Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

wakuu kwanza natanguliza shukrani zangu kwa wote wanao toa michango changamoto na mawazo juu ya kilimo na ufugaji.kwa mda mrefu nimekuwa msomaji tuu hapa na nikapata wazo ambalo kadri siku zinavyokwenda naona kama harafu ya kuwa na maisha angalau bora inanukia kwa karibu sana.

nimekuwa na wazo hili la ufugaji kwa mda mrefu sana.aina ya mifugo ambayo naifikiria kufuga ni NGURUWE KUKU WA KIENYEJI na hivi karibuni na wazo la kware.

ila hasa ni nguruwe na kuku wa kienyeji lkn hasa hasa nguruwe.

nataka nifanye ufugaji huu kwa kiwango cha kusasa kidogo kwa uhakika sio ubabaishaji lkn kabka sijaanza ufugaji kuna mambo nilikuwa nahitaji kuyakamilisha pamoja na kuyafanyia uchunguzi na kupata ujuzi na utaalam wa kutosha.

kwanza kabisa kupata elimu ya ufugaji wa nguruwe ili niweze pata matokeo mazuri ya ufugaji wangu.

elimu juu ya malazi bora na matunzo chakula kinga na tiba.

kuhusu eneo lakufanyia ufugaji huu kwa kweli lipo kubwa sana.zaidi ya ekari 100 hivyo nilifikili baadhi ya vyakula nivilime mwenyewe.

kwa sasa mm nipo dar maisha ya mjini kiasi flani yamenichosha nishakaa sana sioni mabadiliko zaidi ya umri kunitupa mkono.

nimejichanga mpaka sasa nakama milion 5 hivyo nahisi kwa kuanzia kama zinatosha.

nina mdogo wangu ambaye alimaliza form 4 miaka kama 3 iliyopita na sasa yupo tu mtaani nilikuwa na wazo lakumpeleka sehem wanapotoa elimu ya ufugaji wa nguruwe na.kuku ili tukiingia kwenye ufugaji tuwe na elimu kiasi flani na uelewa wa nn tunaenda kukifanya.

na huyo mdogo wangu ndio nategemea yeye ndio awe msimamizi na mwangalizi mkuu sababu mm nitakuwa naendelea na mchakato wa kujiingizia kipato kidogo ili niweze kukidhi majitaji madogo madogo kwa mda ambao tutakuwa hatujaanza kupata mavuno ya ufugaji.

mm nikijana mwenye umri wa miaka 27 kama kuna mdau atakuwa tayari kutaka kuungana na mm au kunisaidia kimawazo au kunipa elimu juu ya huu ufugaji plz asisite.
 
Angalia kwenye ujasiriamali thread inaitwa:uzoefu wa ufugaji nguruwe wenye faida
 
safi sana mkuu wazo la nguruwe nami ninalo mda mrefu sana ni wazo zuri sana japokua nguruwe anachukua mda mrefu mpaka awe mwenye kilo za kutosha na kuzaa pia ngoja wenye elimu waje watoe hapa..
 
wakuu kwanza natanguliza shukrani zangu kwa wote wanao toa michango changamoto na mawazo juu ya kilimo na ufugaji.kwa mda mrefu nimekuwa msomaji tuu hapa na nikapata wazo ambalo kadri siku zinavyokwenda naona kama harafu ya kuwa na maisha angalau bora inanukia kwa karibu sana.

nimekuwa na wazo hili la ufugaji kwa mda mrefu sana.aina ya mifugo ambayo naifikiria kufuga ni NGURUWE KUKU WA KIENYEJI na hivi karibuni na wazo la kware.

ila hasa ni nguruwe na kuku wa kienyeji lkn hasa hasa nguruwe.

nataka nifanye ufugaji huu kwa kiwango cha kusasa kidogo kwa uhakika sio ubabaishaji lkn kabka sijaanza ufugaji kuna mambo nilikuwa nahitaji kuyakamilisha pamoja na kuyafanyia uchunguzi na kupata ujuzi na utaalam wa kutosha.

kwanza kabisa kupata elimu ya ufugaji wa nguruwe ili niweze pata matokeo mazuri ya ufugaji wangu.

elimu juu ya malazi bora na matunzo chakula kinga na tiba.

kuhusu eneo lakufanyia ufugaji huu kwa kweli lipo kubwa sana.zaidi ya ekari 100 hivyo nilifikili baadhi ya vyakula nivilime mwenyewe.

kwa sasa mm nipo dar maisha ya mjini kiasi flani yamenichosha nishakaa sana sioni mabadiliko zaidi ya umri kunitupa mkono.

nimejichanga mpaka sasa nakama milion 5 hivyo nahisi kwa kuanzia kama zinatosha.

nina mdogo wangu ambaye alimaliza form 4 miaka kama 3 iliyopita na sasa yupo tu mtaani nilikuwa na wazo lakumpeleka sehem wanapotoa elimu ya ufugaji wa nguruwe na.kuku ili tukiingia kwenye ufugaji tuwe na elimu kiasi flani na uelewa wa nn tunaenda kukifanya.

na huyo mdogo wangu ndio nategemea yeye ndio awe msimamizi na mwangalizi mkuu sababu mm nitakuwa naendelea na mchakato wa kujiingizia kipato kidogo ili niweze kukidhi majitaji madogo madogo kwa mda ambao tutakuwa hatujaanza kupata mavuno ya ufugaji.

mm nikijana mwenye umri wa miaka 27 kama kuna mdau atakuwa tayari kutaka kuungana na mm au kunisaidia kimawazo au kunipa elimu juu ya huu ufugaji plz asisite.

Ufugaji ni muunganiko wa mambo mengi sana.
1. Ujue unataka kufuga nini?
2. Unafugia wap?
3. Unafugaje?
4. Unafuga kwa ajili gani?
5. Soko lipo wapi?

Kabla hujaanza hiyo project yako jiulize hayo maswali hayo hapo juu.
Unatakiwa kupata taarifa ya kila hatua utakayopitia.
Unahitaji mbegu bora ya nguruwe, unahitaji wataalamu wa mifugo, unahitaji ku-link na soko etc.

Kwa ushauri wangu mwepesi fanya utafiti kwanza then ndo uingie ukiwa unajua kila kitu.
 
wakuu kwanza natanguliza shukrani zangu kwa wote wanao toa michango changamoto na mawazo juu ya kilimo na ufugaji.kwa mda mrefu nimekuwa msomaji tuu hapa na nikapata wazo ambalo kadri siku zinavyokwenda naona kama harafu ya kuwa na maisha angalau bora inanukia kwa karibu sana.

nimekuwa na wazo hili la ufugaji kwa mda mrefu sana.aina ya mifugo ambayo naifikiria kufuga ni NGURUWE KUKU WA KIENYEJI na hivi karibuni na wazo la kware.

ila hasa ni nguruwe na kuku wa kienyeji lkn hasa hasa nguruwe.

nataka nifanye ufugaji huu kwa kiwango cha kusasa kidogo kwa uhakika sio ubabaishaji lkn kabka sijaanza ufugaji kuna mambo nilikuwa nahitaji kuyakamilisha pamoja na kuyafanyia uchunguzi na kupata ujuzi na utaalam wa kutosha.

kwanza kabisa kupata elimu ya ufugaji wa nguruwe ili niweze pata matokeo mazuri ya ufugaji wangu.

elimu juu ya malazi bora na matunzo chakula kinga na tiba.

kuhusu eneo lakufanyia ufugaji huu kwa kweli lipo kubwa sana.zaidi ya ekari 100 hivyo nilifikili baadhi ya vyakula nivilime mwenyewe.

kwa sasa mm nipo dar maisha ya mjini kiasi flani yamenichosha nishakaa sana sioni mabadiliko zaidi ya umri kunitupa mkono.

nimejichanga mpaka sasa nakama milion 5 hivyo nahisi kwa kuanzia kama zinatosha.

nina mdogo wangu ambaye alimaliza form 4 miaka kama 3 iliyopita na sasa yupo tu mtaani nilikuwa na wazo lakumpeleka sehem wanapotoa elimu ya ufugaji wa nguruwe na.kuku ili tukiingia kwenye ufugaji tuwe na elimu kiasi flani na uelewa wa nn tunaenda kukifanya.

na huyo mdogo wangu ndio nategemea yeye ndio awe msimamizi na mwangalizi mkuu sababu mm nitakuwa naendelea na mchakato wa kujiingizia kipato kidogo ili niweze kukidhi majitaji madogo madogo kwa mda ambao tutakuwa hatujaanza kupata mavuno ya ufugaji.

mm nikijana mwenye umri wa miaka 27 kama kuna mdau atakuwa tayari kutaka kuungana na mm au kunisaidia kimawazo au kunipa elimu juu ya huu ufugaji plz asisite.

Hongera kwa wazo zuri na maono. Mimi niafuga hao vitimoto, na mpaka sasa nimefikisha kama 250 hivi. Kitu muhiimu sana nachoweza kukuambia ni chakula, hao wanakula usiombe, madawa, yaani kuwepo na mtaalam ambaye anakuja kuwaona angalau after every two weeks, minyoo inawafanya wadumae sana, ingawaje ni wavu,ulinu saana! Ila ukitaka kufuga vizuri, watunze, vizuri, usafi wa mabanda, upatikanaji wa maji ya uhakika ni lazima. jitahidi na sakafu iwe imara sana, huwa wanachimba hawa utapata kazi ya ku repair kila baada ya miezi 6 usipoimarisha sakafu yao.

Ukifikia idadi kubwa, uanze kufikiria ka bajaji, au pick up, au ka canter, kulingana na uwezo. Mimi nina ka canter tan 1.5, kananisaidia sana kufuata vyakula masokoni nk.

Sina picha, ntapiga niweke inaweza kuhamasisha wengine pia.

Soko ni kuubwa huwezi kulimaliza. na wakijua unauza utawachoka, huwezi kusupply watatosheka.

Vinginevyo, nipo Mwanza, ukipenda kuja kuwaona, ni PM
 
Idea ni nzuri but huyo mdogo wako unaetaka awe msimazi una uhakika na yeye anataka hiko hiko?
Asije kuwa na ndoto zingine kabisa
wewe unapanga yako na yeye anapanga yake

Muhimu wewe ujifunze kila kitu
halafu msimamizi umfunze wewe
akiharibu unatafuta msimamizi mwingine unamfunza
 
hello team
nataka kufuga nguruwe dar

naomba mwongozo niaze na wangap sehem gan nzuri kwa dar
 
Shukurani za dhati mweneye uzi One Month Semindu, homeboy MalafyaleP na Maishamema,

Ninapita nondo mlizoziweka kwa karibu, nia yangu ni kufugia hapo eneo la Chalinze,

Nitaanza na hao Majike 8 badala ya watoto 50 nilioazimia mwanzoni, lkn ikiwa nataka niwe na kundi nitakalolinenepesha ili niwauze ndani ya miezi walau 6 nifanyeje?

Mwisho wa kusema haya naombeni kuuziwa majike myaonayokuwa ni bora 8 yaliyopandishwa na madume yafaayo kwa idadi hiyo na pia watoto 25 wa kuwanenepesha.
Masikini_Jeuri ulifikia wapi mkuu na hii project?
 
Last edited by a moderator:
Natambua wapo watu wengi ambao imani zao zinaruhusu wanatamani kufanya mradi wa ufugaji nguruwe wenye faida.Labda wengine wamejaribu bila mafanikio.Kwa uzoefu wangu ( refer thread yangu:Ufugaji na kilimo unalipa sana)hivi ndivyo waweza fanya kupata mfanikio.
1. Kwanza tambua hii ni agri-business,basi kama business nyingine inahitaji usimamizi wa kutosha. Watu hudhani ukianzisha mradi na kuweka kijana wa kuwalisha basi unangojea faida tu. Ni vema ukaelewa mahitaji ya hao wanyama (chakula,usafi,malazi,tiba na jinsi ya kuzuia magonjwa) na wewe sasa ndio uwe mwalimu wa herdman wako
2.Tambua faida inatokana na aina bora ya mbegu na malezi. Nia ni kuwalea wanyama wakue kufikia uzito wa soko kwa muda mfupi.Kwa kawaida nguruwe huuzwa kwa nyama akiwa na uzito kuanzia 50kg. Shambani kwangu huuzwa kuanzia miezi 5.
3. Waangalizi(herdmen) ni watu muhimu sana kwako.Ni lazima wafundishwe vizuri na maslahi yao yaangaliwe kwa makini
4. Nguruwe akiugua atibiwe mara moja. Nguruwe ni mnyama ambae haugui kirahisi akilelewa vema unless kama kuna outbreak ya ugonjwa(kama swine fever). Mara mojamoja huugua inabidi herdman awe na uwezo wa kugundua mapema na mnyama apewe tiba mara moja. Ukiwalea vizuri muda mwingi wanahitaji chanjo tu za minyoo na ukurutu
5. Nguruwe walishwe ration(balanced feed) sio pumba tu au masalia ya jikoni. Tambua mahitaji ya chakula ya nguruwe(protein,wanga,mafuta,madini,vitamin) na hakikisha mchanganyiko unaofaa kwa umri husika wa nguruwe.Shambani kwangu chakula kikuu ni mahindi/mtama,pumba za mahindi na mpunga,mashudu ya alizeti, ambayo tunalima hapo shamba.Pia huchanganya madini (nguruwe mix) na mifupa/chokaa
6. Tambua gharama kubwa ya ufugaji ipo kwenye chakula (atleast 70%). Kwa wastani nguruwe mkubwa anahitaji 2kg/siku. Kwa hiyo kumlea nguruwe mmoja hadi miezi 6 anahitaji 240kg(miezi 2 ya kwanza huwa ananyonya)
(a) ukininunua chakula ambacho tayari kimechanganywa gharama ni kama tshs 600/kg
(b) ukinunua vyakula na kuchanya mwenyewe gharama ni kama tshs.400/kg
(c) Ukilima vyakula na kuchanganya mwenyewe gharama ni kama tshs 150-250/kg
Hizo ni gharama za wastani kwa morogoro na Dar es salaam.Utaona kama waweza kulima mazao kwa ajili ya mifugo wako gharama inapungua sana. Nguruwe hula pia vyakula vingine kama mihogo,majani,viazi vitamu,maboga etc. Angalia vyakual rahisi kwa mazingira unayofuga
Faida yako ipo kwenye kuuza nguruwe wa nyama. Wanunuzi wa mbegu sio wengi na sio consistent. Kwa hiyo itakuchukua a minimum ya miezi 6 kuanza kupata faida kutoka kwenye mradi wako.Huu ndio ukweli. Lengo ni kuuza idadi fulani ya nguruwe Kila mwezi. Kwa mfano ingalau nguruwe 20 kila mwezi.Unadhani unahitaji nguruwe wangapi kwa wakati mmoja kufanikisha hilo???
8. Soko la nguruwe ni kubwa na linazidi kukua. Walaji wengi wapo Dar es salaam. Waweza kuuza live hapo shambani au ukapeleka mwenyewe machinjioni inategemeana na soko lipo mbali kiasi gani. Nguruwe wa miezi 6 anaweza kukuingizia tshs.200,000-300,000 kutegemea na namna ulivyouza na uzito 9.Unaanzaje kufuga kibiashara? Mfano.
(a) Faida ndani ya miezi 6,na kuuza nguruwe 20 kila mwezi.
Nunua nguruwe jike wenye mimba uzao wa 2 ; wa2 mimba miezi 3;wa2 miezi 2 na wa2 mimba mwezi1,wa2 ambao ndiowamepandwa na wa2 wenye umri wa miezi 6. Nunua kwa mfugaji mwenye mbegu inayoanza kuzaa mapema. Ukinunua wa uzao wa kwanza namba inakuwa nguruwe 3 badala ya 2 kwa sababu uzao wa kwanza watoto ni wachache,6-9.Pia unahitaji dume mzuri mwenye umri wa miezi 8 au zaidi.Kwa namna hii kila mwezi nguruwe wa2(au 3) watazaa watoto sio chini ya 20. Utaanza kuuza mbegu ndani ya miezi 2.Na baada ya miezi 6 utauza nguruwe sio chini ya 20 kila mwezi kwa nyama
Nguruwe jike mwenye mimba waweza kumpata kwatshs350,000-400,000
Mauzo 4-6m kila mwezi. Neti profit itategemeana na gharamaza chakula kama nilivyo ainisha awali.
Shambani kwangu tunawaachisha watoto kunyonya wakiwa na week6 na jike hupata joto na kupandwa tena ndani ya siku 3-7. Hivyo nguruwe wetuhuzaa mara 2.5 kwa mwaka. Watoto huwauza wakiwa na miezi 2 kwa 45,000-60,000 kutegemeana uzito
(b) Kama utaanza kufuga nguruwe watoto wenye miezi 2?!
Ina maana utaanza kuuza nguruwe wa nyama baada ya miezi isiyopungua 14. Pia utahitaji kuwafanya nguruwe wako wapate mimba kwa groups ambayo inahitaji uzoefu wako na herdman. Utahitaji pia dume lenye umri wa miezi12 au zaidi. Pia kwa mtu anaeanza ufugaji inasumbua kidogo. Lakini ni nafuu kidogo interms of upfront capital though gharama za ufugaji zinaWEZA kuwa kubwa. Utahitaji kuanza nao wengi pia ili kupata faida na utahitaji kufuga muda mrefu kama nilivyoeleza hapo juu.
Kama una mpango wa muda mrefu na mtaji wa kugharamia chakula na mengineyo kwa muda mrefu,hii ni namna nzuri pia.
Kwa mtu anaetaka kufuga kibiashara,mie humshauri option 8(a) hapo juu
Shambani kwangu Morogoro kwa sasa nguruwe wa 2 au 3 wanazaa kwa mwezi. Kuanzia November nguruwe 5-7watazaa kwa mwezi.
Hope hii itawasaidia watakaopenda kujaribu hii project. Ni muhimu kutembelea mfugaji halisi kupata uzoefu kabla ya kuanza ufugaji.
NYONGEZA1
Mojawapo ya vitu watu wanakosea wakati wa kuanza ufugaji wa nguruwe ni uchaguzi wa mbegu bora.Wengi anapotembelea mtu anaefuga na kukuta nguruwe wakubwa wanapata hamasa bila kuuliza maswali muhimu yatakayomsaidia kujua kama mbegu anayoona inafaa.
Mtu anaefuga kibiashara huwa na:majike na dume(au madume kutegemea na idadi ya majike).Lengo ni kuzalisha nguruwe wa kutosha watakaokua haraka na pia kuwa na nyama nzuri(isiyo na mafuta mengi) wakati wa kuuza akiwa na miezi 6 au 7.Ni vema basi ukjua sifa za jike na Dume!
Dume:iwe mbegu inayokua haraka na kuzalisha nyama nzuri.unapochagua asiwe na ulemavu wowote na awe na matiti 12 au zaidi. Large white,duroc,hampshire na crosses zake zinafaa.Ukiweza kupata first cross za duroc au hampshire ni wazuri zaidi kuwatumia kama terminal sire(dume wa kuzalishia nguruwe wako wa mauzo)
Jike:awe kutoka mbegu zinazozaa watoto wengi na pia uwezo mzuri wa kulea watoto.Awe na matiti 12 au zaidi.ni vema kutoka kwenye crosses za largewhite na landrace.Pia saddle back na crosses zake.

Kwa leo ni hayo.nitaendelea ku-update hii thread ninapokuwa na muda kwa topic mbalimbali.Ninatambua kuna breeds nzuri zaidi kama camborough,etc.nilizoelezea hapo ni breeds unazoweza kupata kirahisi humu nchini.
Mheshimiwa nimefuatilia sna thread zako, nimekuwa interested sana kwa kweli, ila mimi naomba contacts zako nataka kuja uko kwa ajili ya kujifunza ufugaji wa nguruwe plz, kama utapata hii mesg naomba unitafute kwa kupitia(nestoryedward@yahoo.com )
 
Nnauza wa nyama 40-50 nguruwe every 2 months,sometimes every month.nauza pia significantly wenye mimba kwa wafugaji wapya
 
nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000
banda la mabanzi=1,000,000
chakula = 1,000,000
dawa= 200000
after 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,
utachakuwa vitoto jike 100,
mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
mkubwa ni tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000
after 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700
kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike)
year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
kutoka hapo unamentein number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500
1500*200000= tsh 300,000,000/= kwa mwaka
nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
welcome to the club

kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu.
Kila mwaka nalima mahindi, alizeti, maboga ekari 30 kwa ajili ya chakula cha
nguruwe tu.

Nakupenda saana mpwa,

mkuu mm ni mgeni kidogo humu nmemekua nikipitia huu mjadala tangu mwanzo mpaka sasa na nmetokea kuuelewa sana na ningependa kufanya hii project.......ubarikiwe sana
 
Naomba mtu aliye mkoa wa Kilimanjaro hususani Wilaya ya Hai....anipm tufanye hii project kwa Share...akiwa na eneo lenye mabanda itakuwa ni vizuri zaidi...niko na mtaji wa 2.5m
 
Back
Top Bottom