Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Wakuu habari za muda huu, nimefanya tafiti ya wafugaji wengi wa samaki hupendelea kufuga sato na kambale, sijabahatika kuona sangara. Mwenye utaalamu na hili anijuze je, sangara hawafugiki kwenye mabwawa ya kujengwa kwa cementi?

Nilimuuliza mtaalam, fulani akanijibu kuwa Sangara hafugiki kwasababu ni ambae anahitaji kutembea masafa marefu sana anahitaji eneo kubwa kumfuga.

Samaki wanaofugwa kwa Tz ni Sato/perege (Tilapia) na kambare kwa maji baridi kwa maji chumvi ni Prawns, Milky fish (Mwatiko) na kaa
 
Aisee mimi nafanya ufugaji wa samaki wanalipa sana ila mitaji tu ni changamoto ili mtu uweze kuzalisha kwa wingi inahitaji eneo kubwa udril kisima kama una changamoto ya maji,ila kiufupi tu ni biashara inalipa kuliko ufugaji wa kuku,hao samaki wanaonekana Wana miezi 6/
20221122_162107.jpg
 
Aisee mimi nafanya ufugaji wa samaki wanalipa sana ila mitaji tu ni changamoto ili mtu uweze kuzalisha kwa wingi inahitaji eneo kubwa udril kisima kama una changamoto ya maji,ila kiufupi tu ni biashara inalipa kuliko ufugaji wa kuku,hao samaki wanaonekana Wana miezi 6/View attachment 2501235
Honger, unafugia mkoa gani natak nijifunze maana huku niliko sijui barid mno miezi 6 still wadogo.!
 
Nilimuuliza mtaalam, fulani akanijibu kuwa Sangara hafugiki kwasababu ni ambae anahitaji kutembea masafa marefu sana anahitaji eneo kubwa kumfuga.

Samaki wanaofugwa kwa Tz ni Sato/perege (Tilapia) na kambare kwa maji baridi kwa maji chumvi ni Prawns, Milky fish (Mwatiko) na kaa
Yeah ni kweli kabisa then hata ulishaji wa sangara wanahitaji nyama sana
 
Aisee mimi nafanya ufugaji wa samaki wanalipa sana ila mitaji tu ni changamoto ili mtu uweze kuzalisha kwa wingi inahitaji eneo kubwa udril kisima kama una changamoto ya maji,ila kiufupi tu ni biashara inalipa kuliko ufugaji wa kuku,hao samaki wanaonekana Wana miezi 6/View attachment 2501235

Mm napenda na nataman sana kufuga samaki pamoja na kuku!!

nikitaka kufuga samaki kuanzia kujenga bwawa inatakiwa niwe na kias gan kwa kuanzia kiwango cha chini?
 
Mm napenda na nataman sana kufuga samaki pamoja na kuku!!

nikitaka kufuga samaki kuanzia kujenga bwawa inatakiwa niwe na kias gan kwa kuanzia kiwango cha chini?
Kiwango cha chini kabisa ni nguvu kazi yaani watu wa kukuchimbia bwawa charging ni kulingana na eneo na vifaranga ni kulingana na ukubwa wa bwawa pia uwe angalau 1000,000-1,500,000
 
Nimetangaza bingo kwa machalii fulani kwamba mtu akiniletea kambale hai hata kama ni mdogo vipi nampa buku tano. Nawatafuta sana hawa samaki. Nimepata sato ila kambale bado. Mategemeo ni makubwa,nikishindwa kuwapata mitaani, nitawafuata mbegani, wapo kule.
Sato umewapata wapi
 
Ndugu zanguni nahitaji vizimba vya namna hii (angalia picha hapo chini);
1. Naweza kuvipata kwa urahisi kwa kuagiza kutoka nchi gani?
2. Bei yake ikoje?

Cage1.jpg

Cage2.jpg

Cage3.jpg
 
Hii kitu itakuwa hailipi mkuu. Ndiyo maana tangu 2010 watu wanaelezea matamanio yao tuuuu ya kufuga lkn hatuoni shuhuda za mafanikio. Washauri Ni weeeengi hatari.

Waliowahi kuingia field hii wanasema ufugaji wa samaki usikie tu. Kuna changamoto lukuki. Kulana zenyewe kwa zenyewe, unalisha miezi 6 lkn size haiongezeki, samaki kunuka tope na hivyo kukataliwa na wateja, magonjwa, udongo kuwa na madini sumu yanayouwa ama kudumaza samaki n.k

Ndiyo maana humu huoni mamilionea wakiibuka kupitia ufugaji wa samaki.

Imagine tangu 2010 ni swaga tuuuu.
Fugia ziwani ndugu, achana na mabwawa
 
Back
Top Bottom