Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

wanunuzi kuna ambao wanakufata hadi kwenye mabwawa wakanunua kwa jumla na ukiamua wewe mwenyewe unaweza fungua duka la samaki ukauza reja reja. bei kwa kilo ni kuanzia elfu saba

Mkuu naomba kama una contacts za wanunuzi wa jumla wa samaki (sato) unifahamishe.
Asante sana.

Roky.
 

Hapo kwenye chakula, changamoto ni bei ya hicho chakula.
Mfuko wa kilo 15 ni sh. 40,000 hadi sh. 45,000...!!
 

Kiongozi, kuna uzi nilifungua kuelezea makosa yanayofanyika katika ufugaji wa samaki. Mojawapo ni chanzo cha mbegu. Pili, usimamizi na uhudumiaji wa bwawa. Fika wizara ya mifugo na uvuvi utapata takwimu za wapi ukajifunze na mengineyo.

Narudia tena kabla ya kuchukua vifaranga kwa mzalishaji wasiliana na wataalam wa wizara.
 

Sawa mkuu
 

Kiongozi. Ufugaji wa matanki unaouona kwa wenzetu ni intensity one. Kwa maana wanaweka samaki samaki wengi kwa cubic meter (mita za ujazo). kwa mfano samaki 20-50 kwa mita cubic.

Lakini huduma yake ni ya hali ya juu. Kwanza, maji yanaingia na kutoka masaa 24 au kila baada ya masaa kadhaa. Pili, hewa ya ziada ni wakati wote.

Tatu, chakula ni cha kulisha tu na ni quality feed. Kwahiyi hapo umeme wa uhakika 24hrs. Uzalishaji ni wa hali ya juu. Note: Ubadilishaji wa maji upo wa haina mbili. Kuzungusha maji hayo hayo kwa.kufanya saome treatments au kuinguza maji.mapya kabisaa. Mwisho, ukitempa na uangalizi vifo ni mara moja. Karibu kwa maswali kuhusu ufugaji huu
 

Nakubaliana na wewe tuwaombe SIDO walifanyie kazi hili suala. Pia kuna suala la aerators pamoja na vipuli vinginevyo. Lakini pia kuna suala la ingredients.za.chakula cha samaki wakulima.wetu wanaweza.kulivalia njuga. Cha ajabu ukinunua chakula nje unatumia.2000-2080 tzs kwa kilo lakini bongo hapa unatumia 3000 up.
 
Long time kiongozi. Naomba feedback ikiwa kama ulianza. Pia karibu kwa discussion kwa chochote ulichokipata kuhusu ufugaji. Nipo flexible

Nimeanza
shida yangu wanunuzi
unajua namna ya kunisaidia?
 
Nauza pump na filter zake, hizi kwa fish pond, litter 10,000 per hour. any interest. Tuwasiliane PM
 
Nimeanza
shida yangu wanunuzi
unajua namna ya kunisaidia?
Umefikisha average weight gram ngapi? Kuna masoko ya jumla mawili ambayo yanategemea uzito wa samaki ( haya yapo tu). Pia kuna mama ananunua lakini uwezo wake sio kilo zaidi ya 300.
 
ufugaji wa samaki huwa unahitaji mtaji wa kiasi gani minimum?
 
ufugaji wa samaki huwa unahitaji mtaji wa kiasi gani minimum?
Inategemea na eneo lako kama ni mfinyanzi au mchanga. Vile vile ni mfumo gani wa uzalishaji unatumia....rejea thread hapo juu. Gharama za uchimbaji na ujenzi zitakuwa zimepanda kidogo. Ukijibu hayo utapatiwa gharama
 
Samaki ni bidhaa adimu hata kwa mikoa ya kanda ya ziwa inakuwaje unasema tatizo ni wanunuzi?

naitaji kununua vifarang wa samaki 1000..naombeni mchanganuo wa gharama za kuwanunua,kuwafuga hadi kuuza bila kusahau gharama za vifaa nataka kutumia tank...!!
 
naitaji kununua vifarang wa samaki 1000..naombeni mchanganuo wa gharama za kuwanunua,kuwafuga hadi kuuza bila kusahau gharama za vifaa nataka kutumia tank...!!

Inategemea na aina gani unahitaji kufuga
 
sheria inasemaje kuhusu kujenga vizimba kwenye mito?

Kwanza uainishe eneo husika na kuomba kibali cha kutumia eneo hilo katika halmashauri husika na kama kuna mamlaka maalum ya usimamizi.

Kisha, fanya environment impact assessment kuona kuna athari gani utasababisha kwa ufugaji huo.

Mwisho omba kibali cha kufuga wizara ya mifugo na uvuvi kama matokeo ya EIA ni rafiki kwa mradi na jamii.
 
Nimeanza
shida yangu wanunuzi
unajua namna ya kunisaidia?

Wapo wafugaji wanatafuta soko, wapo wanunuzi wanatafuta samaki.

1. Kwa soko la uhakika wape mawasiliano yako na aina za samaki unaofuga kwenye chuo cha samaki cha Mbegani.

2. Kama una usafiri peleka samaki wako kwenye soko la feri, waone wahusika utalipishwa ushuru wa soko na utafanya biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…