Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

wanunuzi kuna ambao wanakufata hadi kwenye mabwawa wakanunua kwa jumla na ukiamua wewe mwenyewe unaweza fungua duka la samaki ukauza reja reja. bei kwa kilo ni kuanzia elfu saba

Mkuu naomba kama una contacts za wanunuzi wa jumla wa samaki (sato) unifahamishe.
Asante sana.

Roky.
 
Ufugaji samaki ni tasnia inayokua kwa kasi duniani hata hapa nchini ni kweli inakua. Hali halisi ya kijiografia hapa nchini ni chachu ya maendeleo ya ufugaji samaki.

Kwa wakulima waliokwishaanza naombeni majibu yenu kwa maswali yangu haya.

1. Je! kuna yeyote ambaye amevuna samaki aina ya sato wenye nusu au kilo moja ndani ya miezi kuanzia sita, tisa na mwaka mmoja ?

2. kuna yeyote ambaye amefuga madume tu? (sato) na vipi ukuaji wake upoje ?

3. Kwa mtazamo wako we unaonaje kati ya kufuga samaki mchanganyiko jinsia zote au jinsia moja, upi kwako umeona ni bora.

4. Changamoto ya chakula unaionaje ?

ANGALIZO: Usitumie majibu ya kugoogle au kufundishwa darasani. Majibu yalenge hali halisi ya kijiografia Tanzania

Hapo kwenye chakula, changamoto ni bei ya hicho chakula.
Mfuko wa kilo 15 ni sh. 40,000 hadi sh. 45,000...!!
 
Habari za leo wadau?

Mimi kuhusu ufugaji samaki nimehamasika ila napenda niwafahamu ma kuwatembelea wafugaji samaki waliofanikiwa. Hapa nina maanisha walioweza kuuza samaki wakiwa na miezi sita kwa uzito mzuri. Hii imetokana na kwamba ktk hii biashara tunaenda kinadharia mno. Uzalishaji unaoongelewa siyo ambao unapatikana kihalisia labda mimi huwa nakutana na waliofeli tu. Maana huwa wanakalamika samaki wanadumaa. Wadau niunganisheni na waliofanikiwa.

Kiongozi, kuna uzi nilifungua kuelezea makosa yanayofanyika katika ufugaji wa samaki. Mojawapo ni chanzo cha mbegu. Pili, usimamizi na uhudumiaji wa bwawa. Fika wizara ya mifugo na uvuvi utapata takwimu za wapi ukajifunze na mengineyo.

Narudia tena kabla ya kuchukua vifaranga kwa mzalishaji wasiliana na wataalam wa wizara.
 
Bandugu,

Hakika Elimu Bahari. Kwa muda mrefu nimekuwa na hamu ya kufahamu mengi juu ya UFUGAJI WA SAMAKAI kibiashara na kwa ajili ya kitoweo (maana kwa kweli nakipenda sana kitoweo hiki). Leo nimepata mwanga baada ya kuutembelea uzi huu. tafadhali Bw Ha Muji naomba contacts zako tuwasiliane zaidi.

TCHAO!

Sawa mkuu
 
ndugu hebu funguka vizuri bana kama unatubania uhondo vile... unajua sisi wengine ambao mahesabu yametupita ukianza kutaja squire mita basi ndio hatuelewi kabisa..ok najua wewe kama mtaalam unaweza ukaniambia mzunguruko wa tank wa kiasi gani unaweza ukaweka samaki 1000(mfano) inawezekana nikaenda kwenye viwanda vya plastic tank nikatoa order wakanitengenezea ukweli ufugaji wa samaki ukisoma maelezo utajiri unauona huu hapa ila tukija kwenye utendaji hasa huu ufugaji wa kisasa ni shughuli pevu....na hapo unaposema unajaza maji kwa lita moja sijakupata kidogo... halafu hivi hizi pump unakuwa unaiwasha kwa muda au ni kuanzia unapoingiza samaki mpaka unapowavuna... chanzo changu cha maji nategemea maji ya kuleta na gari ambayo sio ya chumvi.... hii project kk inaniumiza kichwa acha ukweli ninao kuku wa nyama ni mmbadala wa samaki ila nikipata taarifa za kutosha kuhusu ufugaji huu kweli murrano yangu naiona ilee ikitokea japan....over

Kiongozi. Ufugaji wa matanki unaouona kwa wenzetu ni intensity one. Kwa maana wanaweka samaki samaki wengi kwa cubic meter (mita za ujazo). kwa mfano samaki 20-50 kwa mita cubic.

Lakini huduma yake ni ya hali ya juu. Kwanza, maji yanaingia na kutoka masaa 24 au kila baada ya masaa kadhaa. Pili, hewa ya ziada ni wakati wote.

Tatu, chakula ni cha kulisha tu na ni quality feed. Kwahiyi hapo umeme wa uhakika 24hrs. Uzalishaji ni wa hali ya juu. Note: Ubadilishaji wa maji upo wa haina mbili. Kuzungusha maji hayo hayo kwa.kufanya saome treatments au kuinguza maji.mapya kabisaa. Mwisho, ukitempa na uangalizi vifo ni mara moja. Karibu kwa maswali kuhusu ufugaji huu
 
Wadau wa ufugaji samaki tunakabiliwa na changamoto nyingi . Binafsi naamini tunaweza kutatua baadhi ya changamoto sisi wenyewe bila kusubiri wazungu au wachina ikiwa tutaamua kwa dhati. Malighafi zote tunazo tunachohitaji ni akili ya ubunifu tu na mtaji ambao naamini baadhi yetu wanavyo. Mfano: Changamoto ya upatikanaji wa floating pellets inaweza kwisha tukibuni simple and cheap pelleting machine kwa kushirikiana na ndugu zetu wa SIDO kinachotakiwa ni sisi kuwapelekea SIDO wazo letu na details ya kitu tunachokitaka, hawa jamaa hawavumi lakini wamo wamebuni vitu vingi sana vyenye manufaa kwa wakulima eg. mashine ya kutengeneza mkaa kw kutumia vumbi ya mkaa, incubators, water pumps, mashine za kupukuchua mahindi/karanga/kukata viazi, kubangua korosho/kahawa, kuvuna mpunga n.k

Nakubaliana na wewe tuwaombe SIDO walifanyie kazi hili suala. Pia kuna suala la aerators pamoja na vipuli vinginevyo. Lakini pia kuna suala la ingredients.za.chakula cha samaki wakulima.wetu wanaweza.kulivalia njuga. Cha ajabu ukinunua chakula nje unatumia.2000-2080 tzs kwa kilo lakini bongo hapa unatumia 3000 up.
 
Long time kiongozi. Naomba feedback ikiwa kama ulianza. Pia karibu kwa discussion kwa chochote ulichokipata kuhusu ufugaji. Nipo flexible

Nimeanza
shida yangu wanunuzi
unajua namna ya kunisaidia?
 
Nauza pump na filter zake, hizi kwa fish pond, litter 10,000 per hour. any interest. Tuwasiliane PM
 
Nimeanza
shida yangu wanunuzi
unajua namna ya kunisaidia?
Umefikisha average weight gram ngapi? Kuna masoko ya jumla mawili ambayo yanategemea uzito wa samaki ( haya yapo tu). Pia kuna mama ananunua lakini uwezo wake sio kilo zaidi ya 300.
 
ufugaji wa samaki huwa unahitaji mtaji wa kiasi gani minimum?
 
ufugaji wa samaki huwa unahitaji mtaji wa kiasi gani minimum?
Inategemea na eneo lako kama ni mfinyanzi au mchanga. Vile vile ni mfumo gani wa uzalishaji unatumia....rejea thread hapo juu. Gharama za uchimbaji na ujenzi zitakuwa zimepanda kidogo. Ukijibu hayo utapatiwa gharama
 
Samaki ni bidhaa adimu hata kwa mikoa ya kanda ya ziwa inakuwaje unasema tatizo ni wanunuzi?

naitaji kununua vifarang wa samaki 1000..naombeni mchanganuo wa gharama za kuwanunua,kuwafuga hadi kuuza bila kusahau gharama za vifaa nataka kutumia tank...!!
 
naitaji kununua vifarang wa samaki 1000..naombeni mchanganuo wa gharama za kuwanunua,kuwafuga hadi kuuza bila kusahau gharama za vifaa nataka kutumia tank...!!

Inategemea na aina gani unahitaji kufuga
 
sheria inasemaje kuhusu kujenga vizimba kwenye mito?

Kwanza uainishe eneo husika na kuomba kibali cha kutumia eneo hilo katika halmashauri husika na kama kuna mamlaka maalum ya usimamizi.

Kisha, fanya environment impact assessment kuona kuna athari gani utasababisha kwa ufugaji huo.

Mwisho omba kibali cha kufuga wizara ya mifugo na uvuvi kama matokeo ya EIA ni rafiki kwa mradi na jamii.
 
Nimeanza
shida yangu wanunuzi
unajua namna ya kunisaidia?

Wapo wafugaji wanatafuta soko, wapo wanunuzi wanatafuta samaki.

1. Kwa soko la uhakika wape mawasiliano yako na aina za samaki unaofuga kwenye chuo cha samaki cha Mbegani.

2. Kama una usafiri peleka samaki wako kwenye soko la feri, waone wahusika utalipishwa ushuru wa soko na utafanya biashara.
 
Back
Top Bottom