapi kumwaga zege?
3. Je, gharama za kuchimba kisima cha maji ni sh ngapi? na mashine ya kuvutia maji kupeleka kwenye tank itakuwa ni sh ngapi (nataka yaka kwenye tank kwakuwa nitakuwa nikitumia auto drinker)
Ikifika 2018/19 nataka niwe na nguruwe zaidi ya mia tano, soko la nguruwe ni kubwa sana wakuu.
Karibuni kwa mawazo yenu