Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Fisadikuu;
Usikuwe Tomaso wa kila kitu mkuu. Mimi nimewahi kufuga nguruwe. Tena Landres, dume likakaa nami miaka 2 tu. Nikamchinja, akatoa kilo 240. Sikujui hunijui, sina haja ya kukudanganya

mkuu mangatara

hili ni jukwaa ambalo ni watu wengi hupata manufaa ..... Landres wengi hufikia 130-150kg kwa uzoefu wangu Wa hapa Tanzania tena wafugaji Wa Dar na pwani ..... kiuhalisia 200-250kg Caracas swine haileti ukweli .... hiyo nguruwe hata kusimama itakuwa ngumu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,
Pamoja na kebehi zao, nakuunga mkono kuwa weye unajua unalo litenda. Nakuhakikishia kuwa, mimi ni mfugaji wa hicho kitu. Nina zaidi ya miaka 20 hakuna hata siku moja nimekosa kuwa na nguruwe 10m kwa banda langu.
Kifupi tu ni kwamba, nimejenga house, nimenunulia "magari", nimesomeshea watoto 3 wakafika chuo kikuu. Kama kuna mtu anayedharau mradi huo, atembee aone.
Nimewahi kufuga mpaka nguruwe 300 kwa mara moja

heshima kwako mkuu.
 
mkuu ningependa unipe uzoefu wako wanafika kilo 100, baada ya siku ngapi kwa mbegu nzuri ya kibiashara.
changamoto ya chakula chao ikoje kwa upatikanaji.
nimeona mara nyingi wakilishwa mabaki ya mimea je mimea inaweza kuwa chakula chao kikuu?
 
Mkuu pleo .... breed nzuri ya nguruwe ni large white au land race .... ufugaji mzuri usio na usumbufu ni kutumia chakula kwa kuchanganya Pumba za mahindi, Pollard, mashudu ya alizeti (sunflower cake), soya meal, Sodium (chumvi) .... mifupa (calcium) na premix aina ya pig mix .... nguruwe hulishwa kwa ration either asubuhi au jioni ... maji ya kunywa ni muhimu wakati wote .... banda la nguruwe linahitaji usafi na ili kuzuia bacteria, nzi na harufu inafaa kutumia chokaa au majivu kunyunyizia floor ya banda baada ya usafi kila siku ..... Nguruwe huchomwa sindano za kinga ya micro-bacteria kama sulphudimadine na pia minyoo ya nje na ndani hii unachoma subcoteous .... pia watoto wa nguruwe wanapozaliwa ni vizuri kuwaongezea joto bandani kwa kuwawashia mkaa au taa ya joto (brooding) .... baada ya siku tatu piglets huchomwa sindano ya madini aina ya iron na kuwaachisha kunyonya maziwa wakiwa na umri wa mwezi mmoja na nusu na hapo ndipo unaweza kuhasi madume kwa ajili ya ukuaji mzuri na kunenepesha

uzito mzuri wa nguruwe kwa ajili ya nyama ni 60-90kg ..,. katika umri wa 5months

Angalizo .....Ufugaji wa nguruwe kuna tatizo kubwa la in- breeding ..... nguruwe ndugu wasiruhusiwe kuzaana wenyewe kwa wenyewe ... hii husababisha tatizo la vilema, vifo na udhaifu wa afya kwa mzao

ukiweza kupata majani mateke teke, migomba ya ndizi, mashina na majani ya mihogo inaweza kuongeza afya na virutubisho kwa nguruwe pia kuboresha mfumo wa digestion na kusave chakula cha dukani
 
Last edited by a moderator:
nashukuru mkuu bluetooth kwa maelekezo murua ya kina pia.
naona unawapa chakula bora sana, nikupongeze kwa hilo. ningependa kuweka maswali ya nyongeza mawili; mpaka kufikia kilo wastani 80 anakuwa amekula kilo ngapi na thamani ya chakula chao ni kiasi gani kwa kilo.

natanguliza shukrani kwa muda wako.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,
Pamoja na kebehi zao, nakuunga mkono kuwa weye unajua unalo litenda. Nakuhakikishia kuwa, mimi ni mfugaji wa hicho kitu. Nina zaidi ya miaka 20 hakuna hata siku moja nimekosa kuwa na nguruwe 10m kwa banda langu.
Kifupi tu ni kwamba, nimejenga house, nimenunulia "magari", nimesomeshea watoto 3 wakafika chuo kikuu. Kama kuna mtu anayedharau mradi huo, atembee aone.
Nimewahi kufuga mpaka nguruwe 300 kwa mara moja

nicheki mkuu"
0653918931
 
aha aha sasa ndani ya mwezi si hutakuwa huna hata nguruwe mmoja,acha uroho subiri wafike japo 200,tena location tofauti.utakumbuka maneno yangu siku ukikuta waha wenzako wameiba nguruwe wote hapo nyumbani

hahahaaaa acha roho mbaya haibi mtu hapa
 
nashukuru mkuu bluetooth kwa maelekezo murua ya kina pia.
naona unawapa chakula bora sana, nikupongeze kwa hilo. ningependa kuweka maswali ya nyongeza mawili; mpaka kufikia kilo wastani 80 anakuwa amekula kilo ngapi na thamani ya chakula chao ni kiasi gani kwa kilo.

natanguliza shukrani kwa muda wako.

Mkuu pleo ..... Kuna kitu kinaitwa FCR (Feed Convertion Ratio) katika ufugaji ..... hii inakokotoa ratio za chakula na bei katika muda fulani ..... naomba u-google hili somo utapata majibu haina tofauti na actual feeding practice
 
Last edited by a moderator:
Mkuu pleo ..... Kuna kitu kinaitwa FCR (Feed Convertion Ratio) katika ufugaji ..... hii inakokotoa ratio za chakula na bei katika muda fulani ..... naomba u-google hili somo utapata majibu haina tofauti na actual feeding practice

nashukuru kwa mwongozo nimepata 3 kwa mbegu, mazingira na chakula bora,
 
Last edited by a moderator:
yalimo

Means kila siku unauza kilo 200-250 haibakii hata kilo moja? Nahisi huna hata nguruwe mmoja, ila una mpango mkakati wa kufuga hao nguruwe, kingine may be unajiliwaza kuwa zimebakia siku chache mwaka kuisha na nguruwe hujafuga na chuo umemaliza.

Ushauri wangu waache wazaliane..
 
Last edited by a moderator:
Ni sawa ila nguruwe mmoja kutoa kilo 200-250 ni uongo

Wandugu msibishe vitu msivyovijua, Mimi pia ni mfugaji wa pig, nilinunua mbegu toka Misheni Fulani huku kwetu, wanauzwa kwa kilo nguruwe Mzima anapimwa. Mwenye mimba 4500@ kg na asiye na mimba ni 4000@ kg.

Mimi nilimnunua mwenye mimba alikuwa na kilo 198, kwa 891,000/= na madume wao hapo wanafika kilo 200 hadi 250, ni wale wenye masikio yalolala kwa mbele, kitaalamu sijui wanaitwaje.
 
mkuu Ramea..... twende taratibu ..... kinachozungumziwa hapa ni mavuno ambayo ni nyama kwa ajili ya kuuza in Kg ..... unaweza kuita Caracas kwa lugha ya kizungu ..... uzito Wa Caracas (nyama)huwa ni 75% ya uzito wa live animal ..... hebu Fanya hesabu vizuri
 
Last edited by a moderator:
means kila siku unauza kilo 200-250 haibakii hata kilo moja????
nahisi huna hata nguruwe mmoja, ila una mpango mkakati wa kufuga hao nguruwe, kingine may be unajiliwaza kuwa zimebakia siku chache mwaka kuisha na nguruwe hujafuga na chuo umemaliza. ushauri wangu waache wazaliane

Mkuu Luis, labda atufundishe amewalisha nini mpaka wakafikia kilo hizo over 200 kg wote anaowachinja kila siku. kwa kweli mimi mwenyewe nimeshaandaa business plan ya kufuga nguruwe na ni kitu napenda sana ila bado natafuta funding na nazidi kutafuta elimu (kuna mtu mmoja alisema ''ukipewa masaa 6 kukata mti tumia masaa 4 kunoa shoka''). naomba kama kuna mwenye kitabu softcopyy aiweke.. Mr. YALIMO UMEWALISHA NINI MPAKA WOTE WAKAWA NA 200 KG??? MAWESE!!!
 
mimi siuzi kinda hata moja nimefungua baa yangu nauza nyama choma ya ngurue kilo sh. 10000. na vinywaji. na ngurue wangu ni wakubwa mno wanaweza kutoa hadi kilo 200 mpaka 250.

Kama hz kilo n kweli, nahitaji jike moja, Kwa bei utakayo amua ww
 
Nguruwe wa kilo 200? Nguruwe bora ni wale wa kilo 70-80 zaidi ya hapo mhhh. Anza huo mradi unalipa sana.

Hawa wa huu uzito bado nao n kaz vile vile, au wafungwe kwa angalau miez 10 mpk mwaka
 
Back
Top Bottom