Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Nilianza kufuga nguruwe Sep. 2019, nilianza na nguruwe 11 ila watatu ni kama wamedumaa naombeni msaada wa kuwafanya afya yao iwe vizuri?



NB: Ni mgeni kabisa kwenye ufugaji hata formula ya chakula huwa nagoogle ila nawachanganyia viru kama Pig boost hivi karibuni nimeanza kuwachanganyia pig extra.
 
Nilianza kufuga nguruwe Sep. 2019, nilianza na nguruwe 11 ila watatu ni kama wamedumaa naombeni msaada wa kuwafanya afya yao iwe vizuri?



NB: Ni mgeni kabisa kwenye ufugaji hata formula ya chakula huwa nagoogle ila nawachanganyia viru kama Pig boost hivi karibuni nimeanza kuwachanganyia pig extra.
Unawachanganyia kwenye chakula gani?
Au wana minyoo!
 
Formula ya chakula huwa nachanganya vitu vifuatavyo
  1. Pumba za mahindi,
  2. Mahindi yaliyobaraswa,
  3. Mashudu ya Alizeti
  4. Dagaa
  5. Damu iliyokaushwa (Muda mwingine)
  6. Chokaa ya Wanyama
  7. Chumvi

Dawa ya Minyoo wamechomwa week 2 zilizopita
Mkuu, huo mchanganyiko uko vizuri, na dawa ya minyoo umesema umewachoma wiki mbili zilizopita, subiri matokeo, au ndiyo miili yao tu,
Si unajua penye mamba na kenge hawakosi!
 
astaghafirllah wewe unaleta ukafir humu tutakutangazia expire date yako...naanza nimesema mwisho wa kupost haram zako ni mwaka huu....nitakushtakia kwa muumbaji wa vidole na mdomo wako ili aone unavyodhulumu watu
Haramu kwako halali kwa mwingine shekhe
 
1.Nguruwe anachukua miezi 6 mpaka 12 mpaka kufikia uzito wa kutosha (inategemeanan na malisho)
2.Inategemeana na nafasi yako, ukiwa upo pale full time, wapagazi watatu ni more than enough (kumbuka usipokuwapo watu wanakuwa na uzembe flan). mimi nnao sita chini ya usimamizi mkali.
3.inategemea uko wapi. huku kwetu hata kama haulimi gunia la pumba za mahindi ni Tsh 10,000/=! mashudu ya alizeti gunia ni 20,000/=!
4. Ekari moja wanakaa kwa amani yote. ni vizuri kuwa mbali na makazi ya watu.
5. inategemea uko wapi. kwangu mm nauwezo wa kuuza nguruwe 200 kwa mwezi bila shida. watoto inasumbua kidogo kwa sababu wananunua wafugaji, ukitaka kuwauza kwa urahisi wakuze mpaka miezi mitatu hv.
6. Minyoo na ukurutu. Kikubwa ni chanjo na usafi wa hali ya juu KILA SIKU (nguruwe ni msafi sana akitunzwa, wa kwangu nikimkuta sebuleni nacheka tu-ni WASAFI kama pet)

Nguruwe wanahitaji usimamizi wa karibu sana, uwajue kwa namba ili uweze kufuatilia maendeleo yao kila asubuhi. Ukiona mnyama mmoja amezubaa mwite doctor haraka sana. usiachie wasaidizi kila kitu, kuwa makini na kuhakikisha wanapata milo miwili ya kutosha bila kusahau vegs. nguruwe wanapenda maji-usiwanyime starehe ya kwa kuwabananisha hawatanenepa vya kutosha. Nguruwe ana uwezo wa kuzaa mara mbili kwa mwaka. Mimi sijasoma kilimo na mifugo, ni ubishi tu na kuthubutu vilivyoletwa na maisha magumu. MUHIMU UKUBALI KUKAA SHAMBA, JF UIPATE KWA TTCL NA SOLLAR!
Kwa wastani nguruwe anaweza kula kilo ngapi kwa mwaka ?
 
Habari wakuu, naomba kujua ukweli apa nasikia ukipandisha jike kwa dume waliozaliwa mama mmoja watoto watakao zaliwa wanakufa muda mfupi baada ya kuzaliwa.
 
Habari wakuu, naomba kujua ukweli apa nasikia ukipandisha jike kwa dume waliozaliwa mama mmoja watoto watakao zaliwa wanakufa muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Ukipandisha jike na dume ambao ni ndugu, kuna uwezekano wa haya kutoke;
1, Mimba kuharibika.
2, Kuzaliwa watoto "goi goi" hawana nguvu wala afya! Watoto dhaifu.
3, Kimungu mungu, kimiujiza ujiza wakaishi na wakakua!
 
Huuu ugonjwa uliotangazwaa Leo umenitibulia biashara yangi ambayo kilasiku nakunyaaa laki moja mpk SAS nimeuzaa kilo 2 tu cjuii itakuaje watu wakisusa kbsa kulaa nguruwee
 
Back
Top Bottom