Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Hivi mtoa mada alikuwa na mpango wa nguruwe wa kisasa au ilikua ni Hawa kienyeji?
 
Nasikia Kuna taarifa za ugonjwa wa nguruwe uko mbeya na mikoa ya jiran,wanakufa hatari
 
BREAKING

Jipatie mashine mbalimbali za Kilimo na Ufugaji kwa gharama nafuu,

■Mashine moja inayosaga na kukoboa.

■Mashine ya kumenyea Mahindi.

■Mashine ya kupukuchukua Mahindi.

■Mashine ya kupigia Mpunga.

■Mashine ya kuchakata Majani kwa ajili ya mifugo.

■Mashine ya kuchanganyia Chakula cha kuku, Samaki n.k

Ofisi ipo Lumumba, mkabala na Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es salaam

Mikoani tunatuma

Kwa mawasiliano piga
0622 896789
 
1.Nguruwe anachukua miezi 6 mpaka 12 mpaka kufikia uzito wa kutosha (inategemeanan na malisho)
2.Inategemeana na nafasi yako, ukiwa upo pale full time, wapagazi watatu ni more than enough (kumbuka usipokuwapo watu wanakuwa na uzembe flan). mimi nnao sita chini ya usimamizi mkali.
3.inategemea uko wapi. huku kwetu hata kama haulimi gunia la pumba za mahindi ni Tsh 10,000/=! mashudu ya alizeti gunia ni 20,000/=!
4. Ekari moja wanakaa kwa amani yote. ni vizuri kuwa mbali na makazi ya watu.
5. inategemea uko wapi. kwangu mm nauwezo wa kuuza nguruwe 200 kwa mwezi bila shida. watoto inasumbua kidogo kwa sababu wananunua wafugaji, ukitaka kuwauza kwa urahisi wakuze mpaka miezi mitatu hv.
6. Minyoo na ukurutu. Kikubwa ni chanjo na usafi wa hali ya juu KILA SIKU (nguruwe ni msafi sana akitunzwa, wa kwangu nikimkuta sebuleni nacheka tu-ni WASAFI kama pet)

Nguruwe wanahitaji usimamizi wa karibu sana, uwajue kwa namba ili uweze kufuatilia maendeleo yao kila asubuhi. Ukiona mnyama mmoja amezubaa mwite doctor haraka sana. usiachie wasaidizi kila kitu, kuwa makini na kuhakikisha wanapata milo miwili ya kutosha bila kusahau vegs. nguruwe wanapenda maji-usiwanyime starehe ya kwa kuwabananisha hawatanenepa vya kutosha. Nguruwe ana uwezo wa kuzaa mara mbili kwa mwaka. Mimi sijasoma kilimo na mifugo, ni ubishi tu na kuthubutu vilivyoletwa na maisha magumu. MUHIMU UKUBALI KUKAA SHAMBA, JF UIPATE KWA TTCL NA SOLLAR!
Unapatikana maeneo gani mkuu
 
Ndio nimeanza kufuga, napitia thread humu sioni wataalamu wa nguruwe naombeni maujuzi na mimi nije niitwe tajiri
 
Back
Top Bottom