Hodi humu wadau.
Nataka kuingia kwenye ufugaji wa samaki aina ya sato.
Eneo ninalo la kutosha, ni uwezo wangu tu wa kutengeneza mabwawa.
Maji ninayo, nimechimba kisima kwa kutoboa kwa mtambo (drill).
Naomba ushauri kwa kuanzia nikitaka kuchimba mabwawa mawili, kila moja litakuwa na ukubwa wa 250m[SUP]2 [/SUP](urefu mita 10 na upana mita 25). Jumla mabwawa mawii yatakuwa na ukubwa wa mita za mraba 500. nitahitaji mtaji wa shs ngapi kwa ajili ya kuchimba hayo mabwawa mawili, kujengea, kuweka fence kuzuia nyoka, ndege, vyura, kenge na wadudu wengine waharibifu. Ningependa kupata picha kamili at least hatua ya mabwawa hayo kukamilika ujenzi ninahitaji mtaji wa sh ngapi kwa makadirio.
Nikikamilisha nitaenda awamu ya pili kutafuta bajet ya vifaranga na chakula, hainiumizi akili hiyo.