Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Wakuu habari za muda huu, nimefanya tafiti ya wafugaji wengi wa samaki hupendelea kufuga sato na kambale, sijabahatika kuona sangara. Mwenye utaalamu na hili anijuze je, sangara hawafugiki kwenye mabwawa ya kujengwa kwa cementi?

Nilimuuliza mtaalam, fulani akanijibu kuwa Sangara hafugiki kwasababu ni ambae anahitaji kutembea masafa marefu sana anahitaji eneo kubwa kumfuga.

Samaki wanaofugwa kwa Tz ni Sato/perege (Tilapia) na kambare kwa maji baridi kwa maji chumvi ni Prawns, Milky fish (Mwatiko) na kaa
 
Honger, unafugia mkoa gani natak nijifunze maana huku niliko sijui barid mno miezi 6 still wadogo.!
 
Yeah ni kweli kabisa then hata ulishaji wa sangara wanahitaji nyama sana
 

Mm napenda na nataman sana kufuga samaki pamoja na kuku!!

nikitaka kufuga samaki kuanzia kujenga bwawa inatakiwa niwe na kias gan kwa kuanzia kiwango cha chini?
 
Mm napenda na nataman sana kufuga samaki pamoja na kuku!!

nikitaka kufuga samaki kuanzia kujenga bwawa inatakiwa niwe na kias gan kwa kuanzia kiwango cha chini?
Kiwango cha chini kabisa ni nguvu kazi yaani watu wa kukuchimbia bwawa charging ni kulingana na eneo na vifaranga ni kulingana na ukubwa wa bwawa pia uwe angalau 1000,000-1,500,000
 
Sato umewapata wapi
 
Ndugu zanguni nahitaji vizimba vya namna hii (angalia picha hapo chini);
1. Naweza kuvipata kwa urahisi kwa kuagiza kutoka nchi gani?
2. Bei yake ikoje?





 
Fugia ziwani ndugu, achana na mabwawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…